Wito kwa Watanzania kumfata Sheikh wetu Ponda Issa Ponda kwa kukiunga mkono chama cha ACT wazalendo

Sheikh kwani kidini uchaguzi wa hizi serikali zetu ni halali?
 
Hapo kichwani sijui umejaza nini maalim, even your thoughts need a GPS to find each other.
 
Kwa hiyo ninyi MSI na dini ndio mna haki ya kufata matakwa yenu ndugu.

Hebu rejea maudhui makuu ya andiko langu.

kila watu tabaka ni jukwaa la mabadiliko. Iwe chama, iwe dini.

Lengo ni kumuondoa mkoloni kwa kila jukwaa kutumia matakwa yao ilimradi tu hatuunji katiba.

Kama huundi mkono usinizuie.

Hakuna abaetangaza kuuwa, bali tunapigania kujitoa ktk lakucha ya wale wanaobagua, walevi, watekaji, wasagaji waliojificha ndani ya ccm
 
Sijapendekeza lolote kati ya uliyoorodhesha. Langu ni kuelewesha tu kuwa dini unayoishadidia, uislamu au ukristu, ni matokeo hasi ya utumwa na ukoloni. Ni ajali ya kihistoria na kijiografia. Wala wewe kuwa muislamu au mkristu halikuwa chaguo lako bali umejikuta tu umezaliwa na wazazi waliojikuta ni waislamu/wakristo kwa sababu nilizozitaja. Hivyo tutulize vichwa tutafute namna ya kujikomboa kutoka utumwa huu wa kifikra, tujitambue kama waafrika/watanzania na si kwa lebo ya uislamu/ukristo waliotuwekea wazungu na waarabu. Kamwe waarabu au wazungu hawatatuona kuwa ni wenzao kwa kujivika imani zao. Ukitaka kuthibitisha hili jaribu kubisha hodi kwa nyumba ya mwarabu siku ya Idd au Maulid uwaeleze kuwa wawe ni muislam mwenzao
 
Takbiiiiiiirrrrrr!!!
 
Nimekuelewa kuwa Ujamaa, Ubepari, Usekyula ni dhana si za kwetu tumeletewa na wazungu.

Kwa maana turudi kwenye ujumla ili turejee kwenye asili yetu.

My friend. Kuna maneno yamezoeleka kutamkwa kwa jamii. Ikiwemo neno Udini, dini tumeletewa. Na kuna maneno hatujazoea kuyatamka. Na yakiletwa huwa ni kama nuru. Akili haipokei kwa haraka. Kama vile ukipigwa nuru ukiwa ktk giza.

Neno Dini kwa tz ni kama jinai. Lkn ukisoma katiba hiki nilichosema si kosa ya jinai wala madai. Kwani dini ni imani, mama vile Ujamaa ni imani.

Na hakuna mtu aweza kuishi bila imani. Swali la msingi je tuna imani ambayo ni universal? Kama taifa. Kama hakuna kwanini sasa matakwa yako kulazimisha kuwa ndio mwongozo wa nchi.

Kwa muda mrefu tumekuwa ccm wanatumazimisha imani ya Ujamaa iwe ndio imani ya nchi.

Lkn moja ya matakwa ya imani hii ya Ujamaa (marxi) inasema ili tupate maendeleo tunapaswa kukubali kuwa Mungu hayopo. Na kwamba dini ni uratibu. Je imani hii ni universal.

Sasa mimi sitaki kwenda huko. Bali matakwa yangu au yetu ni kutaka kukiondoa chama cha Mapinduzi kwa kutumia watu ambao hawaamini, si mlevi, si mzinzi atuelekeze njia ya kuiondoa ccm. Kwanini iwe UCHURO.
 
Hii comment imeonyesha jinsi ulivyo na akili ndogo
Ujamaa unauhusiano gani na uislamu au ubepari sababu kinyume cha ujamaa ni ubepari

Ukiangalia ukarimu wa dini ya kislamu unaendana na ujamaa kuliko ubepari
Iweje leo ujamaa uwe mbaya kwa uislamu

Tanzania viongozi ni mabilionea unasema ni wajamaa
 
Kwa hiyo chadema kutoteuwa wajumbe wa kamati kuu waislam ni ubaguzi? Achilia mbali wale waliochaguliwa kwa kuwa ni wazanzibar

..sio kweli.

..Mwenyekiti wa Taifa Bawacha ni Muislamu.

..pia kuna Mjumbe wa Kamati Kuu wa kuteuliwa na Mwenyekiti ni Muislamu.

..Chadema hakuna Udini pale, ni suala la mhusika kuwa tayari kukabiliana na mateso ya vyombo vya dola, mahakama, na msajili.

..Hata Shekhe Ponda alipowataka Waislamu wamchague Lissu mwaka 2020 alijua chama hicho hakibagui.
 
Pata somo kidogo.

Imani na itikadi ya Ujamaa inaendelea kutawala. Lkn uchumi wa kijamaa ndio umekufa, umeshindwa.

Ndio maana waona serikali inaongozwa kiimla.

Sasa ni kweli Ujamaa na Uislam unafanana sana.

Tofauti iliopo ni ktk itikadi. Wakati Ujamaa unaamini hakuna Mungu, hivyo kila kitu tunamalizana tukiwa hai. Uislam unaamini Uwepo wa Mungu.

Hivyo hata serikali tutakayoioendekeza chini ya ACT ni Taifa Moja, Imani zote, Chini ya Mungu
 
Mwenyekiti bawacha coincides ni Muislam. Lkn walichaguliwa kwasababu ni Mzanzibar
 
Na inshallah aanguke mweleka wa mende tena kwa pua. Aaamin.
 
Mwenyekiti bawacha coincides ni Muislam. Lkn walichaguliwa kwasababu ni Mzanzibar

..hapana.

..yule Mama Muislamu kawashinda vigogo haswa wa Chadema akiwemo Susan Kiwanga, na mgombea aliyetangaza wazi kuwa anamuunga mkono Tundu Lissu.

..Chadema hakuna udini, unachohitaji ni utayari wa kuvumilia mateso na dhuluma toka jeshi la Polisi, Usalama, Msajili, na Mahakama.

..Na Lissu ndiye mgombea Uraisi pekee aliyewatetea Mashekhe wa Answar Sunna, Uamsho, pamoja na Wazanzibari waliouwawa toka zama za Sheikh Abeid Karume.
 
Nimekuelewa. Kwahiyo yule dada yetu walichaguliwa kwa kura. Hoja yangu ni nafasi za teuzi za kamati kuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…