The Phylosopher
JF-Expert Member
- Mar 11, 2015
- 1,968
- 2,957
Sijui kama ni makusudi au uvivu wa kufikiri, au kuamua kuishi kwa mazoea. Kila mwaka baraza la mitihani wanakuja na majina ya wanafunzi na shule bora katika matokeo ya mitihani ya ngazi tofauti.
Kinachosikitisha ni kwamba kuna utofauti mkubwa sana wa mazingira ya utoaji elimu hapa nchini, hali hiyo ya utofauti wa mazingira kwa sehemu kubwa huathiri matokeo ya wanafunzi.
Hili jambo liko wazi sana kwani ukipita kwenye shule zetu utajionea utofauti mkubwa sana wa namna hali halisi ilivyo. Mf kuna shule ambazo unakuta shule ina kila kitu anachohitaji mwanafunzi, yaani idadi ya wanafunzi kwa darasa25-35 maabara yenye kila kitu, madawati ya kutosha, maktaba, waalimu wanapata kila kitu na motisha juu pamoja na wafanyakazi wengine wa kutosha.
Eti unachukua hiyo shule unataka uishindanishe na shule kama ya Goba ambayo dalasa la nne pekee kuna wanafunzi 400, hakuna cha maabara wala maktaba hao waalimu Wana madai na malalamiko hayasemeki.
Ni wazi kwamba hapo hakuna ushindani, ni sawa na kumchukua mtu ukamnyima chakula siku tano halafu unataka akapambane na bondia, kisha akipigwa uanze kumzomea na kumsifu bondia hii sio sawa.
Kama nia ni kuinua hamasa, basi hizi shule zishindanishwe kimakundi ili kila mtu au shule ishinde katika kundi la wenzie wanaofanana mazingira ya utoaji elimu.