The Phylosopher
JF-Expert Member
- Mar 11, 2015
- 1,968
- 2,957
- Thread starter
- #21
Mfano uliotoa hauna uhalisia katika hoja iliyoko mezani maana kwa mfano huo na mimi ningekuuliza kwa nini mabondia hupima uzito kabla ya hupambana?Hebu fikiria TFF iamue simba, yanga na azam Kwa kuwa zina viwanja vizuri, pesa, na wachezaji professional washindanishwe wao kwa wao, halafu timu zilizobakia 13 ambazo hazima ukwasi kama simba, yanga, na azam nazo zishindanishwe zenyewe kwa zenyewe kwenye ligi hiyo hiyo. Unafikiri ni nini kitatokea kwa mpira wa Tanzania?
Huu utaratibu unaotumiwa sasa unawadhalilisha waalimu na wanafunzi ambao husoma katika mazingira magumu sana ambapo serikali ilipaswa kuwawezesha lakini imeshindwa alafu anakuja waziri au kiongozi anawafokea waalimu na wanafunzi kana kwamba hawana akili au ni wazembe.