Wito kwa Waziri wa Elimu: Shule zishindanishwe/zitengwe kulingana na mazingira ya utoaji elimu

Mfano uliotoa hauna uhalisia katika hoja iliyoko mezani maana kwa mfano huo na mimi ningekuuliza kwa nini mabondia hupima uzito kabla ya hupambana?

Huu utaratibu unaotumiwa sasa unawadhalilisha waalimu na wanafunzi ambao husoma katika mazingira magumu sana ambapo serikali ilipaswa kuwawezesha lakini imeshindwa alafu anakuja waziri au kiongozi anawafokea waalimu na wanafunzi kana kwamba hawana akili au ni wazembe.
 
 
Huku kibondo s/m Busunzu B la nne pekee ina wanafunzi 800.
Yap hata hapa dar kuna shule inaitwa muhimbili 2 ina waalimu 4 tu lakini ina madalasa kuanzia chekechea hadi la saba. Na shule za aina hii zipo nyingi sana. Kinachoumiza ni kwamba waalimu na wanafunzi wa shule hizi husimangwa kwa maneno makali na kejeli za kila aina, hii sio sawa kabisa
 
Wakiongoza akina Mzumbe na Ilboru, hamlalamiki. Shida inakuja wakiongoza akina St. Naniliu.
Hapa tatizo sio kashinda nani tunahitaji fair competition yaani kwa ilivyo sasa hakuna kiongozi anayeweza kupeleke watoto wake wakasome kwenye hizi shule kwa kuwa wanajua hazikidhi vigezo.
 
U
Umeongea ukweli mtupu umchukue taazan umshindanishe na mwanafunzi Wa goba kwanza watoto wetu wanasema kunamaswali mengune wanayakuta sikuyamtihani tu shuleni hawajawahi kupewa mbenu yakujibu maswali ya aina ile wanadai waliofundishwa huwa wanayajibu vizuri elimu maututi ipotaabani Tanzania
 
Mbona Baraza wamepetenganisha,Kuna zile zenye candidates zaidi ya 40 na zile zenye candidates 40 kushuka chini
 
Olimpio darasa la Nne walikuwa 720 lakini Wana ufaulu mzuri kuliko private nyingi na olimpio ni ya serikali.Ungepebdekeza serikali ibireshe mazingira ya shule zake.sio kupanua goli
 
Mimi sioni sababu ya kutenganisha, kinachohitajika ni shule zisizo perform vizuri zinatakiwa kuweka efforts zifaufaulu. Yaani watu badala ya kupiga kelele watoto wetu wote wafaulu vizuri nyie mnataka another form of assessments,hamuoni hii ndio italeta ubaguzi wa matabaka zaidi??? .....
 
Vipi ukizongatia kigezo Cha idadi? Maana Kuna kigezo Cha Above 45 na below 45.
Sasa Kuna shule za sekondari huko Itimbili Ina wanafunzi form four hawazidi 40 lakini matokea yao still ni mabovu. St. Fransis walikuwa na wanafunzi 63 ,madarasa 2.kemeboys wanafunzi 92 wastani madarasa matatu. Kuna shule ya serikali Ina wanafunzi 413 wa form four tu. Walimu wa form four hata 12 hawafiki. Unatarajia Nini?
Serikali iajiri walimu wa kutosha.
 
Olimpio darasa la Nne walikuwa 720 lakini Wana ufaulu mzuri kuliko private nyingi na olimpio ni ya serikali.Ungepebdekeza serikali ibireshe mazingira ya shule zake.sio kupanua goli
Aisee kumbe olimpio ni ya serikali, ndo najua leo
 
Nakibali kabisa. Shule kumi bora katika kufelisha, zichunguzwe, zisaidiwe Ili zikuze ufaulu mwaka unaofuata. Shule za Zanzibar huwa zinafanya vibaya Sana. Sijajua shida ni Nini hasa
 
Tatizo linaanzia hapa, Kipaumbele ni kwenye mashindano na sio uelewa kufundisha....

Hii inapelekea wanafunzi kukariri, kudanganya na kulenga mitihani na sio uelewa; ili mradi tu wawe na matokeo mazuri

Kipimo cha kufundisha ni kumtoa mtu hatua moja mpaka nyingine hivyo unaweza ukamtoa mtu kwenye point 7 mpaka kwenye point 14 na mwingine ukamtoa kwenye zero mpaka kwenye three

Sasa unadhani ukitenga makundi ni mzazi gani atapenda mtoto wake apelekwe kwenye kundi D; au ni shule gani haitadanganya ili kwenye kundi A
 
Naomba tuliza akili yako mkuu dhida iliyopo ni kukosekana kwa usawa wa huduma na mahitaji ya lazima katika baadhi ya shule huku zingine zikitoshelezwa kwa kiwango kikubwa na serikali hiyohiyo.

Kana kwamba haijui chochote serikali hiyo hiyo inaanza kuwachimba mkwara kuwaharasi na kuwashusha vyeo wale ambao shule zao hazikufanya vzr.
 
Olimpio darasa la Nne walikuwa 720 lakini Wana ufaulu mzuri kuliko private nyingi na olimpio ni ya serikali.Ungepebdekeza serikali ibireshe mazingira ya shule zake.sio kupanua goli
Sasa wewe unaitaja olimpio kwani ina tofauti gani navshuleza private? Shule ambayo macho yote ya serikali yako hapo hizi ndio miongoni mwa shule hupewa upendeleo katika kuzipatia mahitaji yake.
 
1.Serikali inamiliki shule zenye mazingira magumu sana.
Na
2. Serikali hiyohiyo ndiyo inatoa mitihani!!!!


Serikali iboreshe mazingira ya shule zake.
 
Swala la elimu ni mfupa mgumu uliotushinda toka kitambo.kinachofanyika ni kuulamba lamba tu na kuuacha hapo.Hatujawa tayari kuupasua na kusuka upya elimu yetu.mawazo ya wadau mbalimbali yameshatolewa miaka na miaka ila bado hatujui tatizo ni nini hadi tunakosa uamuzi wakusuka upya hii sekta.Mawazo yako yanaweza kua sawa ila hayawezi kua mwarobaini wa changamoto nyingi za sekta ya elimu.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Kuna shule darasa halizidi wanafunzi 18, wataachaje kufaulishwa...
 
Nia mnataka shule za serikali nazo ziwe zimeongozaa maana sahivi zinapigwa mbaya sana🙂

Kama hoja ndo hiyo, pia waangalie vipato wa familia masikini wapunguziwe grade zao mtu aliyetoka familia masikini akipata four ya 30 aendelee form six maana wa familia njema anapata kila kitu.
 
Mtoa mada ana akili,lkn wachangiaji hasa wa5 wa mwanzo hawana akili.just to say shule za kata ya kwanza ni.... Shule za seminari ya kwanza ni. .......etc etc etc.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…