Kabla hujapost video ya Jay, ulionywa sana na wadau wako wa Instagram kwamba kupost video ya mgonjwa si Jambo jema, lakini ukakaidi, ukapost.
Alipoku Waziri Mkuu Peter Pinda alisema kama umeonywa na umekaidi, upigwe TU.
Ndivyo ilivyokuwa kwako, umeonywa, umekaidi kichapo kiwe juu yako.
Kama asiye funzwa na mamaye hufunzwa na ulimwengu, na sis walimwengu wa taifa hili tumechoshwa na tabia zako za hovyo za kushambulia utu wa watu, kuingilia Uhuru wao wa faragha, kuwatukana, kuwadhalilisha na kuwatendea kila ubaya.
MangeKimambi, Mungu hayupo likizo, na amesikia kilio Cha muda mrefu. Machozi ya Watanzania wengi walio umizwa na wewe yamefika kwenye kiti cha enzi.
NI wakati wako sasa kutubu na kuomba msamaha.
Ivumayo haidumu, ngoma ikilia sana mwisho wake NI kupasuka