Wito wangu kwa Wanawake: Achaneni kabisa na usafiri wa bodaboda, sio salama kwenu

Wito wangu kwa Wanawake: Achaneni kabisa na usafiri wa bodaboda, sio salama kwenu

Ushauri wangu kwa serikali bodaboda nazo zipunguzwe, kama wanavyo dili na machinga sasa wageukie na boda boda nazo.
Kwanza ni hatarishi, wanao ziendesha wengi wao hawastahili, zimekuwa nyingi mno mjini, zinasababisha msongamano mkubwa na mengine mengi ambayo yanasababisha kuwepo na sababu ya boda boda kuondolewa au kupunguzwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Wangepumguza ushuru wa bajaj angalau ziwe nyingi na bei poa...
 
calculation zao za kukatiza mataaaa, huwa zinaniwazisha sanaaa,

wanapo gongana wao kwa waoo ndo tenaaa wabaki ukiwaza

Wito - abiria usimruhusu dereva boda boda avuke mataa endapo taa haziruhusu
Mimi akinibeba ni marufuku kukatiza
Mataa ikiwa red hata kama hakuna magari, pia akipiga overtake za kipimbi na akawa hasikii nashuka zangu fasta...
 
ukisoma tu huu uzi hapa utagundua watu wengi sana wamekufa kupitia hizi bodaboda na wengi sana wamepata ulemavu kwa kusoma tu huu uzi...
Boda boda ni chinja chinja. Shime wandugu, kama unaweza tumia usafiri mwingine please tumia ili kuepusha majanga.
 
Kwanini hutumii simbank au nenda kwa wakala sio lazima ufike bank

Sent using Jamii Forums mobile app

Uko sahihi mkuu, lakini hiyo bank wana matawi machache sana ( Arusha, Mwanza na DSM) hapa DSM kwenyewe wamebaki na tawi moja tu.

Pia wakati huo kiwango cha juu cha kuweka pesa kwa siku ilikua 3M, mie nilikua na muamala wa kuzidi hiyo pesa.
Niliposhuka airport muda ulibaki mdogo sana benki zifungwe, nikaona bodaboda ataniwahisha. Ila advertise zake mbili tu zilitosha kunifanya niairishe hilo jambo hadi kesho yake.
 
Majuzi nilichoka maeneo fulani namuona mdada yupo kwenye boda boda huku anachati.

Uwiii. Nilimshangaa kwa kweli mana hana hata habari yaani.
 
Just imagine ndiyo kamtoko hivii, umetia kalkiti yako, na ka way pembeni anaelewa Depal ile namna, nywele inameremeta hivii, dereva anakupa helmet lake chafu utavaa..?
Sasa na wewe muda huo si urequest bolt au ubber gari tu.
 
Nilishuhudia mdada pale flyover za ubungo mdada yupo kwenye bodaboda amekaa kiupande kama kawaida yao. Yule boda akaminya break ya ghafla yule dada anatoka mzima mzima kutokea juu ya flyover adi down. Lol alifariki palepale, mdada mrembo hakupata ata nafasi ya kulia
Ayayayaya hii ajali naikumbuka. Mwaka jana au mwaka juzi kama sikosei. Daah!
Halafu kesho yake natoka Goba nipo kwenye bajaji namsikia mama niliyepanda naye anawapa taarifa ndugu juu ya msiba kumuuliza ananielezea. Nikamwambia niliishuhudia hiyo ajali. Huyo mama alikua mama mdogo wa binti. Inasikitishana sana. Akaniambia ndio amemaliza chuo. Noma sana mauti haya!
 
Ayayayaya hii ajali naikumbuka. Mwaka jana au mwaka juzi kama sikosei. Daah!
Halafu kesho yake natoka Goba nipo kwenye bajaji namsikia mama niliyepanda naye anawapa taarifa ndugu juu ya msiba kumuuliza ananielezea. Nikamwambia niliishuhudia hiyo ajali. Huyo mama alikua mama mdogo wa binti. Inasikitishana sana. Akaniambia ndio amemaliza chuo. Noma sana mauti haya!
Hakuna kitu mabinti hujisikia kama kukalia kiti cha bodaboda! Akikaa mkao wa kujibinua na huku anachati! haumwambii kitu maamuzi yote humuachia dereva.
 
Na pia kina dada waache uvivu, kasafari ka hapa na hapo tu anataka boda. Zimewalemaza sana na kufanya kuzitumia kwa vijisafari hata vya mtaa na mtaa.
 
Back
Top Bottom