DOKEZO Wizara ya Afya, Je, kuna mlipuko wa ugonjwa wa macho?

DOKEZO Wizara ya Afya, Je, kuna mlipuko wa ugonjwa wa macho?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Jibu: NDIO

Mkuu hili suala lililopo sio shida ya uoni kama ilivyoelezwa kwenye maelezo hayo ya WHO
 
Namimi niko vibaya sana tangu mwaka jana mwezi wa nane mpaka sasahivi macho yananitesa sana, kuna wakati yanapeana zamu, wakati mwingne yanawasha yote kwa pamoja dah. Niko geita
 
Mkuu hili suala lililopo sio shida ya uoni kama ilivyoelezwa kwenye maelezo hayo ya WHO
Naelewa sio Uoni..Kuna aina ya mlipuko wa homa ya macho..Mara nyingi hutokea maeneo ya Kanda ya ziwa au Mikoa yenye Ziwa..Homa hii inaathiri jicho moja..linakua jekundu na Linawasha husababishwa na Bacteria wasafirishwao kwa hewa(Airbourne disease) hivyo maambukizi yake ni rahisi kama kuambukizana Mafua..Mara nyingi inaisha ndani ya muda mchache hudumu kwa wiki 1 au mbili
 
Habari wana JF poleni na majukumu ya kazi na pirikapirika za January hii....

Naomba niende kwenye point ya kukumbushana kuhusu yanayojiri Huku mitaani na Masokoni ambapo wengi wetu tunasaka ridhiki zetu huko

Kumekuwa na ugonjwa mpya wa Macho ambao muathiriwa anakuwa anatokwa na Machozi huku macho yakibadilika rangi na kwa ya rangi nyekundu mithiri ya mtu anayetumia sigara kubwa pia huambatana na kutokwa na uchafu sehemu ya Macho

Hii ni hatari huku mtaani tumeanza kuwa na mashaka kiasi cha kutoaminiana katika kutizamana katika nyuso. Hii ni hatari kwa hapa Mjini.

Mamlaka fuatilieni mapema kabla halijawa janga kamili.

Nawasilisha.
 
Inaitwa Red Eye na inakuwepo kwa msimu. Ile inaambukiza hasa kwa wenye makundi Sawa ya damu. Kwa watoto wanapona haraka Sana ndani ya siku 2-3 Ila mtu mzima wengine wiki na zaidi. Macho yanauma mchangamchanga ndani na Mwanga ni Shida kuangalia. Machozi ya Uhakika. Tiba asili ni kuosha macho na maji ya vuguvugu uliyoweka chumvi kidogo.
 
Huwezi amini nmeisoma hii heading na kumpasia simu rafiki yangu ambaye tangu jana tunahangaika na tatizo hili.

Na sijachukua precautions zozote kwa hiyo kama ni kuambukizwa basi i'm the next.
 
Inaitwa Red Eye na inakuwepo kwa msimu. Ile inaambukiza hasa kwa wenye makundi Sawa ya damu. Kwa watoto wanapona haraka Sana ndani ya siku 2-3 Ila mtu mzima wengine wiki na zaidi. Macho yanauma mchangamchanga ndani na Mwanga ni Shida kuangalia. Machozi ya Uhakika. Tiba asili ni kuosha macho na maji ya vuguvugu uliyoweka chumvi kidogo.
𝐡𝐚𝐤𝐢𝐤𝐚𝐚
 
Back
Top Bottom