DOKEZO Wizara ya Afya, Je, kuna mlipuko wa ugonjwa wa macho?

DOKEZO Wizara ya Afya, Je, kuna mlipuko wa ugonjwa wa macho?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Screenshot_20240114-102933_Instagram.jpg
Toka insta huko..,
 
red.jpg


TAHADHARI KUHUSU UGONJWA WA MACHO (VIRAL CONJUNCTIVITIS)

Kwa siku za karibuni kumekuwa na ongezeko la wagonjwa wanaumwa ugonjwa wa macho ‘viral conjunctivitis’ hasa wanafunzi.

MAAMBUKIZI

Ugonjwa guu husababishwa na virusi na unaambukizwa kutoka kwa mtu anayeumwa macho kwenda kwa mtu mwingine kwa nja zifuatazo;
  • Kushikana mikono na mtu mwenye ugonjwa huo bila kunawa mikono ukijigusa sehemu za uso na machouna hatari ya kupata maambukizi,
  • Kugusa vitu kama kalamu, simu, kompyuta, daftari, vitabu, vitasana vitu vingine vinavyochafuka na majimaji ya macho (machozi) kutoka kwa mgonjwa anayeumwa ugonjwa huo,
DALILI
  • Macho kuwasha na kutoa machozi kupita kiasi,
  • Maumivu ya macho, kichwa, mafua na kuvimba kpe,
  • Macho kubadilika rangi na kuwa mekundu na
  • Kushindwa kuangalia sehemu yenye mwanga.
NAMNA YA KUJINGA
  • Kunawa mikono mara kwa mara kwa maji tiririka na sabuni au kutumia vitakasa mikono (sanitizers),
  • Unapokuw aumepata maambukizi unashauriwa kunawa uso na maji tiririka pekee mara kwa mara,
  • Kutofikicha macho ili kuepuka madhara zaidi,
  • Epuka kushikana mikono na kuchangia matumizi ya vitu mbalimbali kama simu, kompyuta, na vitu vingine kama hakuna ulazima.
ZINGATIA

Ripoti Kituo cha Afya kwa msaada zaidi ukiwa na dalili za ungonjwa huu.
 
Ndio maana wazungu wakiwa huku wanatinga sana eyeglasses...

Na wabongo wanaovaa tunawaona kama Mabishoo ila ina umuhimu sana hasa katika kuzuia vumbi na moshi mchafu kuingia machoni

Tuwe na desturi hiyo hasa kwa nchi zetu hizi masikini zenye vumbi na moshi kila kona
 
Wale waliosoma same 2015, huu ugonjwa ulitukamata tena ilikuwa kipindi Cha paper la necta form 6 2015
Jicho linaiva kama nyanya daah
Tulikuwa tunasema aliepata amekojolewa na nairobi fry
 
Mimi ni mkazi wa mwanza buzuruga yani hii shida ya macho(Red Eyes) saiv imeshanichukua takribani miaka miwili na nilishatumia dawa tofauti za macho lakin hamna kilichonisaidia na kuna muda inafika nikiamka asubuhi napatwa hali ya ukungu then baada ya muda hali inakaa sawa. Kama kuna dawa wataalamu wanisaidie maana hii hali inanitesa sana
 
Huu ugonjwa hatari sana nimesafiri nikiwa sina nafika huku kwa watu ndo unajionesha
 
Back
Top Bottom