TAHADHARI KUHUSU UGONJWA WA MACHO (VIRAL CONJUNCTIVITIS)
Kwa siku za karibuni kumekuwa na ongezeko la wagonjwa wanaumwa ugonjwa wa macho ‘viral conjunctivitis’ hasa wanafunzi.
MAAMBUKIZI
Ugonjwa guu husababishwa na virusi na unaambukizwa kutoka kwa mtu anayeumwa macho kwenda kwa mtu mwingine kwa nja zifuatazo;
Kushikana mikono na mtu mwenye ugonjwa huo bila kunawa mikono ukijigusa sehemu za uso na machouna hatari ya kupata maambukizi,
Kugusa vitu kama kalamu, simu, kompyuta, daftari, vitabu, vitasana vitu vingine vinavyochafuka na majimaji ya macho (machozi) kutoka kwa mgonjwa anayeumwa ugonjwa huo,
DALILI
Macho kuwasha na kutoa machozi kupita kiasi,
Maumivu ya macho, kichwa, mafua na kuvimba kpe,
Macho kubadilika rangi na kuwa mekundu na
Kushindwa kuangalia sehemu yenye mwanga.
NAMNA YA KUJINGA
Kunawa mikono mara kwa mara kwa maji tiririka na sabuni au kutumia vitakasa mikono (sanitizers),
Unapokuw aumepata maambukizi unashauriwa kunawa uso na maji tiririka pekee mara kwa mara,
Kutofikicha macho ili kuepuka madhara zaidi,
Epuka kushikana mikono na kuchangia matumizi ya vitu mbalimbali kama simu, kompyuta, na vitu vingine kama hakuna ulazima.
ZINGATIA
Ripoti Kituo cha Afya kwa msaada zaidi ukiwa na dalili za ungonjwa huu.
Wale waliosoma same 2015, huu ugonjwa ulitukamata tena ilikuwa kipindi Cha paper la necta form 6 2015
Jicho linaiva kama nyanya daah
Tulikuwa tunasema aliepata amekojolewa na nairobi fry
Mimi ni mkazi wa mwanza buzuruga yani hii shida ya macho(Red Eyes) saiv imeshanichukua takribani miaka miwili na nilishatumia dawa tofauti za macho lakin hamna kilichonisaidia na kuna muda inafika nikiamka asubuhi napatwa hali ya ukungu then baada ya muda hali inakaa sawa. Kama kuna dawa wataalamu wanisaidie maana hii hali inanitesa sana