Wizara ya Afya waanza kampeni ya kumsafisha Hayati Magufuli

ngebe

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2020
Posts
1,789
Reaction score
5,117
Maneno aliyokua anayaongea hayati na kuwakalilisha wananchi wake, sasa imekua ngumu kwa Wananchi kuelewa kila ukiwaambia kitu utasikia Mbn Magufuli alisema hivi, mbn Magufuli alisema vile!

Wananchi wamekua wagumu kuvaa Barakoa Hongera Wizara ya Afya kwa kutoa Elimu Mujarab

IMG_20210623_185550.png
 
... duh! Ukisikia U-turn ndio kama hivi sasa! Alisisitiza watu wavae barakoa za kushona mbona yeye hakuwahi kuzivaa ili kuonesha mfano! Kuhusu Corona wakubali tu kwamba alichemka.
 
Lazima tutafute utaratibu wa kudhibiti viongozi, Mwendazake alivuruga kabisa hili swala la Corona, huwezi kuwalaumu Watanzania kugeuka matomaso, haiwezekani serikali inageuka geuka namna hii, washike lipi.

Yule yule Madam Gwajima aliyetamba kuishinda Corona, leo anataka watu waanza kuvaa barakoa!! Rais alipaswa kuondoa uongozi wote wa Wizara ya Afya kwanza, hawana moral authority ya kuwaambia watu wachukue tahadhari ya Corona.
 
Na alisema iko kama titi moja hivi!?
Hivi kama ile ya madaktari bado inaambukiza
Je hizi za kushona tena za vitamba vya masisiemu itakuaje?
Tatizo la korona haibezwi
Itakukula fasta kama alivyoliwa yule mtu
Sijui huko aliko kama anaendelea kuibeza
 
Ukweli ni kwamba watu tuliaminishwa kuwa Tanzania hakuna korona na kuhusu kujikinga kwa barakoa tuliaminishwa barakoa zina korona,hivyo kwa serikali hii baada ya kubadilisha gia angani wanapata shida sana kuelimisha watu kuhusu kujikinga,ndio maana mtaani watu tupo tupo tu na ukimwona mtu kavaa barakoa tunamshangaa,ndio maana kwa sasa wizara wanajaribu kurejea maneno ya mwenda zake kwa sehemu alizo jaribu kuhimiza watu kuchukua taadhari ya kujikinga na korona,wanajaribu kumtumia kwa vile yeye ndiye aliye tufanya tuamini hakuna korona.ukweli ni kwamba mzee alituondoa hofu kiasi kilichopitiliza
 
Lazima tutafute utaratibu wa kudhibiti viongozi, Mwendazake alivuruga kabisa hili swala la Corona, huwezi kuwalaumu Watanzania kugeuka matomaso, haiwezekani serikali inageuka geuka namna hii, washike lipi.

Yule yule Madam Gwajima aliyetamba kuishinda Corona, leo anataka watu waanza kuvaa barakoa!! Rais alipaswa kuondoa uongozi wote wa Wizara ya Afya kwanza, hawana moral authority ya kuwaambia watu wachukue tahadhari ya Corona.
Watanzania wengi mno ni wanafiki wakubwa, na hata sasa wote mnaobwatuka humu, barakoa hamvai!! ni unafiki tu wa kijinga na kulaumu wengine wakati hata wewe hapo ulipo, huna barakoa wala huzingatii chochote, ajabu zaidi, upo, na korona hupati
 
Ukweli ni kwamba watu tuliaminishwa kuwa Tanzania hakuna korona na kuhusu kujikinga kwa barakoa tuliaminishwa barakoa zina korona,hivyo kwa serikali hii baada ya kubadilisha gia angani wanapata shida sana kuelimisha watu kuhusu kujikinga,ndio maana mtaani watu tupo tupo tu na ukimwona mtu kavaa barakoa tunamshangaa,ndio maana kwa sasa wizara wanajaribu kurejea maneno ya mwenda zake kwa sehemu alizo jaribu kuhimiza watu kuchukua taadhari ya kujikinga na korona,wanajaribu kumtumia kwa vile yeye ndiye aliye tufanya tuamini hakuna korona.ukweli ni kwamba mzee alituondoa hofu kiasi kilichopitiliza
Sio tuliaminishwa, Bali ni ukweli kwamba, Zipo nchi ambazo ziliagiza barakoa ktoka nchi zingine, baada ya kufikishwa zilionekana kuwa na virusi vya Corona

mf, Us aliagiza barakoa kutoka uchina, tuliona kwa macho yetu, zikirudishwa

Ni kwa nini mtu useme waliaminishwa na wakati ni kweli kulionekana kuwepo barakoa zenye virusi?
 
Maneno aliyokua anayaongea hayati na kuwakalilisha wananchi wake, sasa imekua ngumu kwa Wananchi kuelewa kila ukiwaambia kitu utasikia Mbn Magufuli alisema hivi, mbn Magufuli alisema vile!

Wananchi wamekua wagumu kuvaa Barakoa Hongera wizara Ya Afya kwa View attachment 1827811kutoa Elimu Mujarab
Hili tangazo kiboko Kila mahali magufuli.muacheni baba wa watu apumue Tena msimshirikishe Corona yenu kabisa
 
Back
Top Bottom