Wizara ya Afya waanza kampeni ya kumsafisha Hayati Magufuli

Mungu hapendi watu vuguvugu - leo uko kanisani unakula mkate na divai, kesho unatuma wasiojulika kuteka watu... Huyo alikuwa gent wa shetani tu. Kama Mungu aliisaidia Tanzania ni kwa sababu ya maombi ya Watanzania wengine. Siyo Magufuli.
 
Watanzania wengi mno ni wanafiki wakubwa, na hata sasa wote mnaobwatuka humu, barakoa hamvai!! ni unafiki tu wa kijinga na kulaumu wengine wakati hata wewe hapo ulipo, huna barakoa wala huzingatii chochote, ajabu zaidi, upo, na korona hupati
Mkuu jikite kwenye issues sio personalities
 
Mkuu Tanzania ni kubwa kuliko Magufuli. Serikali lazima ilinde hadhi yake bila kujali nani ni Rais wa wakati huo. Hizi mbinu zake za kishirikina za kupambana na Corona ndio zinaleta shida sasa kwa Serikali sasa.
 
Watajijuwa mie na familia yangu najikinga
Mkuu usijidanganye kabisa Corona ni tofauti sana na HIV, hii nikuomba kila mtu ajikinge,jamii ikichafuka lazima uipate maana inaambukizwa naweza sema kizembe sana.
Elimisha marafiki ndg na jamaa.
 
Wadudu wadogo wadogo wamekwisha maliza kazi yao. Wamebakiza mifupa tu...

Ungekua na elimu ya uhai ukajua nafasi ya mwili, roho na nafsi usingeandika ulichoandika
Ila nikuache tuu wewe muumini wa amstadam
 
Tangazo lenyewe lina makosa. Unaposema "watu kabla ya kusema chochote inabidi wajidhihirishe ndio waseme" unamaanisha kwamba hawana ulazima wa kujidhihirisha kuhusu kinachozungumzwa. Hapo maneno n "hawana budi wajidhihirishe" kuonesha kwamba wana ulazima wa kufanya hivyo.
 
Mkuu Tanzania ni kubwa kuliko Magufuli. Serikali lazima ilinde hadhi yake bila kujali nani ni Rais wa wakati huo. Hizi mbinu zake za kishirikina za kupambana na Corona ndio zinaleta shida sasa kwa Serikali sasa.
Acha utopolo wewe unazungumzia nini? TZ haina shida ya corona kama majirani zetu kwa kuwa tulikuwa makini na mbinu za kibeberu au wewe uko nje ya nchi nini? Tumefaulu sana katika kupambana na corona hakuna cha lockdown wala nini wakati majiranj zetu wamehangaika sana na bado wanahangaika sasa unataka kusema TZ hajafanya vizuri kwenye kupambana na corona?
 
Ungekuwa mtu wa imani ungekubali kuwa kazi ya Mungu haina makosa. Alazwe kwa kadiri ya matendo yake (alipojichagulia) - risasi kwa Lissu, kudukuwa maongezi ya watu, kesi za kubambikizia watu, wizi wa kura za uchaguzi 2020, kula hela ya msaada wa tetemeko, matusi ya nguoni...
Ungekua na elimu ya uhai ukajua nafasi ya mwili, roho na nafsi usingeandika ulichoandika
Ila nikuache tuu wewe muumini wa amstadam
 

Ulimuona akimpiga Tundu risasi? Rais wetu Samia alishawaambia aliyepiga zile risasi sio serikali wala aliyepiga zile risasi hawezi kuwa askari wake kamwe!

Sasa wewe ulikua unamchukia JPM siku zote nilijua ameondoka ameondoka kwa mapenzi ya Mungu roho yako imetulia. Ila sasa nashangaa Gubu na hasiraaaa zinavyokupamba moto......
Pole mwaya
 
Huu uongo, virus vinawekwaje kwenye barakoa?,wangepigana vita kali,,barakoa zilikua zinakataliwa sababu nyingine zilikua na mapungufu,,sio kwamba eti kuna watu walichota virusi na kuweka kunako barakoa,,hiyo haiwezekni
 
Tanzania kuna watu wanafiki na kwa sasa hatuaminiani!, njaa inatuponza, Magufuri hakuamini kuna Corona sababu alikuwa kwenye jumba jeupe wakati huo hakujua ana hitilafu ya afya ambayo gonjwa hilo ndilo rafiki la kuondoa uhai. Ukiwa na tatizo la blood pressure, sukari, HIV +, na hata ujauzito kwa wanawake ikikupata unaenda udongoni. Tujifunze kuacha unafiki. Oneni Viongozi wanavyobadili kauli sababu ya njaa. Mama yetu oyeeeeeee
 
Nyie vilaza ndio mnatupa tabu.... hivi unajua uchumi wetu unategemea utalii kwa kiasi gani? Unajua jinsi gani misimamo ya Magufuli imevuruga image ya nchi kwa wageni? Hakuna anayesema ije lockdown, lakini hii ya kujifanya kama hakuna tatizo ndio tatizo kubwa. Ulaya mwaka huu ukiisha wanamaliza maswala ya chanjo, unadhani ni mtalii gani atataka kwenda kwenye nchi iliyowekwa kwenye danger zone ya Corona; ambako akienda siku anarudi kwao atafungiwa ndani kwa wiki 2 mpaka 3. Au unadhani tembo na simba wako Serengeti tu?

Huyo mtukufu wenu alikuwa mshamba, asiyejua kufanya hata SWOT analysis, yeye kila kitu anaona dawa yake ni ugomvi tu.
 
JpM sio wa kuzimwa kwa mbwembwe tu uonekane utendji uliotukuka, mengine haya hayataleta impact kwetu sisi tunaotaka kuona vitu
 
Tunamshukuru Mungu kwa vile kazi yake haina makosa. Na wewe mshukuru kwa kutuondolea udhia.
 
Kwani Tanzania tuna Corona?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…