Vien
JF-Expert Member
- Mar 6, 2020
- 8,508
- 15,276
Habari wakuu wote nawasalimu
Kumekua na changamoto kwenye swala upatikanaji wa hati miliki kutoka wizarani, Kwa utaratibu uliopo ni hivi
Mtu anapotaka kumilikishwa ardhi inabidi awe na
1) Mkataba wa mauziano + Mkataba wa asili
Hii mfano kama umenunua kiwanja kutoka kwa kampuni ama mtu binafsi lazima upate mkataba wa mauziano, lakini pia mkataba wa asili pia unatakiwa, huu ni kwa ajili ya kuonyesha historia ya hilo eneo liko vipi, ili kule wizarani waweze kujiridhisha kabla ya kukumilikisha
2) Survey plan
Hii ni ramani ambayo inaonyesha hilo eneo limethibitishwa kuwa lina vigezo vyote kwa matumizi either ya makazi biashara n.k, ili uipate hii lazima hilo eneo liwe limekidhi vigezo
3) Plot no,
Pindi survey plan inapokamilika, kwa kilo kiwanja cha eneo husika huwepa no pamoja na cordnate points zinazozunguka mipaka ya kiwanja
4) Taarifa za mmilikishwaji
Hapa utahitajika uwe na Nida, passport n.k, na kuna form ya umilkishwaji utazaja ambayo inatoa tathmini nzima ya eneo unalotaka kupewa hati yake
Baada ya kukamilisha hivi vitu taarifa zote zinapelekwa mansipaa husika, baada ya taarifa kuingizwa kwenye mfumo utapewa control no ya kwanza ambayo gharama zake ni sawa kwa kila mtu kiasi ni 5000
Hiyo ni kwa ajili ya kufungua file, baada ya hapo utasubiri tena ili upate control no ya pili ambayo hii ni final na pia gharama hutofautiana kulingana na ukubwa kiwanja na mahali kiwanja kilipo
Sasa changamoto kubwa ambayo inakuja kujitokeza unaweza ukashangaa umelipa control no zote alafu ukasubiri kwa muda kupata sms ya kuwa muamala umesajiliwa lakini usipate hii sms, ukienda manispaa husika kufuatilia unakuta maombi yako yamekua rejected, Ukiuliza sababu watakuambia labda kuna document imekosekana, au saa zingine utaambiwa labda ramani haionekani vizuri n.k
Sasa mimi naona huu ni udhaifu inawezekanaje mfumo utoe control no ya final payment ikiwa document hazijakamilika,nafikiri hii changamoto wengi wamekutana nayo
Kwa uelewa wangu ilipaswa kuwa hivi, malipo ya awali ya kufungua file kiasi cha 5k, ni sawa, baada ya hapo wapitie documents za mteja kujiridhisha kama anastahili kupatiwa hati miliki, ikiwa imetokea documents hazijakamilika hayo maombi yawe rejected, lakini sio mtu analipa mpaka final payment alafu anakuja kukuta ombi limekua rejected anatakiwa aanze upya hii sio sawa kabisa.
Hili swala linaumiza sana