Wizara ya Ardhi
Govt Institution
- May 14, 2024
- 306
- 165
Jengo la Ofisi ya Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ni moja ya majengo ambayo yamesanifiwa na kujengwa kwa ubora na muonekano maridhawa katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma.
Jengo hili limejengwa kwa usanifu wa kisasa wa ghorofa lenye muonekano wa kuvutia ambao kwa pamoja na majengo ya Wizara na taasisi nyingine yanalipamba jiji la Dodoma kwa unadhifu wake.
Majengo haya yamezinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan Oktoba 30, 2026, ambapo aliambatana na Mgeni wake Rais wa Angola, João Manuel Gonçalves Lourenço.