WIZARA YA ARDHI YATEKELEZA OMBI LA WANANCHI WA BAGAMOYO KUONESHWA MIPAKA YA MAENEO YAO

WIZARA YA ARDHI YATEKELEZA OMBI LA WANANCHI WA BAGAMOYO KUONESHWA MIPAKA YA MAENEO YAO

Wizara ya Ardhi

Govt Institution
Joined
May 14, 2024
Posts
306
Reaction score
165
bbee6491-a755-4153-bc0f-1db7ca714eb1.jpeg
76c86543-f363-4d56-87bd-c25acb9b79ff.jpeg
4a913ebc-6f9a-42b7-ab13-d547ce05b3bb.jpeg
b30dadd6-3639-45f2-824e-3db0f50fb0e5.jpeg
ae861630-ce42-4b87-bf1d-d8247bdc261e.jpeg
eb688690-0af5-49d3-9a4e-0130dc922bd6.jpeg


BAGAMOYO, PWANI

Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, leo tarehe 21 Oktoba 2026, imetekeleza ombi la wananchi wa Bagamoyo, mkoani Pwani, la kuoneshwa mipaka ya maeneo yao yaliyopo katika eneo la Uwanja wa Ndege wa Sanzale, wilayani humo.

Akisimamia na kuelekeza utekelezaji wa zoezi hilo, Naibu Kamishna Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bw. Hussein Sadick, amewahakikishia wananchi kuwa zoezi hilo litafanyika kwa weledi, haki na kuzingatia maslahi mapana ya wananchi.

Utekelezaji wa zoezi hilo ni sehemu ya mwendelezo wa kutekeleza maelekezo ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, kufuatia ombi lililowasilishwa na wananchi wa maeneo hayo mbele yake pamoja na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Leonard Akwilapo, wakiiomba Serikali kuwasaidia kupata ufafanuzi wa mipaka ya maeneo yao.

Aidha, wataalamu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi wanaendelea kutoa huduma kupitia Kliniki ya Ardhi wilayani Bagamoyo, mkoani Pwani, iliyoanza tarehe 19 Oktoba 2026 na inayotarajiwa kuhitimishwa tarehe 23 Oktoba 2026.

Kliniki hiyo ni sehemu ya juhudi za Serikali za kusikiliza kero za wananchi, kutoa ufafanuzi wa masuala ya ardhi na kutafuta suluhisho la changamoto zinazohusiana na migogoro ya ardhi.

Hatua hiyo inaonesha dhamira ya Serikali ya kuhakikisha kuwa changamoto za wananchi katika sekta ya ardhi zinashughulikiwa kwa kuzingatia haki, weledi na maslahi ya wananchi, sambamba na kuimarisha usimamizi na utatuzi wa migogoro ya ardhi nchini.
 
Back
Top Bottom