Wizara ya Elimu acheni kuwa madalali wa Scholarship za Ubalozi

Bi Mkubwa pekee ndo anatamani kuona unafika level kubwa maishani mwako! Ila Afrika sijui kwanini tu?!
 
Ni exprience nzuri sana kuwa na watu waliokwenda nje ya nchi kupata maarifa!
 
Mkuu mimi naomba kueleweshwa kidogo. Hawa wafadhili huwa wananufaikaje wanapotoa hizo scholarship? Maana wanatumia pesa ila huwa sijui namna wanavyofaidika hapo baadae.
 
Mkuu mimi naomba kueleweshwa kidogo. Hawa wafadhili huwa wananufaikaje wanapotoa hizo scholarship? Maana wanatumia pesa ila huwa sijui namna wanavyofaidika hapo baadae.
Mara kadhaa ni kutengeneza uhusiano mzuri baina yao na nchi husika, pia huwa ni kama kulainisha mipango ambayo wanatamani kuingia na nchi fulani. Lakini kubwa ni kubadilishana uzoefu Mkuu
 
Watanzania waliopo kwenye nafasi za juu ni watu wanaopenda kubania watanzania wenzao kwa makusudi na wana roho mbaya. Ni watu wabaya sana. Mungu anawaona.
 
Angalizo nzuri.

Ni vyema ubalozi wenyewe kutangaza kuhusu ufadhili wa masomo nje ya nchi kwa umma ili kuepuka madhila na utapeli. Baadhi ya njia za kufanya hivyo zinaweza kujumuisha:

1. Kuandaa tovuti rasmi ya ubalozi inayotolea maelezo kamili kuhusu ufadhili unaotolewa, pamepuatia tarehe za maombi, vigezo vya usahihi, na namna ya kuwasilisha maombi.

2. Kufanya matangazo ya umma kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii ya ubalozi, ili kuhakikisha habari zinasambazwa kwa watu wanaohitaji.

3. Kushirikiana na taasisi za elimu na mashirika mengine ya jamii ili kusambaza taarifa kuhusu fursa hizi za ufadhili.

4. Kutoa miongozo na ushauri kwa watu binafsi wanaoomba ufadhili ili kuepuka madhila na kuongeza uwazi.

Lengo kuu ni kuhakikisha kwamba taarifa za ufadhili zinapatikana kwa uwazi na wazi kwa wale wanaohitaji, ili kuwezesha mchakato wa maombi kuwa wa haki na wa uwazi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…