Wizara ya Elimu: Shule za bweni shule za msingi zifungeni. Ni uzembe wa malezi

Nasisimkwa hapa kwa hoja za wadau huku nikiwafikiria wanangu wadogo leo hii niwaache waende kweli boarding hapana hapana. Na suala la eti lazima darasa la 4 sijui la 7 wakae boarding hyo kwangu haitakuwepo.
 
Tenageza ya Ulaya wakati facilities zetu bado mbovu!!
 

Uko sahihi 100%
Hio ndio sababu kubwa kabisa kuliko zote. Je ni wangapi waweza kung'amua? Probably 1/1,000,000. Ni shida!
 

Uko sahihi 100%
Hio ndio sababu kubwa kabisa kuliko zote. Je ni wangapi waweza kung'amua? Probably 1/1,000,000. Ni shida!

Smart Answer.
Nafikiri tutafutane Inbox tuanzishe Campain ya kuwaokoa watoto wetu
PM please
 
Mimi nasema mtoto aende boarding akiwa advance sikuhizi watoto Wana maliza mapema ni vizuri wazazi tuwalee watoto mpaka wapevuke ndio tuwapeleke boarding.
Tatizo la kulea
Nyie hamliwezi kwasasa,
Kwasababu wengi wenu ni Waajiriwa na Watafutaji,hamtaki kubaki na kulewa Watoto wenu,Mtoto analelewa na Housegirl katika mazingira tatanishi.....
Ndio maana wakaona wao kwa akili zao(zembe)Bora wawapeleke Mashule ya Bweni
 
Yaani inafika mahali wazazi tunahisi VIGOGO wizara ya elimu MNAHONGWA na wamiliki wa shule wa shule binafsi, yaani wamejitawala mno !! hakuna uthibiti kabisa, mtoto akifika darasa la NNE lazima ahamie boarding wakati utafitu umefanyika uingereza nakuonyesha hili suala linawaharibu sana watoto kisaikolojia na kijamii. pia hata uingereza imeonekana shule hazina miundombinu muafaka ya kulinda watoto wa umri huo
 
yaani watoto wetu wanatumika kama chombo cha matangazo, WIZARA YA ELIMU MNATIA AIBU KWENYE HILI
 
Sometimes nashawishika kuwa kuna jambo nyuma ya pazia.
Ni siku ya 4 naangalia comment hii na kuwaza kwa undani sana. Kuna wakati tuliambiwa FEZA schools pia zilikuwa na jambo nyuma ya pazia. Hawa wanaoanzisha shule za boarding, yawezakuwa ni biashara tu lakini, kweli yabidi tukubali na mengine ya ziada. Baadhi wanatoa ofa ya ada kwa watoto fulani kama kivutio.

Kwa wataalamu wa elimu, elimu ya msingi muhimu ni hizo KKK basi! Ndo maana huwa sioni shule nzuri au mbaya ya msingi. Akijua kusoma, kuandika, na hesabu basi! Kwa nini mzazi avutiwe kupeleka mtoto boarding? Kuna nini?
 
Hapa mimi next year nitakuwa mhanga kwenye hili. Kijana wangu anaingia darasa la saba na siku zote nilikuwa naye home. Ila kulifanyika kikao cha shule kwa wazazi wa wanafunzi wanaotajia kuingia darasa la saba. Wazazi na walimu na uongozi wa shule wakafikia maamuzi kwamba watoto wate watakaa bweni mwakani.

Sina ujanja. Itabidi nikubali tu kijana amalize shule ya msingi.
 
Uko sahihi 100%
Hio ndio sababu kubwa kabisa kuliko zote. Je ni wangapi waweza kung'amua? Probably 1/1,000,000. Ni shida!
Ni watu wachache sana sadly.Kwa kulitambua hili,nimeanza kazi ya kutafsri hili bandiko kwa kiswahili,labda itasaidia ku-raise awareness.Kiukweli hali ni mbaya sana.
 
Saikolojia ya elimu inaniambia kuwa mtoto mdogo hafaulishwi kwa kusoma mda mwingi
 
Ni kweli! Muache amalize shule. Shule zinaendeshwa kwa njama kubwa. Vikao vya aina hiyo, huwa kuna watu walionunuliwa, kazi yao ikiwa ni kuhakikisha waendeshaji wa shule wanapitisha mambo yao. Wanajua wakikaa bweni, ada itapanda wapate faida. Elimu imekuwa biashara. Hii ni hali inayotia mashaka sana juu ya shule za private.
 
Huwa najiuliza kama unaona kulea huwezi bora usizae. Unampeleka mtoto 4years boarding eti sababu uko busy??? Umoja na mshikamano wa taifa lolote unaanzia kwenye ngazi ya familia ila sasa tunapoteza thamani ya familia, wazazi hatuwapi watoto wetu malezi badala yake tunatumia pesa kubomoa familia na kunaandaa taifa la watu wasiokua na upendo wala mshikamano.
Hata mtoto apate As kila level kama hana values za jamii yake, hajielewi hata thamani yake wala thamani ya jamii yake ni bureeeee
 
Upo sahihi Mkuu ipo shule jirani hapa eti mtoto akifika darasa la sita na la Saba wanalazimisha wazazi uwapeleke watoto huko boarding wakati tulipokua tumewapeleka darasa la kwanza hilo walisema kwa wale wanaotoka mbali nikasema hili hapana naomba uamisho sijawahi kufikiri kumuacha mtoto wa shule ya msingi alale shuleni...nikamuamisha nipo nae nyumbani na shule anakwenda hizo shule zina watoto wadogo hadi unatingisha kichwa aisee...
 
Shule hizo ni mpango mkakati wa kuharibu watoto mkuu.Waalimu na watoto wenyewe wanatumika kama agents.Kwa bahati mbaya wazazi wengi ni mambumbu sana katika jambo hili.
 
Hivi masomo gani Hayo jamani ya kuanzia SAA 11 asubuhi. Mwenyewe Nilikuwa za serikali tena Nakumbuka LA NNE mwaka 98 nilipata kama mia NNE masomo Fulani ivi sema nimeyasahau jamani.
Labda kwa level ya secondary masomo kuanzia muda huo ni sawa ila primary jamani hakuna kitu. Kwanza wanasoma nini mbona content yenyewe ni ndogo sana.
 
Sasa si ubora mzazi unakaa na mwanao na kumshape kuliko huko boarding maana ukiwa kazini una meet mtoto jioni akitoka shule kuliko huko boarding, mwenyewe nilisoma boarding naichukia silipendi na hapo nilikuwa nimeshakuwa mkubwa Ila nilikuwa napata tabu, sembuse mtoto wa primary naona Hadi huruma
 
Saikolojia ya elimu inaniambia kuwa mtoto mdogo hafaulishwi kwa kusoma mda mwingi
Wanawapa tu watoto mzigo msingi mtoto ana Soma boarding ili iweje wakati kuna mashule mengi tu unaenda
 

Natamani wazazi wangekuwa na ufahamu huu na huruma kwa watoto wao kiasi hiki.

Mlio tayari tupeane mawasiliano tuunganishe nguvu twende wizara ya Elimu kulisemea.
Mnasemaje wadau wenye kujali watoto wetu? Usiangalie uchache wetu. Umoja ni nguvu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…