Wizara ya Fedha, BoT na TAKUKURU imulikeni Letshego /Faidika Tanzania ni majambazi

Wizara ya Fedha, BoT na TAKUKURU imulikeni Letshego /Faidika Tanzania ni majambazi

Hii ni taasisi ya Fedha inayojihusisha na mikopo kwa wafanyakazi na wafanyabiashara
Juni 2021 mfanyakazi (sitamtaja) alikopa ths 3,500,000 kwa makato ya Tsh 126,400 kwa mwezi,

Sasa picha limeanza mwaka huu mfanyakaz akataka kuwalipa deni lao (kumbuka ameshakatwa kama miezi 20)
Toka Juni 2021,

Kwanza wakasema balance Yao mpaka uende kwenye branchi zao za mikoa na kwa kesi yake yeye ikabidi aende Morogoro mjini, Akajaza fomu kuomba kupewa deni lake Ili alipe (afute mkopo) wakamwambia balance haitoki kirahisi hivyo ni mpaka miezi mitatu! Akasema sawa akarudi zake kijijin

Tarehe 6 (alhamis) Kabla ya Pasaka wakamwambia balance yake imetoka akachukue
Kutoka siku Ile Hadi kufika Moro goro mjini ni ngumu,
Kesho yake ilikua ijumaa kuu,
Na jumatatu ikawa ni jumatatu ya Pasaka!
Akaenda jumanne akaletewa deni la 3,930,000 ( na kumbuka alishakatwa zaidi ya miezi 20 !! Makato ya 126400 ambapo ukizidisha toka Juni 2021 Hadi march (126400*21= 2,654,400) ambayo tayari ilishalipwa..

Lakini jamaa akasema potelea pote akaamua kuwalipa iyo 3.93 m!
Baada ya kusoma iyo statement wameandika pesa mwisho kulipa ni tr 14!
Kumbuka hapo wameweka siku 7 Bila kuhesabu wikiend au zile siku za pasaka!
Jamaa kajipinda kaja kulipa tar 17 (siku 3) mbele
Anapeleka risiti Letshego wanasema amechelewa kulipa na hivyo aongeze 56,000 kama faini!!

Jamaa uvumilivu ukamshinda akasema haongezi pesa!
Na wao wakasema wataendelea kumkata! Iyo 126,400 Kila mwezi kama kawaida!

Jamani huyu jamaa afanyeje hapo katika mazingira haya!

Asanteni
BoT na TAKUKURU imulikeni Letshego /Faidika Mkimaliza kwao ninaombeni muhamie KAMPUNI YA HERITAGE FINANCE Yenye makao yake makuu Arusha Tanzania
 
Kumbe sheria ziko tight, nilidhani ingekuwa rahisi ili nipige hela kwa Wakulima
Acha kabisa utaishia pabaya mno. Kilichopo saaa hivi wanakusanya taarifa kimya kimya, kwahiyo wale wanaokeuka sheria hawajui ila info zao zote ziko BOT. Na ndiyo maana utashangaa microfinance nyingi zitakuja kufungiwa. Tatizo kubwa wengi wanaoanzisha hawataki kutumia watalaamu etc. Compliance kwa issue za bank huwa tight mno.
 
Okay, wacha tuvute subira
 
Utapiga sana hela ila jitahidi kuwa na upande either kwa Mungu au Kwa wa dunia maana ni biashara yenye hela ila vita nje nje
Umenipa moyo, wacha nijipange niingie kwa kuanza kuwakopesha mwezi wa 12 najua kufikia mwezi April na Juni mwakani nitaanza kupata rejesho langu
 
Umenipa moyo, wacha nijipange niingie kwa kuanza kuwakopesha mwezi wa 12 najua kufikia mwezi April na Juni mwakani nitaanza kupata rejesho langu
Ni kweli naona huku vijijini wanakopeshana japo no documents of what kikubwa kujuana vyema na unaowakopesha na kuwekeana masharti himilivu .

Kila la kheri ndugu .
 
Ni kweli naona huku vijijini wanakopeshana japo no documents of what kikubwa kujuana vyema na unaowakopesha na kuwekeana masharti himilivu .

Kila la kheri ndugu .
Shukrani Mkuu 🙏

Vijijini ukiweka Mzigo wa milioni 5 unaweza kupata faida si chini ya millioni 7.5 kwa miezi hiyo 6 ya kusubiria wavune
 
Ninavyojua mimi Letshego ni benki. Kwa upande wangu nina maoni tofauti kidogo. Kabla sijawalaumu Letshego lazima mkopaji asome tena mkataba wake ulikuwa unasemaje. Pia unapolipa mkopo unakatwa kupitia account yako na bank statement huonyesha kabisa jinsi ulivyokatwa. Alishindwa nini kuchukua statement na kupiga hesabu? Hata kama kulikuwa na penalties statement ingeonyesha.

Hii kauli "Lakini jamaa akasema potelea pote akaamua kuwalipa iyo 3.93 m!" ni ya kijinga sana na kushindwa kujua haki zake. Huwa najiuliza kwanini haya mambo huwakumba sana watu wa vipato vya chini? Yaani hapo kwa mtu makini ni fursa ya kesi na kujipigia mahela ya fidia. Tafuta wakili uwaburute hao watu mahakamani utapiga hela. Pia nawasihi sana watanzania wenzangu tuwe na tabia ya kusoma mikataba kabla ya kusaini hata kama njaa imekaba kiasi gani. Kama unaona huwezi kusoma mkataba tafuta kijana smart ndani ya circle yako akueleweshe.

Kingine ni kujua haki zako. Hata ikiletwa katiba kutoka mbinguni haitasaidia kama bado watu ni wajinga kiasi cha kudhulimiwa waziwazi. Hii ndo sababu hata mbunge anaweza simama na kusema tulipishwe Tsh 100 kwenye mafuta au mwingine akasema wabunge wajengewe maeneo yao maalum ya starehe.
 
Bank ikawe Letshego hicho nikakundi cha wahuni
 
Bank ikawe Letshego hicho nikakundi cha wahuni
Basi hatari. Nilikuwa nimekariri pale Manzese kulikuwaga na benki flani halafu walivyoondoka jengo hilohilo wakachukua Letshego nikajua ile benki labda imebadili tu jina.
 
Kuna dogo namjua alianza na branch moja la microfinance akawa anakopesha wastaafu na wakulima huu mwaka wa kumi ana matawi zaidi ya 20 nchi nzima na ana ukwasi balaa.

Hajavuka 40 lkn kwenda Dubai na Ibiza kula bata ni dakika sifuri kama kwenda RiverSide kwa wahaya. Aisee kwenye hii business kuna mambo mengi tusiyoyajua ikiwemo utapeli.
 
Ni hatari usijaribu mkuu wangu. Jinsi sheria zilivyo ni kwamba wanakuacha unafanya ujinga siku wakija wanakulambusha Money laundering. Very soon microfinance nyingi wamiliki wake watafungwa. Stay tuned mkuu, sheria zake ni kali mno! Ila watu wengi hawajui ingawa walifundishwa
Chawa wa mama hii habari umetoa wapi?
Watu kama Platinum Wana miaka na miaka wanafanya huu ujinga ulishawahi ona wanachukuliwa hatua?
 
Ni hatari usijaribu mkuu wangu. Jinsi sheria zilivyo ni kwamba wanakuacha unafanya ujinga siku wakija wanakulambusha Money laundering. Very soon microfinance nyingi wamiliki wake watafungwa. Stay tuned mkuu, sheria zake ni kali mno! Ila watu wengi hawajui ingawa walifundishwa
BOT wamelala usingizi wa pona.
 
Letshego na Faidika ni kampuni moja?
Waanze na platinum jamani.
Hao platnum walikuja kazini kwetu mwezi January. Walikua watatu jamaa mmoja mtanashati na pisi kali mbili.

Basi baada ya morning report wakaanza kutoa elimu ya mikopo pale na kusema wana riba nafuu na unaweza kuchukua mkopo kwa ajili ya kununulia mkopo mwngne (yani kama unadaiwa na loanboard wao wanaweza cover).

Wakasambaza business card zao pale baada ya kikao nikaanza kuona staffs wengine wakienda kujiandikisha. Dah! Jamaa wanajua kushawishi aisee.
 
Back
Top Bottom