Wizara ya Fedha, BoT na TAKUKURU imulikeni Letshego /Faidika Tanzania ni majambazi

hiyo ni shida yetu wabongo, kila kitu kinajulikana kabla ya kukopa, wakati unahitaji hela akili unaweka mfukoni, hutaki kujua masharti kabisa, una saini tu
baadaye ndo unatoa akili mfukoni
kama anahisi kuna uonevu aende bot wachunguze
Sure.
Nenda benki kuu mzee hutojutia. Watatema hela yako fasta kabisa
 
Wakuu naombeni hatua za kufuata Ili huyu jamaa awasilishe malalamiko yake BOT
 
Bora tu
 
mimi nilikopa 2,500,000 tu kwenyetaasisi furani ila nililipa 4,450,000 baada ya miezi 5 tu mzee nilipigiwa mahesabu nikaona isiwe kasi nikalipa mpaka sasa nimekoma ...kikubwa nimejifunza tukope kwenye mabenki tu huu ni uzembe wetu wenyewe kushindwa kupiga mahesabu vzr tukipata matatizo ya haraka
 
Hakika,
Hawa faidika ni ny*ko kwakweli
 
Kama ni mtu makini unayejuwa thamani ya pesa na unatafuta pesa kwa shida huwezi kopa hizi FINANCE njaa. Hawa si watoa huduma bali ni kukupeleka katika umasikini wa kudumu.

Ukikopa mkopo wenye makato ya miaka 7 au 8.

Riba yao ni mara 3 ya pesa uliyokopa.

Mfano ukikopa milioni 3 kwa miaka 8 jiandae kulipa 12M


Unajiuliza hapo umekopa utatue tatizo au umejichimbia shimo.


UPUMBAVU WA WATUMISHI MBALIMBAI.

Hizi finance zina tabia ya kukushawishi na kujigamba kuwa unapata MPUNGA ndani ya masaa 24, tena nyingine zinatembea na pesa Live ukijaza tu form unapewa Mzigo.

Hili watu wengi wanaona ni rahisi coz hakuna usumbufu bila kuwaza RIBA YAKE MBELE.

NMB,CRDB NA BANK NYINGINE.

Mikopo yao inachukua muda ni kweli unapambana mwenyewe inaweza chukua hata mwezi au au wiki 2 au 1.

Lakini hawa ni uhakika siyo wababaishaji kama hizi finance janja janja.

Mtu anaona kufatilia 2 weeks ni nyingi anaona bora ajilipue huko kwa wakausha damu.


Zaidi CRDB naona wako vzr sana coz CRDB Unaweza kukopa 10M hlf makato hayo hayo NMB ukaambiwa mwisho 7M
 
Chawa wa mama hii habari umetoa wapi?
Watu kama Platinum Wana miaka na miaka wanafanya huu ujinga ulishawahi ona wanachukuliwa hatua?
Huyo chawa hamna kitu anajua yeye kusifia serikali tu
 
Asanteni kwa ushauri wenu jamaa ametuma malalamiko yake BoT kupitia complaining desk na bot wanashughulikia
 
Mikopo hii huchukuliwa na watu wenye akili timamu kabisa ambao kweli huwa hawapitii kanuni za mkopo vizuri, ama kwa uharaka au kutojua. Lakini benki zote zilipaswa zitoe maelezo ya kutosha kwa wakopaji ili kuepuka migogoro. Lakini kwa huku kutojua kwetu benki zinatumia kuzidi kutukandamiza.
 
Muombe mkataba wake kwanza wa mkopo then watu ndo tutakuwa na uwanja mpaka wa kumshauri.

Watanzania wengi huwa tunapokwendaga kwenye hizi microfinance kuomba mikopo huwa tumebanwa kweli kweli na wenyewe huwa wajanja kwa baadhi kwa kutusainisha mikataba kwa lugha ya kiingereza.

Kwaiyo ukishatajiwa mashart mawili matatu kiwepesi fasta anaanguka sahihi na kuchukua hela kilio kinakuwa baadae kama hivi
 
Sijaelewa hapo alipokuwa amelipa Deni kwa miezi 20.... Then akaja kulipa pesa 3.93mil kwa kusema potelea mbali.... Mwenzetu anaokota wapi hizo pesa na wengine wakaokote pia??
 
Acha uongo wewe chawa. Hizo taarifa zinakusanywa miaka mingap? Na watu wanaendelea kuumizwa na ushahidi upo wazi kabisa
Kumbuka wanaokusanya taarifa ni wengine na wanao chukua hatua ni wengine kabisa.

Unaweza kusema hapo mtaani kwako watu hawakujui kiundani lakini kiuhalisia watu wanataarifa zako zote,siku zikihitajika wewe mwenyewe unaweza kushangaa imekuwaje

All in all vyombo vyetu vingi viko macho mno na vinafanya kazi kweli kweli sema wamenyimwa tu power ya kutake action,ila yote tunayolalaimika humu kila siku serikali inayajua na yako mezani sema wenye mandatory ya kuchukua hatua ndo hao wamekula buyu
 
Sijaelewa hapo alipokuwa amelipa Deni kwa miezi 20.... Then akaja kulipa pesa 3.93mil kwa kusema potelea mbali.... Mwenzetu anaokota wapi hizo pesa na wengine wakaokote pia??
Alilipa marejesho 20
Yaani miezi 20,

Na baadae akaambiwa kufuta mkopo ndio alipe 3.926 m cash
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…