Wizara ya Madini imesema inafuatilia jiwe la bilioni 240 linalopigwa mnada Dubai, yasema ilipata taarifa mtandaoni

Sasa watu kulamba asali nalo ni jambo la kukasirika jamani
 
Ndio matokeo ya uongozi mzima wa kitaifa kule Divai?
Tulishaonya hapa kwamba chekeni na waarabu, mtaona. Kuwekwa picha ya Mh wetu No1 pale Dubai tukasema tutayaona mbeleni.
Leo hata miezi miwili- mitatu haijapita, tunasikia madini ya thamani yanauzwa kule bila mwenye shamba kujua. Integrity yetu kitaifa iko wapi? Majibu ya wizara ya madini ni dhaifu sana.
 
Taarifa zimetoka kwenye mitandao ya kijamii? Inasikitisha sana.
 
Chief anaupiga nwingi sana... Sasa tunaelewa maana yake
 
... tulipata taarifa "kupitia mitandao ya kijamii". Mbona yule mwehu alitamani ifungiwe?
Mwehu aliyeweza kuzuia madili kama haya...yaani jiwe kubwa hivyo ila mamlaka hazina taarifa!!! Labda kama wauzaji hawana taarifa sahihi.

Ila inawezekana maana wachimbaji wengi w Longido na Loliondo wabakimbilia kuuza Kenya.
 
Una uhakika hilo jiwe limetoka Tanzania?
Mwehu aliyeweza kuzuia madili kama haya...yaani jiwe kubwa hivyo ila mamlaka hazina taarifa!!! Labda kama wauzaji hawana taarifa sahihi.

Ila inawezekana maana wachimbaji wengi w Longido na Loliondo wabakimbilia kuuza Kenya.
 
Wamekubali limetoka Tanzania?
Wewe una uhakika ni jiwe kutoka Tanzania?
 
Huwa mnapapatikia sana wazungu
Yaani anakuja na private jet kwenye mbuga akiwa kabeba makamera eti kaja kupiga picha kumbe mwizi

Mswahili anabeba mabegi hajui kuna nini ndani eti Potter
 
Tani mbili?acha kuchekesha baraza...Tani mbili ni zaidi ya bajeti ya nchi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hangaya kiguu na njia huku nyuma ndo haya.ama ndo alilifikisha dubai
 
Ngoja nifanye chapu nirudi zangu Dubai labda naeza bahatisha vidola kadhaa kutoka kwenye hili jiwe.
 
Nilikua ninawacheka Congo kuwa pamoja na utajiri wa madini walionao bado wana low literacy level, high mortality rate. Kumbe tunasafiri nao katika boat moja.
 
Vipi kuhusu lile tukio la kuingia Butimba na kuwaachia wale walioshikwa wakitorosha dhahabu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…