Wizara ya Madini imesema inafuatilia jiwe la bilioni 240 linalopigwa mnada Dubai, yasema ilipata taarifa mtandaoni

Wizara ya Madini imesema inafuatilia jiwe la bilioni 240 linalopigwa mnada Dubai, yasema ilipata taarifa mtandaoni

Sasa watu kulamba asali nalo ni jambo la kukasirika jamani
 
Leo wa mbunge Mkinga, Dastan Kitandula ameuliza kuhusu jiwe la Tanzania linalipigwa Dubai Uarabuni. Naibu waziri wa madini amesema nao waliona mtandaoni na wanafatilia.

=====

Dansatan Kitandula: Mheshimiwa spika, jiwe la ruby lenye uzito wa kilo 2.8 lipo kwenye maonesho kwasasa Dubai na jiwe hili linasadikika linatoka Tanzania na kwamba siku chache zijazo kutakuwa na mnada wa kuuza jiwe hili. Je kama nchi tunanufaika vipi na mnada huo?

Naibu waziri wa Madini: Ni kweli mnamo tarehe 13 April mwaka huu wizara ya madini ilipata taarifa kupitia mitandao ya kijamii kwamba kuna jiwe la madini ya ruby lenye uzito wa kilo 2.8 na ambalo linadaiwa kuwa na thamani ya dola milioni 120 sawa na zaidi ya bilioni 240 ambalo limepewa jina la bald al hamal na ambalo linakwenda kuwekwa mnadani ndani ya siku 30 baada ya mfungo na jiwe hilo kudaiwa limetoka Tanzania.

Mara baada ya kupata habari hizi, wizara ya Maliasili imechukua hatua za haraka kutafuta kama habari ni za kweli na kama jiwe hili limetoka Tanzania na kwasababu jiwe hili limeshavuka mipaka lipo kwenye nchi nyingine.

Taarifa hizi sasa ambazo tunazikusanya zinahusisha nchi za Dubai na tayari tunafanya mawasiliano na ubalozi wetu kufuatilia ukweli, pia tumebaini mmiliki wa sasa wa jiwe hilo yuko nchini Marekani na mawasiliano naye tumeshafanya tangu jana.

Tutapopata nyaraka za usafirishaji kama kweli limetoka Tanzania, thamani na asili, nyaraka za mauzo tutaleta taarifa bungeni na kama ni la kwetu niwahakikishie watanzania haki yao haitapotea.

Pia, soma=> Ruby yenye thamani ya bil 276 ilisafirishwa kimagendo huko Dubai? Serikali haina taarifa ilifikaje

=> Mali yetu inauzwa mnada wa Dubai Madini ya Ruby

View attachment 2195200
Ndio matokeo ya uongozi mzima wa kitaifa kule Divai?
Tulishaonya hapa kwamba chekeni na waarabu, mtaona. Kuwekwa picha ya Mh wetu No1 pale Dubai tukasema tutayaona mbeleni.
Leo hata miezi miwili- mitatu haijapita, tunasikia madini ya thamani yanauzwa kule bila mwenye shamba kujua. Integrity yetu kitaifa iko wapi? Majibu ya wizara ya madini ni dhaifu sana.
 
Taarifa zimetoka kwenye mitandao ya kijamii? Inasikitisha sana.
 
Huu upumbavu tu kujifanya eti hawajui lilifikaje huko.. wanaona watu wote ni misukule?? Hivi Chief Hangaya atangazwe burj Al Khalifa siku mbili nzima bure kweli??? Wanampenda sana au??? Unaweza kuta ule msafara wa EXPO DUBAI ndio uliondoka na huo mzigo...Za kuambiwa changanya na za kwako.
Chief anaupiga nwingi sana... Sasa tunaelewa maana yake
 
... tulipata taarifa "kupitia mitandao ya kijamii". Mbona yule mwehu alitamani ifungiwe?
Mwehu aliyeweza kuzuia madili kama haya...yaani jiwe kubwa hivyo ila mamlaka hazina taarifa!!! Labda kama wauzaji hawana taarifa sahihi.

Ila inawezekana maana wachimbaji wengi w Longido na Loliondo wabakimbilia kuuza Kenya.
 
Una uhakika hilo jiwe limetoka Tanzania?
Mwehu aliyeweza kuzuia madili kama haya...yaani jiwe kubwa hivyo ila mamlaka hazina taarifa!!! Labda kama wauzaji hawana taarifa sahihi.

Ila inawezekana maana wachimbaji wengi w Longido na Loliondo wabakimbilia kuuza Kenya.
 
Wamekubali limetoka Tanzania?
Wewe una uhakika ni jiwe kutoka Tanzania?
Huu upumbavu tu kujifanya eti hawajui lilifikaje huko.. wanaona watu wote ni misukule?? Hivi Chief Hangaya atangazwe burj Al Khalifa siku mbili nzima bure kweli??? Wanampenda sana au??? Unaweza kuta ule msafara wa EXPO DUBAI ndio uliondoka na huo mzigo...Za kuambiwa changanya na za kwako.
 
Huwa mnapapatikia sana wazungu
Yaani anakuja na private jet kwenye mbuga akiwa kabeba makamera eti kaja kupiga picha kumbe mwizi

Mswahili anabeba mabegi hajui kuna nini ndani eti Potter
 
Ruby kilo 2 kitu gani, serikali ifatilie lipo jiwe lina tani 2 Mahenge lipo chini ya ardhi kilometers 3 taarifa zake zipo Mahenge wafatilie lina geological report,plus picha ya scanner iliyopigwa chini huko eneo la tukio, kuna kampuni ya USA ilitaka kulitoa Magufuli akawa ameingia wakashindwa.
Sasa ni Shamba la bibi watalitoa. Kama kilo 2 bilioni 246 vipi tani 2 ni tilioni ngapi. Mimi sioni mantiki ya serikali kukamua kodi watza masikini hali madini yamejaa KILA wilaya yanaibwa na wageni huku yakipita mipakani, maana mswahili aachi pesa.
Tani mbili?acha kuchekesha baraza...Tani mbili ni zaidi ya bajeti ya nchi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hangaya kiguu na njia huku nyuma ndo haya.ama ndo alilifikisha dubai
 
Ngoja nifanye chapu nirudi zangu Dubai labda naeza bahatisha vidola kadhaa kutoka kwenye hili jiwe.
 
Ruby kilo 2 kitu gani, serikali ifatilie lipo jiwe lina tani 2 Mahenge lipo chini ya ardhi kilometers 3 taarifa zake zipo Mahenge wafatilie lina geological report,plus picha ya scanner iliyopigwa chini huko eneo la tukio, kuna kampuni ya USA ilitaka kulitoa Magufuli akawa ameingia wakashindwa.
Sasa ni Shamba la bibi watalitoa. Kama kilo 2 bilioni 246 vipi tani 2 ni tilioni ngapi. Mimi sioni mantiki ya serikali kukamua kodi watza masikini hali madini yamejaa KILA wilaya yanaibwa na wageni huku yakipita mipakani, maana mswahili aachi pesa.
Nilikua ninawacheka Congo kuwa pamoja na utajiri wa madini walionao bado wana low literacy level, high mortality rate. Kumbe tunasafiri nao katika boat moja.
 
Mwambie bibi yako afatilie rasilimali za taifa, muache kujificha kwenye mgongo wa Magufuli, Magufuli aliisha wahi kamata almasi zilizokuwa zikitoroshwa taifa zima tulishudia, kama liliibwa wakati wa Magufuli kwanini mnada utokee sasahivi baada ya mwaka kufa Magufuli?
Vipi kuhusu lile tukio la kuingia Butimba na kuwaachia wale walioshikwa wakitorosha dhahabu?
 
Back
Top Bottom