Wizara ya maji na benki ya maendeleo ujerumani (KfW) kuendeleza ushirikiano katika kutekeleza miradi ya maji

Wizara ya maji na benki ya maendeleo ujerumani (KfW) kuendeleza ushirikiano katika kutekeleza miradi ya maji

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Hamidu Aweso akiwa jijini Frankfurt nchini Ujerumani leo tarehe 09 Oktoba 2024 amepata wasaa wa kufika makao makuu ya Benki ya Maendeleo ya Ujerumani (KfW) na kukutana na Viongozi wa Benki hiyo kwa lengo la kuboresha na kukuza mashirikiano baina ya Serikali ya Shirikisho la Ujerumani na Tanzania katika uwekezaji kwenye Sekta ya Maji.

Katika maelezo yake Waziri Aweso , ameshukuru kwa mashirikiano yaliyopo katika kutekeleza miradi ya maji ambapo ameahidi kudumisha ushirikiano huo ambapo KFW nao wameahidi kuzidi kushirikiana na Tanzania na kuwezesha upatikanaji wa fedha.

Waziri Aweso ametoa wasilisho na shukrani Kwa miradi inayoendelea kama vile Mradi mkubwa wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi Mkoani Simiyu unaogharimu kiasi cha Shilingi Bilion 400 utakaowezesha upatikanaji wa maji wilaya za Bariadi, Busega, Itilima, Meatu na Maswa ambapo KfW wamepongeza hatua na kazi inayoendelea katika utekelezaji wake.

Miradi mingine inayoendelea iliyojadiliwa ni pamoja na Mradi wa Maji safi na usafi wa Mazingira Babati na uboreshaji wa usafi wa Mazingira katika miji ya Lindi, Kigoma na Sumbawanga na mpango wa ujenzi wa mradi Tunduma-Vwawa Mlowo.

Kupitia ushirikiano huo, Wizara inategemea kupata Euro Million 15 kwa ajili ya miradi ya maji mkoani Lindi na Mtwara miongoni mwa faida nyingine.

Aidha, KfW wamempongeza Waziri wa Aweso kwa kufanikisha Hati Fungani za Mamlaka ya Maji Tanga (Tanga Green Bond) na wameahidi kushiriki katika ufanikishaji wa Hati Fungani kwa Mamlaka za Maji nchini.

IMG-20241010-WA0023.jpg
IMG-20241010-WA0025.jpg
IMG-20241010-WA0024.jpg
 
Back
Top Bottom