Wizara ya Nishati apewe Waziri anayeaminika na watu wengi ili hata akisema lipo tatizo aaminike

Suzy Elias

JF-Expert Member
Joined
Nov 9, 2021
Posts
1,067
Reaction score
6,200
January si Waziri asiyeaminiwa na wengi hata michango ya watu iwe mitaani ama humu mitandaoni ukweli huo unajidhihirisha.

Sasa ili kuwe na kuaminika tena kwa matatizo yahusuyo Nishati nikuombe Rais Samia teua Waziri mwenye japo chembe ya kuaminika na wengi wetu awe Waziri wa Wizara hiyo.

Bado wapo watu katika baraza lako wenye ushawishi kwa wananchi mfano mzee Lukuvi ni mmoja ya Waziri mwenye kauli inayopokelewa na wengi na ni mtu anayeaminika na watu japokuwa naye ni mwanadamu na mapungufu yake.

Kumpa January nishati ni kumchonganisha na watu tu hali itakayomfanya awe na stress zaidi.

Nashauri,January atafutiwe Wizara nyepesi kwa sababu hata yeye ni mwepesi.
 
Apewe huyu..

JUST IN - The managing director of Tanzania's national oil company TPDC, Dr James Mataragio, has dismissed media eports of looming fuel shortages in Tanzania, saying there is no cause for panic

Mataragio insisted that Tanzania has sufficient fuel stocks https://t.co/mUrKzuvOCq
 
Sukuma gang m namuogopa sana January mwacheni afanye kazi
 
Sukuma gang again.........Wanachotaka kuona ikiwezekana Mawaziri wote watoke kanda ile pendwa enzi hizo.
 
Tusifike mahali tukamchagulia Rais mawaziri tangu lini hicho kikawa kigezo cha Uwaziri tuache Rais aongoze tusitake kumwingilia hadi jikoni. Kuna system ya kupima uwezo wa mtu sio wewe mtoa mada, you are wrong. Hata akitafutwa mwingine unaweza pia usimpate unaemtaka wewe. Liache lipite hilo. Yetu tuangalie performance yao. Tusiangalie mtu tuangalie performance tukifika sasa kutazama nani kakaa lazima atoke kwetu ndio mwanzo wa kupotea.
 
Hebu tuambieni january kafanya kitu kipi kibaya but please mtu akisema aweke ushahidi tuache porojo

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
Apewe Kibajaji
 
January si Waziri asiyeaminiwa na wengi

Kiswahili kigumu sana, ebu toa tafsiri sahihi ya hichi ulichoandika hapa, halafu linganisha na maelezo yako!!

Kwa tafsiri ya kawaida, hapa maana yake anaamiwa na wengi, sasa kwa nini abadilishwe!??
 
Mkuu kila mwamba ngoma ...,Kuna watu wengi tu walio na upeo na utashi sio lazima awe Waziri Lukuvi.
Raisi amemteua na kumwamini January Makamba kwenye wizara ya nishati na ni kipindi kifupi karibu atamaliza mchakato wa ujenzi wa LNG,
Sasa sio wakati wa kutibua pale alipoishafika.Tuwe na subira,bado anawajibika kwenye baraza la mawaziri.


.
 
CCM hakuna anayeaminika.
 
Leo nilikuwa nafanya printing ya documents zangu hapa Dodoma, v8jana waliokuwepo hapa naona wanamrushia lawama marehemu kwa kuanzisha mradi mkubwa wa bwawa la umeme badala ya kuendeleza mradi wa gas usioathiriwa na uhaba wa mvua.

Was interesting to listen them. Sijui wana kiwango gani cha elimu, lakini arguments zao zilikuwa za kisomi hasa ingawa ukiwatazama huwadhanii.
 
Naona mmeamua kukamia mpaka jamaa achomoke sijui ni wivu🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…