Wizara ya Nishati apewe Waziri anayeaminika na watu wengi ili hata akisema lipo tatizo aaminike

Wizara ya Nishati apewe Waziri anayeaminika na watu wengi ili hata akisema lipo tatizo aaminike

Tusifike mahali tukamchagulia Rais mawaziri tangu lini hicho kikawa kigezo cha Uwaziri tuache Rais aongoze tusitake kumwingilia hadi jikoni. Kuna system ya kupima uwezo wa mtu sio wewe mtoa mada, you are wrong. Hata akitafutwa mwingine unaweza pia usimpate unaemtaka wewe. Liache lipite hilo. Yetu tuangalie performance yao. Tusiangalie mtu tuangalie performance tukifika sasa kutazama nani kakaa lazima atoke kwetu ndio mwanzo wa kupotea.
Ndio maana katika nchi zenye Demokrasia kamilifu mteuliwa wa Rais anabidi apitishwe na bungee(pamoja na bunge la kutunga hovyo) pia kujieleza aliyofanya hjko nyuma.
Hi teua apisha ni utopolo!
 
Naona mmeamua kukamia mpaka jamaa achomoke sijui ni wivu🤣
Wala sio wivu. Kumbuka jamaa anatolewa wizara nyingi Sana. Afu alimuongea mkuu wa nchi. Ivyo anaweza akamuongea bado huyu huyu Boss wako sio mtiifu pia. Nadhani anakamia Sana madaraka ni Kama anatumia nguvu kubwa Sana kuyatafuta kwa kujipendekeza msoga
 
Waziri anaetokea kwenye kizazi hiki cha wanasiasa especially ccm anaaminikaje?
 
Wala sio wivu. Kumbuka jamaa anatolewa wizara nyingi Sana. Afu alimuongea mkuu wa nchi. Ivyo anaweza akamuongea bado huyu huyu Boss wako sio mtiifu pia. Nadhani anakamia Sana madaraka ni Kama anatumia nguvu kubwa Sana kuyatafuta kwa kujipendekeza msoga
Mkuu wa nchi yupi mwendazake acheni hizo. Historia hiyo, kama anaweza kazi afukuzwe kwa kumuongea mwendazake? Inaonekana watu wameumia sana, hapo ndipo tunapojivisha upofu. Tunaacha kuangalia performance tunazungumza yaliyopitwa na wakati.
 
Mheshimiwa Rais akicheza hizi ngoma itakuwa ndio mwanzo wa kupoteza direction, Sio lazima atawale kabila lako. Nchi hii ina watu na makabila mengi ikifika mahali watu wakaamini kanda moja tu ndiyo inayotakiwa kutoa viongozi itakuwa shida sana nchi itaparanganyika siku sii nyingi. Tuache ukabila tujenge taifa lenye umoja.
 
ukweli usiofichika January haaminiki na watz ,na hii inawafanya watu wasimuamini hata Kama Kuna mahali amefanya kaz kwa uaminifu,watu hawana Imani nae!! kwa hali hii itamfanya wizara iwe nzito kwake ,lakini pia hata watendaji wake watafanya Kaz ktk mazingira yasio ya kuaminiwa na wananchi.Hii wizara inahitaji mtu anayeaminika na watu.
 
Kiswahili kigumu sana, ebu toa tafsiri sahihi ya hichi ulichoandika hapa, halafu linganisha na maelezo yako!!

Kwa tafsiri ya kawaida, hapa maana yake anaamiwa na wengi, sasa kwa nini abadilishwe!??
Isomeke ni Waziri asiyeaminika/aminiwa na wengi
 
ukweli usiofichika January haaminiki na watz ,na hii inawafanya watu wasimuamini hata Kama Kuna mahali amefanya kaz kwa uaminifu,watu hawana Imani nae!! kwa hali hii itamfanya wizara iwe nzito kwake ,lakini pia hata watendaji wake watafanya Kaz ktk mazingira yasio ya kuaminiwa na wananchi.Hii wizara inahitaji mtu anayeaminika na watu.

Sidhani kama kuna mtu anayeaminika ndani ya CCM. Ndani ya CCM wamejaa watu wanafiki, waongo, wadanganyifu, wevi na uchafu wa kila namna.

Leo hii, ndani ya CCM, kuanzia Rais, mawaziri, wabunge, madiwani mpaka wenyeviti wa Serikali za mitaa, yupo hata mmoja anayeweza kusema alichaguliwa na wananchi kwa mchakato safi, wa wazi na wa haki kabisa?

January na Nape, ndio waliwekwa kuwa viongozi kwaajili ya kuiba kura kumpa Magufuli 2015, Kalemani hakuchaguliwa na wananchi bali na marehemu, sawa na walivyo wote wanaoitwa wabunge wa bunge hili la sasa.

Sasa, unataka kuniambia huwa kuna mwizi anayeaminika?

Tunaongozwa na chama na viongozi wanaoamini katika wizi, unafiki na uwongo. Je, utakwepa vipi uchafu wa kila aina nchini? Vyovyote utakavyofanya, utakuwa unatafuta unafuu katika uchafu, lakini huwezi kupata kilicho safi.
 
January si Waziri asiyeaminiwa na wengi hata michango ya watu iwe mitaani ama humu mitandaoni ukweli huo unajidhihirisha.

Sasa ili kuwe na kuaminika tena kwa matatizo yahusuyo Nishati nikuombe Rais Samia teua Waziri mwenye japo chembe ya kuaminika na wengi wetu awe Waziri wa Wizara hiyo.

Bado wapo watu katika baraza lako wenye ushawishi kwa wananchi mfano mzee Lukuvi ni mmoja ya Waziri mwenye kauli inayopokelewa na wengi na ni mtu anayeaminika na watu japokuwa naye ni mwanadamu na mapungufu yake.

Kumpa January nishati ni kumchonganisha na watu tu hali itakayomfanya awe na stress zaidi.

Nashauri,January atafutiwe Wizara nyepesi kwa sababu hata yeye ni mwepesi.
Akatweet tena huko tweeter
 
Mzima na anachapa kazi, wametumwa ,na mabeberu zidumu fukira zangu,tutakula ugali wa dona,nyumbu wanatoka chama C kwenda chama C wakifika huko wanaombewa na kuzaliwa upya
 
Utafiti huo wa kutoaminika huyo waziri Makamba umeufanya mitaa mingapi nchi hii ya wakazi milioni 60?!!!

Majungu na fitna tu yamewajaa......

#SiempreJMT
 
Naunga mkono hoja, apewe mtu asie na rekodi mbaya ya upigaji, huko CCM kila siku wanajisifu wana hazina ya viongozi sasa kwanini wanarudia kuteua sura zile zile zilizopoteza credibility?
 
Back
Top Bottom