Nakumbuka siku moja nimepanda basi la kampuni X nimeweka kibegi changu kwenye keria hizo. Safari ikawa inaendelea tulikuwa tunatoka dar kwenda arusha. Kufika hedaru gari likaharibika bana, abiria wote tukashuka kusubiri litengamae, lilivyokaa sawa kuja kufika moshi ishafika saa mbili usiku mi nikaona nisiendelee na safari nitalala moshi. Katika harakati za kuondoka nikabeba begi kumbe sio langu. Nikalibeba na kusepa mpaka pale kindoroko. Lakwangu lilikuwa na nguo na viatu tuu. Kufika room nakagua nakuta nguo ambazo sio zangu, kukagua kagua naona mfuko wa rambo mweusi, nikaufungua na kupekenyua nakutana na maburungutu ya pesa na kipistol. Jaribu kutafta vitambulisho hamna. Nikahesabu ile hela ilikuwa milioni 25 cash. Kesho yake nikaenda ofisini kwenye hio kampuni nikakuta tayari ripoti zipo za mtu kupotelewa na begi. Lile lakwangu lishaletwa pale na jamaa yupo ana wenge balaa ila uzuri hakusema kilichopo ndani. Nikaongea naye akaniambia alikuwa na haraka hivyo akachanganya mabegi. Nikamuhoji ndani kulikuwa na nini mule kwa bag yake. Akasema vyote, tukaongozana mpaka pale kindoroko. Ile kufika tuu naona mtu anatoka chumbani kwangu, na sa hio nliomba nisifanyiwe usafi ndani kwangu. Aiseeh to cut short hii story nlimkabidhi vitu vyake, ila yule mwamba mpaka leo yupo karanga ananyea debe.