Wizi wa kwenye mabasi wanaswa na kamera ya bus la ABC

Wizi wa kwenye mabasi wanaswa na kamera ya bus la ABC

Mimi pia

Huu wizi umetawala sana kipindi hiki Cha vyuo kufugwa....

Miaka 12 iliyopita nilikua nasafir kwenda Mwanza...wapo wezi ambao hukata tiketi kabisa na kusafir Kwa lengo la kuiba laptop [emoji335]

Tumefika Dodoma tukaenda kula kurudi garini dada haoni begi lake la laptop na vitu vingine....

Yaan tukachukuliwa gari zima mpaka DODOMA CENTER POLICE

Kila mtu anatoka na mizigo yake inafunguliwa na kumwagwa [emoji368] [emoji368][emoji368] searching na police na gari zima tu searchiwa mwanzo mwisho....

Mwisho wa siku hakupata chochote na Kuna abilia mwingine mmoja hakuwepo kwenye siti yake so izo mambo zipogo sanaa.....
Kwa hesabu za kawaida tu, tuseme laptop ya laki 3, Mwizi katumia angalau elfu 30 ya nauli ili akaibe. Atapata faida akiiba.
 
vijana wa siku hizi wajinga sana always nawaambiaga, the first sign to anything ndio ukweli wenyewe vinavyofuata ni ubongo unakuongopea.

yaani wakati anainuka kwa nguvu first sign imemwambia ni begi lako ndo limeondoka. kuangalia kweli halipo, lakini ubongo ukaanza kuongopa na kumwambia hawezi kuwa huyo mzee, ubongo ukamwambia tena bag lipo nje.

vijana hamnisikilizi haya, mmelala sana dku hizi fanyeni mazoezi.
Vijana muda wote anaasikiliza

Honeyyyy honeyyyyy honeyyyy

Kavaa earphones

Ova
 
Na jamaa nae ana kauzembe na uoga kwenye vitu vyake na kupumbazwa na tv.

Hapo kuna kikamba kilikua kinaning'inia hapo kumpa ishara kua begi lipo.
Akapata wenge kikamba kilipokua kinasogezwa akashtuka lakini ndo ile umdhanie ndie kumbe siye. Akamuamini mvaa kapelo.

Na begi lenyewe sio kubwa, kwanini asikae nalo.
Yani atajutia sana jamani..ukute lecturer kuna mtihani ya UE humo hahahh
 
Nakumbuka siku moja nimepanda basi la kampuni X nimeweka kibegi changu kwenye keria hizo. Safari ikawa inaendelea tulikuwa tunatoka dar kwenda arusha. Kufika hedaru gari likaharibika bana, abiria wote tukashuka kusubiri litengamae, lilivyokaa sawa kuja kufika moshi ishafika saa mbili usiku mi nikaona nisiendelee na safari nitalala moshi. Katika harakati za kuondoka nikabeba begi kumbe sio langu. Nikalibeba na kusepa mpaka pale kindoroko. Lakwangu lilikuwa na nguo na viatu tuu. Kufika room nakagua nakuta nguo ambazo sio zangu, kukagua kagua naona mfuko wa rambo mweusi, nikaufungua na kupekenyua nakutana na maburungutu ya pesa na kipistol. Jaribu kutafta vitambulisho hamna. Nikahesabu ile hela ilikuwa milioni 25 cash. Kesho yake nikaenda ofisini kwenye hio kampuni nikakuta tayari ripoti zipo za mtu kupotelewa na begi. Lile lakwangu lishaletwa pale na jamaa yupo ana wenge balaa ila uzuri hakusema kilichopo ndani. Nikaongea naye akaniambia alikuwa na haraka hivyo akachanganya mabegi. Nikamuhoji ndani kulikuwa na nini mule kwa bag yake. Akasema vyote, tukaongozana mpaka pale kindoroko. Ile kufika tuu naona mtu anatoka chumbani kwangu, na sa hio nliomba nisifanyiwe usafi ndani kwangu. Aiseeh to cut short hii story nlimkabidhi vitu vyake, ila yule mwamba mpaka leo yupo karanga ananyea debe.
 
AISEEE!!!

Mwizi aliekwapua begi kavaa kiheshima huwezi kumdhania, hata alieibiwa kampisha apite kiheshima.

Kavaa miwani kujifeki kaelimika / mtu wa hekima.
kofia yenye bendera ya nchi kuonekana mzalendo
shati la kitenge kuonekana mtu wa maadili ya kiafrika
mkononi ana maji kuzuga kipaumbele chake ni afya.

Ndio maana mimi begi ambalo silichungi huwa ni lile kubwa la nguo, begi dogo lazima niwe nalo muda wote pembeni maana naweka laptop, Simu, nyaraka, vyeti, pesa, n.k, yani hata nikienda kuchimba dawa ninalo.

View attachment 2733646
Good. Na kuchunga mzigo wako ndani ya basi hakikisha kwamfano siti yako iko upande wa kushoto, basi pachika mzigo wako kwenye keria iliyo mbele ya siti yako upande wa kulia, ni rahisi kuuchunga mzigo wako na kubaini movement za abiria kwa urahisi muda wote na kwa nafasi.

Hili la kuweka juu ya siti uliyokaa, ni rahisi sana kutaimiwa bila kumbaini mwizi kwa urahisi.
 
Back
Top Bottom