Wizi wa mapato ya Serikali katika Bandari ya Dar es Salaam ndiyo sababu kubwa ya DP World kukabidhiwa

Wizi wa mapato ya Serikali katika Bandari ya Dar es Salaam ndiyo sababu kubwa ya DP World kukabidhiwa

Vipi kama DPW nae asipokuwa muaminifu, tutaweza kumdhibiti?. Unawezaje kumlea mtoto wa jirani wakati umeshindwa kumlea mtoto wako wa kumzaa?.
Hapa ndipo kazi ilipo
 
Kama kuna uchaguzi Mkuu 2025, mama yule akichukua fomu kupitia rangi ya kijani , chama kitapata wakati mgumu kuliko 2015.

Kuna dalili mama yule kauza kila kitu kwenye zile MOU 36, na ukimwangalia usoni hana aibu kabisaaa wala hapepesi macho.
 
Haya ni matusi mengine tu kuja kutaka kuhalilisha Uwekezaji wa kinyonyaji na hatari wa Usalama wa Taifa.

Manake kama hoja ni kuwa akiwa mtu binafsi hawezi kuwa anakubali anaibiwa.

Kwanini wasibinafsishe na kuwagawia hawa mabilionea wetu hapa Nchini?
Hapa kwenu nani mwenye uwezo wa kuwekeza tirilioni sitta?mtaje tumjue
 
Kumekuwa na malalamiko makubwa sana kwa bandari ya Dar es Salaam kukabidhiwa kwa DP World, lakini sababu kubwa zaidi ni wizi wa mapato ya Serikali uliokithiri pamoja na dhuluma kubwa kwa wateja wanaoagiza mizigo bandarini.

Mizigo inayopita bandarini ni mingi sana lakini Serikali imekuwa haipati mapato sahihi ya bandari hiyo kwani fedha hizo zimekuwa zikidhulumiwa tangu kipindi cha Mwl Nyerere na hata alipokuja Dr Magufuli wizi huu ulimkera sana na kujaribu kuchukua hatua ambazo hazikuzaa matunda.

Watanzania tujitoe boliti kwenye macho yetu ndipo tumnyooshee kidole raisi Samia Suluhu Hassan pamoja na Serikali kwa uamuzi waliochukua.

Watanzania tujiulize je tumekuwa tukipeleka mapato sahihi serikalini kama tulivyopaswa kufanya? Je hatukuwa tukidhulumu wateja wanaoagiza mizigo kupitia bandari hiyo? Lengo la Serikali kuleta wawekezaji DP World ni kupata mapato makubwa kwasababu ya uendeshaji wao mzuri wa bandari usiokuwa na hujuma.

Kama kusingekuwa na wizi na ubadhilifu unaofanyika bandarini basi Serikali isingewakumbuka wawekezaji wa nje ya nchi.

Watanzania tujifunze kuacha hujuma kupitia uamuzi huu wa DP World kwenye mali za Serikali kwasababu kadiri itakavyozidi kukosa mapato sahihi ndipo itazidi kualika wawekezaji kutoka nje ya nchi yetu ili wasimamie kwa haki.

Reference:
Kuna vitu hutakiwi kua hata na elimu ya std 5,hiyo bandari pesa yote na ufisadi wanapiga serikali ya ccm...wewe ulitakiwa utoe ushauri wabinafsishe Chama chao cha CCM kwanza...mana ndio kimefreli kwenye kila jambo,walichoweza ni UFISADI kwa kiwango cha juu
 
Kwanini wezi hawafikishwi mahakamani?
Kulea wezi, wazembe na wabadhirifu ni mfumo rasmi wa CCM ulioasisiwa tangu enzi za Nyerere. Haribu hapa, tukuhamishie kule
Mimi ningeona wana akili kubwa ya kujenga nchi yetu,kama chama cha CCM kinge binafsishwa kwa waarabu...mana walichoweza kwa 400% ccm ni ufisadi tu
 
Kama wizi ndio sababu ya ubinafusishaji tuchukue ripoti ya cag na sehemu zote zilizotajwa kuhusika na wizi wabinafusishe
 
Haya ni matusi mengine tu kuja kutaka kuhalilisha Uwekezaji wa kinyonyaji na hatari wa Usalama wa Taifa.

Manake kama hoja ni kuwa akiwa mtu binafsi hawezi kuwa anakubali anaibiwa.

Kwanini wasibinafsishe na kuwagawia hawa mabilionea wetu hapa Nchini?
Acha wizi ..ungekuwa karibu yangu ningekupiga kofi la mgongo
 
Watu wengi hawajui ukweli wao ni ushabiki tuu, na ndio maana hata Rostam Azizi, Godless Lema, General Ulimwengu, Sheikh Ponda, Padre Kitima na wengine wengi tuu, katika mkutano pale SERENA alitutahadharisha kuwa tujadili kwa hoja wala sio ushabiki kwani maendeleo hayachagui Chama, Dini wa Ukabila.
Mkuu "watake wasitake" hili la Bandari lazima DP World waje na walete ufanisi ili Serikali iweze kupata mapato hakuna haya ya kubembelezana kwenye issues zenye maslahi mapana kwa nchi.
Tatizo wawekezaji hao ni waarabu sasa
 
Serikali hii inatia aibu. Ccm itoke ituachie Tanganyika yetu
.
20230509_210058.jpg
 
Acha wizi ..ungekuwa karibu yangu ningekupiga kofi la mgongo
Nakuhakikishia, baada ya ya matusi yako haya utatamani kuukata ulimi wako. Usiechezee himaya za watu usiowajua....

Huna sababu yeyote ile ya msingi zaidi ya kuendeleza lugha na misamiati ya Ukimbari iliyoibuka dhidi ya mtu Mweusi.

Again, haya matusi yenu/yako ndi yanazidi kuhalalisha upinzani dhidi ya DPW.
Mtashindwa
 
Hapa kwenu nani mwenye uwezo wa kuwekeza tirilioni sitta?mtaje tumjue
Hujui unachouliza hapa. Watanzania tumewekeza Zaidi ya Trillioni mbili chini ya Miaka miwili....tuhakikishiwe kuwa tunalipwa/tulipwe Fedha zetu tulizowekeza.
 
Je tunaweza mtenganisha mswahili na upigaji ili tuendelee?
Ha ha mmepata sehemu ya kuendeleza kufanya ugaidi wa mtandaoni na matusi yenu tu. Na kama ulikuwa hujui, hawa Waarabu wote wanajisifia kuwa ni Waswahili, wanajisifia kuwa ni Wazanzibari! Sasa kama nilivyosema huko juu.....Haya ni matusi dhidi ya Mtu mweusi, hayana tofauti yeyote ile na matusi ya Mwarabu, Mzungu dhidi ya Mtu mweusi. Lakini, Ukumbuke pia, Madhalimu ya Dunia hii ni kina nani. Usijiondoe ufahamu!

Hakuna sehemu yeyote ile katika mkataba ule, hakuna sehemu yeyote ile katika bunge la Jamhuri , hakuna sehemu yeyote ile katika ripoti za Kitaalamu iliyosema, Iliyotoa sababu kuwa ni "Wizi" ndio uliowafanya DPW wagaiwe Bandari, As a matter of fact hakuna sababu zezote zile za msingi zinazowapa Serikali kugawa bandari Bure kwa Maharamia wakiarabu zaidi ya Ukaribu na Rushwa iliyotamalaki....itoshe kusema nyuma ya pazia hili ni bakuli kubwa-Nimeliita robota sehemu nyingine- ya kuja kununua Uchaguzi wa 2025.

Ninasimama kidete na maneno yangu. Nikuhakukishie, kwenye makorido ya Ofisi kuna watu hawaonani nyuso kwa nyuso na kwa muendelezo huu wa kejeli, na unyanyasaji ni suala la muda tu kuwa wale mnaowatetea watakuja kuumbuka.

2025 sio mbali. Tutachagua kwa Umakini mkubwa sana.....Majambazi nje!
 
Umenena mkuu
 
Back
Top Bottom