Ego is the Enemy
JF-Expert Member
- Mar 21, 2014
- 8,201
- 16,246
Kumekuwa na malalamiko makubwa sana kwa bandari ya Dar es Salaam kukabidhiwa kwa DP World, lakini sababu kubwa zaidi ni wizi wa mapato ya Serikali uliokithiri pamoja na dhuluma kubwa kwa wateja wanaoagiza mizigo bandarini.
Mizigo inayopita bandarini ni mingi sana lakini Serikali imekuwa haipati mapato sahihi ya bandari hiyo kwani fedha hizo zimekuwa zikidhulumiwa tangu kipindi cha Mwl Nyerere na hata alipokuja Dr Magufuli wizi huu ulimkera sana na kujaribu kuchukua hatua ambazo hazikuzaa matunda.
Watanzania tujitoe boliti kwenye macho yetu ndipo tumnyooshee kidole raisi Samia Suluhu Hassan pamoja na Serikali kwa uamuzi waliochukua.
Watanzania tujiulize je tumekuwa tukipeleka mapato sahihi serikalini kama tulivyopaswa kufanya? Je hatukuwa tukidhulumu wateja wanaoagiza mizigo kupitia bandari hiyo? Lengo la Serikali kuleta wawekezaji DP World ni kupata mapato makubwa kwasababu ya uendeshaji wao mzuri wa bandari usiokuwa na hujuma.
Kama kusingekuwa na wizi na ubadhilifu unaofanyika bandarini basi Serikali isingewakumbuka wawekezaji wa nje ya nchi.
Watanzania tujifunze kuacha hujuma kupitia uamuzi huu wa DP World kwenye mali za Serikali kwasababu kadiri itakavyozidi kukosa mapato sahihi ndipo itazidi kualika wawekezaji kutoka nje ya nchi yetu ili wasimamie kwa haki.
Reference:
Kiuhalisia jpm ilikuwa bahati mbaya kuzaliwa afrika. Alitakiwa azaliwe China,Russia,Cuba,USA and Europe ,hii mbegu haikutakiwa kuwepo kwenye nchi ambazo watu wanatanguliza matumbo yao kuliko maslahi ya nchi kwanza. Jamaa Ni kichwa kwa kweli nadhani hata wazungu walikuwa wanamkubali Kiana yaani ndani kwa ndani. Ila ngoja wamekuja wajanja maboni town, wasio malimbukeni ,not cowboys,ngoja tumalizane do wedi,tunakuja brt later sgr Mana waafrika hawezi kujisimamia wao wenyewe alijaribu gadafi naye Ni mwarabu ,tomasi Sankara aliuwa. Afrika Kuna kalaana sio bure am sure.
Acha tukomae kuongeza nguvu za kiume,kusimamia kucha,kula kimasihara,tubeti,Simba na yanga,later cdm vs ccm.
Hii demokrasia hakikuwepo huko ulaya walipokuwa na Hali Kama hii yetu,yaaani mababu yalitumika kuzinyanyua nchi zao. Someni history,unaleta mdomo kwenye kazi ,fanya kazi.
Ngoja kwanza tumesaini hapa mktaba wa software ya kufuatilia umeme kukatika na kampuni ya kihindi kwa 69bn ,huku huko kijijini watt wanasoma wanakaa chini na bado mnaleta siasa.
Naomba mno mifupa iozee ulaya ila sio afrika.
Wale blacks USA wameshajua kuwa kwao Ni huku Ila hakuna anayejaribu kurudi yaani Bora wabaguliwe kule kule wamechomwa Moto Ila hawarudi
Afrika tunaweza ngono, starehe full stop