Wizi wa mapato ya Serikali katika Bandari ya Dar es Salaam ndiyo sababu kubwa ya DP World kukabidhiwa

Vipi kama DPW nae asipokuwa muaminifu, tutaweza kumdhibiti?. Unawezaje kumlea mtoto wa jirani wakati umeshindwa kumlea mtoto wako wa kumzaa?.
Hapa ndipo kazi ilipo
 
Kama kuna uchaguzi Mkuu 2025, mama yule akichukua fomu kupitia rangi ya kijani , chama kitapata wakati mgumu kuliko 2015.


Kuna dalili mama yule kauza kila kitu kwenye zile MOU 36, na ukimwangalia usoni hana aibu kabisaaa wala hapepesi macho.
 
Hapa kwenu nani mwenye uwezo wa kuwekeza tirilioni sitta?mtaje tumjue
 
Kuna vitu hutakiwi kua hata na elimu ya std 5,hiyo bandari pesa yote na ufisadi wanapiga serikali ya ccm...wewe ulitakiwa utoe ushauri wabinafsishe Chama chao cha CCM kwanza...mana ndio kimefreli kwenye kila jambo,walichoweza ni UFISADI kwa kiwango cha juu
 
Kwanini wezi hawafikishwi mahakamani?
Kulea wezi, wazembe na wabadhirifu ni mfumo rasmi wa CCM ulioasisiwa tangu enzi za Nyerere. Haribu hapa, tukuhamishie kule
Mimi ningeona wana akili kubwa ya kujenga nchi yetu,kama chama cha CCM kinge binafsishwa kwa waarabu...mana walichoweza kwa 400% ccm ni ufisadi tu
 
Kama wizi ndio sababu ya ubinafusishaji tuchukue ripoti ya cag na sehemu zote zilizotajwa kuhusika na wizi wabinafusishe
 
Acha wizi ..ungekuwa karibu yangu ningekupiga kofi la mgongo
 
Tatizo wawekezaji hao ni waarabu sasa
 
Acha wizi ..ungekuwa karibu yangu ningekupiga kofi la mgongo
Nakuhakikishia, baada ya ya matusi yako haya utatamani kuukata ulimi wako. Usiechezee himaya za watu usiowajua....



Huna sababu yeyote ile ya msingi zaidi ya kuendeleza lugha na misamiati ya Ukimbari iliyoibuka dhidi ya mtu Mweusi.

Again, haya matusi yenu/yako ndi yanazidi kuhalalisha upinzani dhidi ya DPW.
Mtashindwa
 
Hapa kwenu nani mwenye uwezo wa kuwekeza tirilioni sitta?mtaje tumjue
Hujui unachouliza hapa. Watanzania tumewekeza Zaidi ya Trillioni mbili chini ya Miaka miwili....tuhakikishiwe kuwa tunalipwa/tulipwe Fedha zetu tulizowekeza.
 
Je tunaweza mtenganisha mswahili na upigaji ili tuendelee?
Ha ha mmepata sehemu ya kuendeleza kufanya ugaidi wa mtandaoni na matusi yenu tu. Na kama ulikuwa hujui, hawa Waarabu wote wanajisifia kuwa ni Waswahili, wanajisifia kuwa ni Wazanzibari! Sasa kama nilivyosema huko juu.....Haya ni matusi dhidi ya Mtu mweusi, hayana tofauti yeyote ile na matusi ya Mwarabu, Mzungu dhidi ya Mtu mweusi. Lakini, Ukumbuke pia, Madhalimu ya Dunia hii ni kina nani. Usijiondoe ufahamu!

Hakuna sehemu yeyote ile katika mkataba ule, hakuna sehemu yeyote ile katika bunge la Jamhuri , hakuna sehemu yeyote ile katika ripoti za Kitaalamu iliyosema, Iliyotoa sababu kuwa ni "Wizi" ndio uliowafanya DPW wagaiwe Bandari, As a matter of fact hakuna sababu zezote zile za msingi zinazowapa Serikali kugawa bandari Bure kwa Maharamia wakiarabu zaidi ya Ukaribu na Rushwa iliyotamalaki....itoshe kusema nyuma ya pazia hili ni bakuli kubwa-Nimeliita robota sehemu nyingine- ya kuja kununua Uchaguzi wa 2025.

Ninasimama kidete na maneno yangu. Nikuhakukishie, kwenye makorido ya Ofisi kuna watu hawaonani nyuso kwa nyuso na kwa muendelezo huu wa kejeli, na unyanyasaji ni suala la muda tu kuwa wale mnaowatetea watakuja kuumbuka.

2025 sio mbali. Tutachagua kwa Umakini mkubwa sana.....Majambazi nje!
 
Umenena mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…