Kuna watu wanafikiria Tanzania kuwa nchi maskini ni sifa kwa mabwana zao
Sikia neno hapa
View attachment 1848789
Ukifikiri vizuri, kwa utulivu - kwa upana na urefu na kina; there is only one conclusion; Umaskini wa Tanzania unatokana na CCM, Yaani CCM ndio mhimili wa umaskini wa nchi na wananchi wa Tanzania - kwa sera mbovu, uongozi mbovu na ukosefu wa dira na welede ambao umejikita katika kila ngazi ya CCM.
Hivyo ili kuondoka na umaskini lazima CCM iondoke madarakani - kwa njia za kisheria (hasa hili la Katiba) au kwa njia nyinginezo. Hapo ndipo Tanzania, seriouly, itaanza kuondoka kwenye umaskini.
Hizi legacy za mwendazake mnapata tabu sana kuzitetea, maana hazina miguu wala uhai ndani yake. Ni ulevi wa waliooshwa akili/ufahamu tu.
Nafikiri unajua wazi kuwa hayati Magufuli alibumba takwimu kuonesha uchumi unapaa, ufisadi umekomeshwa na eti kuna "maendeleo" nk, ilichukua chini ya siku 60 tu toka afe kwa hizo propaganda kusambaratishwa.
1) Rejea ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali - Bandari, Wizara - kama Maliasili, Nishati, Afya, Fedha; Mashirika ya Umma, Taasisi -mfano Zimamoto, Polisi nk na Halmashauri zaidi ya 40 jinsi hela zilivyopigwa kwenye malipo, manunuzi na miradi "hewa".
2) Hotuba ya Mh. Rais Samia, kuwa hali ya uchumi si nzuri. Na uchumi ulikuwa unakuwa kwa asilimia 4.7 badala ya 6,7-7 za hayati Magufuli.
3) Yaliyojiri kwa Bunge la Bajeti - yalionyesha ombwe la uongozi wa awamu ya 5. Yalionyesha jinsi uongozi mbovu wa CCM unavyoendelea kulididimiza Taifa letu. And by the way, umeona quality ya Wabunge na michango ya wabunge wa hayati Magufuli? Lile halistahili kuitwa Bunge la JMT bali la hayati Maguguli.
4) Somo Jipya la Historia ya Tanzania (Revisionism) - hata vitabu vya hiyo historia ya Tanzania vilichapwa na vilikuwa vianze kutumika mwezi huu wa Julai mashuleni.
5) TRA kufungua bank accounts walizokuwa wameiba na kudhulumu watu.
6) Kufumuliwa na kutupwa kesi lukuki za kubambikia - Rufaa ya Viongozi wa CHADEMA na faini ya shs 350m, kesi ya Mdude, na nyinginezo nyingi
7) Taifa kuvuta hewa mpya, fresh kwa mara ya kwanza toka 2016. Yako mengine mengi,ila kwa sasa tuko kwenye Katiba Mpya.
Kwa kifupi, tunamshukuru sana na kumtukuza Mwenyezi MUNGU kwa kumwondoa Magufuli. Legacy yake ni kuwa alikuwa mtu mbaya, katili, kichaa, asiye na weledi wala uwezo wa kuongoza. Matendo ya BWANA ni ya haki na kweli, na hiyo ndiyo alama na kumbukumbu tuliyonayo sisi wenye akili njema na wenye upendo wa dhati na nchi yetu.