Wosia wa Mirathi ya Dkt. Reginald Mengi: Jacqueline Ntuyabaliwe adondokea pua

Nna wasiwasi na mapenzi yake kwa mzee...sidhani kama alikuwa na true love

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
Mahakama imetenda haki.

Kwenye kile kifungu kwenye wosia eti atakae jaribu kuweka pingamizi kwenye maamuzi aliyoyatoa marehemu mzee mengi iwapo atashinda kesi apatiwe Buku. Ndio nilijua wanawake wa kuokoteza uzeeni sio wazuri
 
Ni bora pesa zimebaki kwa familia naamini kabisa utajiri utaendelea kuwanufaisha watanzania huyu mwanamke mbona angehamishia pesa kwenye starehe kubadilisha hotel uko kwa mabeberu

Jacky alitakiwa kumtunza sana Mzee wetu pamoja na kumtunzia heshma na furaha yake kwa kuwapenda watoto na ndugu zake

Sijui mshauri wake alikua nani
 

Love you crazy
 
Yaan kila kitu kilikua staged. Its only that ashukuru akina jk. Angekua anajisaidia kwenye kisado mida hii
 
Yes Jukumu La Msimamizi Wa Mirathi Ni Correction and contribution kwa Heirs Tu.
 


Hii ni baada ya Mahakama Kuu kuutupilia mbali wosia unaodaiwa kuandikwa na Mzee Mengi ambao ulielekeza kwamba Mali zote za Marehemu apewe Jackline na wanawe , huku Watoto wakubwa wa marehemu Mengi wasipewe chochote .

MhJaji Mlyambina wa Mahakama kuu amedai wosia uliopingwa na Mahakama hiyo uliandikwa wakati tayari Mzee Mengi akiwa anaumwa jambo ambalo linaifanya Mahakama ione kwamba hauwezi kuwa halali hasa ikizingatiwa kwamba aliyeandika hakuwa katika afya njema

Imewataja wasimamizi wapya wa mirathi hiyo kuwa ni Abdiel Mengi na Benjamin Mengi

Chanzo : Watetezi TV
 
Mahakama Kuu ya Tanzania Masijala ya Dar es Salaam imetoa uamuzi kuwa watoto wa Marehemu Reginald Mengi;-Abdiel na Benjamin Mengi kuwa wasimamizi wa mirathi ya mali alizoacha marehemu baba yao (Reginald Mengi). Katika uamuzi huo, mahakama imeagiza usimamizi na mgawanyo wa mirathi uanze mara moja.
-
Akisoma hukumu hiyo yenye kurasa 72 mnamo Mei 18/2021 Jaji Mlyambina alisema kuwa wosia wa mwisho wa Marehemu Dkt. Mengi ulioandikwa Agosti 17,2017 haukuzingatia misingi ya kisheria ya uandishi wa wosia.
-
Katika shauri hilo watoto wa marehemu Dkt. Mengi walikuwa wakipinga wosia uliodaiwa kuachwa na Marehemu baba yao kwa madai kwamba wosia huo haukufungwa ‘sealed’ na saini iliyopo kwenye wosia huo ni tofauti na sahihi zingine za Marehemu na pia kwa wakati huo baba yao hakuwa na uwezo wa kuandika kutokana na matatizo makubwa ya kiafya aliyokuwa nayo tangu mwaka 2016.
-
Aidha watoto hao walidai kuwa wosia uliwabagua na urithi wote aliachiwa mkewe mpya na watoto mapacha na hivyo wosia huo ulikuwa kinyume na sheria sababu uliwabagua watoto bila sababu za msingi na za kisheria.
View attachment 1791204
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…