Wosia wa Mirathi ya Dkt. Reginald Mengi: Jacqueline Ntuyabaliwe adondokea pua

Wosia wa Mirathi ya Dkt. Reginald Mengi: Jacqueline Ntuyabaliwe adondokea pua

Kwan uliambiwa yule mzee alikuwa na shida ya uhusiano na huyo binti?!

Binti ndie alikuwa anamuwinda mzee. Kategeshea ujauzito ili amshike akili vizuri mzee, ndoa unaambiwa alifosi ikafungiwe nje ya inchi ili kuepusha matatizo toka familia ya mwanaume.

So hili unalosema lisingewezekana.
wewe bwana acha tantalilia mwanaume gani hapa duniani hapend kukojolea mbususu nzuri kama ya yule mrembo?
pili kama angekuwa hana shida ya mahusiano na yule mlimbwende he coud have easily offered her an offer she cant refuse, ana sasambua mbusus alafu hatujuani.
 
Kipindi chote alichokuwa na mahusiano na mzee nna uhakika hizo b3 za kupiga tayari anazo tatizo lake ni tamaa ya kutaka mabilioni yote ya mzee mchana kweupe wakati mzee ana watoto ambao hakuwa hata matatizo nao....na katika hili naamini alichokuwa anasema mange kuna watu nyuma ya huyu mjinga walim push kufanya huu ujinga kwa maana watamsaidia ashinde kesi ili baadae wagawane hayo mabilioni
Mengi alikuwa na misunderstandings na familia yake kwa mke wa kwanza, sijui kama walimalizana hizo tofauti ila zilikuwapo.
 
Kesi Ya Mirathi ya ya Dr. Reginald Mengi: Former Miss Tanzania Jackline Ntuyabaliwe adondokea pua kwa Mara Ya nane tena katika Rufaa

View attachment 1790872

Mahakama Kuu ya Tanzania Masijala ya Dar es Salaam imetoa uamuzi kuwa mtoto wa Marehemu Reginald Mengi;-Abdiel na kaka wa marehemu, Bw. Benjamin Mengi kuwa wasimamizi wa mirathi ya mali alizoacha marehemu (Reginald Mengi). Katika uamuzi huo, mahakama imeagiza usimamizi na mgawanyo wa mirathi uanze mara moja.

Akisoma hukumu hiyo yenye kurasa 72 mnamo Mei 18/2021 Jaji Mlyambina alisema kuwa wosia wa mwisho wa Marehemu Dkt. Mengi ulioandikwa Agosti 17,2017 haukuzingatia misingi ya kisheria ya uandishi wa wosia.

Katika shauri hilo watoto wa marehemu Dkt. Mengi walikuwa wakipinga wosia uliodaiwa kuachwa na Marehemu baba yao kwa madai kwamba wosia huo haukufungwa ‘sealed’ na saini iliyopo kwenye wosia huo ni tofauti na sahihi zingine za Marehemu na pia kwa wakati huo baba yao hakuwa na uwezo wa kuandika kutokana na matatizo makubwa ya kiafya aliyokuwa nayo tangu mwaka 2016.

Aidha watoto hao walidai kuwa wosia uliwabagua na urithi wote aliachiwa mkewe mpya na watoto mapacha na hivyo wosia huo ulikuwa kinyume na sheria sababu uliwabagua watoto bila sababu za msingi na za kisheria.

=====

Dar es Salaam. Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imeukataa wosia uliokuwa ukidaiwa kuandikwa na aliyekuwa mfanyabiashara maarufu nchini marehemu Reginald Mengi pamoja na mambo mengine ikieleza kuwa haukidhi matakwa ya kisheria ili kuwa wosia halali.

Uamuzi huo ulitolewa jana na Jaji Yose Mlyambina kufuatia shauri la mirathi lililokuwa limefunguliwa na watu wanne wakiwemo ndugu wa marehemu, wakiomba kuteuliwa kuwa wasimamizi wa mirathi hiyo.

Jaji Mlyambina amefikia uamuzi huo baada ya kukubaliana na hoja za pingamizi lililowekwa na mmoja wa watoto wakubwa wa marehemu Mengi pamoja na ndugu yake marehemu Mengi, waliokuwa wakipinga uhalali wa wosia huo.

Shauri hilo la mirathi namba 39 la mwaka 2019 lilifunguliwa na Benson Benjamin Mengi, William Onesmo Mushi, Zoebu Hassuji na Sylvia Novatus Mushi wakiomba kuteuliwa kuwa wasimamizi mirathi hiyo kwa mujibu wa wosia huo.

Hata hivyo, mtoto wa Marehemu Mengi, Abdiel Reginald Mengi na ndugu wa marehemu Mengi, Benjamin Abraham Mengi, waliweka pingamizi dhidi ya wosia huo, wakipinga uhalali wake huku wakiwasilisha jumla ya sababu nne za kuupinga.

Sababu hizo ni pamoja na kwamba haukwa umepigwa mhuri na saini iliyokuwepo ilikuwa ni tofauti na saini ya kawaida ya marehemu Mengi na kwamba haukushuhudiwa na ndugu au mke wa marehemu.

Pia walikuwa wakidai kuwa marehemu hakuwa na uwezo wa kuandaa wosia kwa kuwa alikuwa na matatizo ya kiafya tangu mwaka 2016 na kwamba unaondoa katika urithi, watoto bila kuzingatia mila za Kichaga au kuhusisha ndugu.

Mahakama Kuu baada ya kusikiliza hoja za pande zote katika hukumu yake iliyosomwa juzi na Jaji Mlyambina na nakala yake kupatikana jana kwa matumizi ya umma, alikubaliana na hoja za pingamizi hilo dhidi ya wosia huo na kuikataa kuwa ni batili.

Jaji Mlyambina alikubaliana na sababu hizo za pingamizi na pamoja na mambo mengine, amesema kuwa inawanyima urithi wanaye bila kutoa sababu, na kwamba ziliiingizwa mali za mke wake mkubwa.

Kwa uamuzi huo, Jaji Mlyambina hakuwateua waombaji hao kuwa wasimamizi wa mirathi na badala yake aliwateua Abdiel na Benjamini kuwa wasimamizi wa mirathi na akaelekeza mali za marehemu zigawiwe warithi wanaostahili kwa utaratibu wa kawaida kama wa mtu ambaye hakuacha wosia.

Awali mjane wa marehemu Mengi, Jacquiline alijaribu kuingia katika shauri hilo bila mafanikio baada ya mahakama hiyo kutupilia mbali maombi yake mara tatu.

Credit: Mwananchi

Zaidi soma;

1). Thread 'Jacqueline Ntuyabaliwe Mengi: Nimezuiwa kuingia kwenye kaburi la mume wangu. Nimechoka na sitakubali' Jacqueline Ntuyabaliwe Mengi: Nimezuiwa kuingia kwenye kaburi la mume wangu. Nimechoka na sitakubali

2). Thread 'Hatimaye K Lyn (Jacqueline Ntuyabaliwe) achumbiwa na Reginald Mengi' Hatimaye K Lyn (Jacqueline Ntuyabaliwe) achumbiwa na Reginald Mengi

3). Thread 'Watoto wa Mengi wamburuza mahakamani Jacqueline Mengi "Klynn"' Watoto wa Mengi wamburuza mahakamani Jacqueline Mengi "Klynn"

4). Thread 'Unaodaiwa kuwa wosia wa Reginald Mengi huu hapa, mali zote ni za Jacqueline na watoto wake mapacha' Unaodaiwa kuwa wosia wa Reginald Mengi huu hapa, mali zote ni za Jacqueline na watoto wake mapacha

5). Thread 'Miaka 5 ya Anniversary ya Reginald Mengi na Jackline Mengi wote wafunguka' Miaka 5 ya Anniversary ya Reginald Mengi na Jackline Mengi wote wafunguka

6). Thread 'TANZIA: Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Reginald Abraham Mengi afariki dunia akiwa Dubai, UAE' TANZIA: Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Reginald Abraham Mengi afariki dunia akiwa Dubai, UAE
Huyu dada apunguze tamaa, vyovyote itakavyokuwa atapata... hii yakutaka kuchukua mali zote sio sawa.. waangalie wasije wakaanza kuuana sasa
 
Dada naona analialia twitter ila na majibu anayapata. Mimi nilitegemea angeelewa makosa yake kwa hiyo hukumu ila bado kichwa ngumu sasa asubiri kutoka damu masikioni maana atapewa 1,000. Mali wanapewa watoto yeye atapewa mkopo wa mtaji.
 
Aiseer. Weee nayeee... mali zake peke yake? Unaijua historia vizuri ya marehem na mkewe Mercy Shangali mjukuu wa mangi wewe? Ama wapaparika tu. Huoni hapo mali zingine zilikua za mke mkubwa? Kama hujuagi vitu tulia ufunzwe sheria japi kidogo. Mali za marehem mercy zinakuaje za mengi? Wosia wa marehem? Una kichaa kweli wewe. Ule unaamini ni wosia wa marehemu ule?
Kabla mke wa kwanza kufariki (Mercy), nasikia walishagawana mali kila mtu akaendelea na maisha yake hadi umauti unamkuta hapo juzi kati.

So kwenye hilo la mali kati ya mengi na mke wa kwanza naona walisha settle.

Ila kwa wanae wakubwa nadhani ndio kuna changamoto. Kilichotukia ni kuwa mzee aliwapa watoto wake wakubwa sehemu za miliki za za makampuni yake ila sio urithi. Sasa bi dada akajiamulia yeye kuwa watoto kupewa sehemu ya mali kuzisimamia ndio mgao wa urithi.
 
Ndio biashara za wadada wa mjini. Kama sio furniture basi saloon, boutique ama spa. Biashara za kislay queen
Hawataki biashara ya kuumiza kichwa...mambo sijui ya kuvaa gumboots sijui eti aingie shamba kukagua mpunga mara sijui ufugaji hawataki...wao wanataka ametoka nyumbani amepiga makeup anapanda gari anafika ofissini kakaa kwenye sofa anajisnap na kutupia insta...
 
Back
Top Bottom