Autodidacts
JF-Expert Member
- Jun 9, 2021
- 1,165
- 1,804
Hayati Magufuli a.k.a mwendazake aliwahi kukiri kuwa hakutarajia kuwa Rais wa awamu ya tano. Wengi tunakumbuka yaliyotokea, mpambano wa Membe na Lowassa ndio uliomzaa Magufuli kama suluhu ya kambi mbili pinzani ndani ya CCM wakati huo.
Mwendazake alipata heshima na makofi mengi ndani ya siku 100 kwa kauli mbiu ya kutumbua majipu, akapata na sifa nyingi bandia. Akageuza sifa, mapambio na heshima aliyopata kuwa sera ya nyongeza. Hakutaka tena kitu chochote mbadala,akalewa sifa na kuona hakuna Rais kama yeye wote waliomtangulia akawaona kama wezi na wanyang'anyi!
Kwa kawaida ya kimaumbile ya IQ ndogo, mwanadamu wa IQ ndogo anapofikia hatua aliyofikia mwendazake ya kulewa sifa huwa hataki kushuka wala kukosolewa. Matokeo ni kwamba kila anaekosoa anashughulikiwa, amri na ubabe utawala, sheria nazo uonekana ni adui mwingine ivyo mtoto anaezaliwa ni uundaji wa vikundi vya kiharifu vinavyolindwa na serikali kushughulika na wapinzani ili kulinda heshima ya Rais na sio katiba aliyoapia kuilinda. Baadae anazaliwa mtoto wa pili yaani udikteta!
Nimemsikia jana Rais Samia anaelekea kwa kasi kuumba kile kile cha mwendazake. Sasa anaona heshima yake ni bora kuliko katiba na matakwa ya wananchi. Kauli yake kuwa suala la katiba kusubiri uchumi ukue, utajiuliza je unaweza kupata maendeleo bila katiba yenye kukubaliwa na wengi? Kwa nini watu wasiwe huru kufanya mikutano kama katiba ya sasa inavyosema? Je kauli ya Rais kuweka masharti ya uhuru wa mikutano umezingtia sheria ipi inayozidi katiba au ni kauli binafsi tu kama ya mwendazake? Ni wazi ameanza kupingwa sana.
Sasa ni dhahiri mama kalewa sifa. Atapingwa. Ataanza kulinda sifa hizo na heshima aliyopewa kwa gharama, ivyo ataunda vikundi haramu kushughulika na wanaompinga, akina Sabaya wapya tuwatarajie!
USHAURI: Rais Samia aondokane na chawa wa mwendazake, achague upande wa wananchi na sio kikundi cha wachache wenye kulenga maslahi binafsi, atapata heshima ya kweli na ya kudumu badala ya hii heshima ya bandia na ya muda mfupi.