Wote wameingia kibahati na kutotarajia, Rais Samia hana jipya tena

ni chadema wacha kukimbia kivuli wewe mjusi.

mbona nyinyi kila aliyempinga mtu kabla mlimwita mataga??
Kwani ata nikiwa CHADEMA kuna shida?
Ni chama pekee chenye uthubutu na watu makini sana,najivunia sana hili chama. CCM ata ukiwa kiongozi mazuri au ata ukiwa profesa utaonekana kama mwehu wa barabarani sababu ya kundi la watu wa ovyo wasio na akili hasa vijana
 
Hayati Magufuli a.k.a mwendazake aliwahi kukiri kuwa hakutarajia kuwa Rais wa awamu ya tano. Wengi tunakumbuka yaliyotokea, mpambano wa Membe na Lowassa ndio uliomzaa Magufuli kama suluhu ya kambi mbili pinzani ndani ya CCM wakati huo.

Mwendazake alipata heshima na makofi mengi ndani ya siku 100 kwa kauli mbiu ya kutumbua majipu, akapata na sifa nyingi bandia. Akageuza sifa, mapambio na heshima aliyopata kuwa sera ya nyongeza. Hakutaka tena kitu chochote mbadala,akalewa sifa na kuona hakuna Rais kama yeye wote waliomtangulia akawaona kama wezi na wanyang'anyi!

Kwa kawaida ya kimaumbile ya IQ ndogo, mwanadamu wa IQ ndogo anapofikia hatua aliyofikia mwendazake ya kulewa sifa huwa hataki kushuka wala kukosolewa. Matokeo ni kwamba kila anaekosoa anashughulikiwa, amri na ubabe utawala, sheria nazo uonekana ni adui mwingine ivyo mtoto anaezaliwa ni uundaji wa vikundi vya kiharifu vinavyolindwa na serikali kushughulika na wapinzani ili kulinda heshima ya Rais na sio katiba aliyoapia kuilinda. Baadae anazaliwa mtoto wa pili yaani udikteta!

Nimemsikia jana Rais Samia anaelekea kwa kasi kuumba kile kile cha mwendazake. Sasa anaona heshima yake ni bora kuliko katiba na matakwa ya wananchi. Kauli yake kuwa suala la katiba kusubiri uchumi ukue, utajiuliza je unaweza kupata maendeleo bila katiba yenye kukubaliwa na wengi? Kwa nini watu wasiwe huru kufanya mikutano kama katiba ya sasa inavyosema? Je kauli ya Rais kuweka masharti ya uhuru wa mikutano umezingtia sheria ipi inayozidi katiba au ni kauli binafsi tu kama ya mwendazake? Ni wazi ameanza kupingwa sana.

Sasa ni dhahiri mama kalewa sifa. Atapingwa. Ataanza kulinda sifa hizo na heshima aliyopewa kwa gharama, ivyo ataunda vikundi haramu kushughulika na wanaompinga, akina Sabaya wapya tuwatarajie!

USHAURI: Rais Samia aondokane na chawa wa mwendazake, achague upande wa wananchi na sio kikundi cha wachache wenye kulenga maslahi binafsi, atapata heshima ya kweli na ya kudumu badala ya hii heshima ya bandia na ya muda mfupi.
Hahaha kwani si nyie mlisema mama anaponya nchi, leo imekuaje Bavicha??
 
Kwani ata nikiwa CHADEMA kuna shida?
Ni chama pekee chenye uthubutu na watu makini sana,najivunia sana hili chama. CCM ata ukiwa kiongozi mazuri au ata ukiwa profesa utaonekana kama mwehu wa barabarani sababu ya kundi la watu wa ovyo wasio na akili hasa vijana
aliyekwambia chadema wote wanawakilishwa na vijana wasomi na wenye uthubutu nani!!!

endelea kujivunia dhahania,lakini ukweli ni kwamba ni kama kundi la nyumbu wanaosikiliza na kwenda na kila hoja ya anayepingana na serikali.
 
aliyekwambia chadema woye wanawakilishwa na vijana wasomi na wenue uthubutu nani!!!

endelea kujivunia thahania,lakini ukweli ni kwamba ni kama kundi la wadudu wanaosikiliza na kwenda na kila hoja ya anayepingana na serikali.
Kuandika tu haujui,akili utaitoa wapi?
Unachoandika hakieleweki 🚮🚮
 
Rais Samia ana uwezo mdogo wa kufikiri na kupanga mambo kabla ya mambo kutayarishwa (thinking on her feet).

Ndiyo maana kajibu vibaya suala la kuruhusu mikutano, suala ambalo jibu lake limempa kesi ya kuvunja katiba.

Halafu, ana uwezo mdogo wa kuchuja habari na kujua hii uongo na hii ukweli.

Ndiyo maana kanukuu makala ya uongo kuhusu kujifukiza ili kuondoa Coronavirus.

Zaidi, hajui kutumia msaaada wa wasaidizi wake kumuandalia mambo ya kusema na kuchuja kipi ni fake news na kipi ni kweli. Hili ni jambo hatari sana kwa rais.
Mkuu samahani masahihisho kidogo

Kwenye ANA = HANA

All in all naunga mkono
 
Mkuu samahani masahihisho kidogo

Kwenye ANA = HANA

All in all naunga mkono
"ana uwezo mdogo wa kufikiri".

Maana yake hana uwezo mkubwa wa kufikiri.

Ukisema hana uwezo mdogo wa kufikiri sasa unataka kumuondolea kabisa uwezo wa kufikiri.

Mbakishie kidogo Rais wetu, katutoa mbali ujue kwenye matusi yale ya maneno ya kunya ya mwendazake.
 
Kama ni hivyo, huo ni udhaifu mkubwa tu.

Alitakiwa kujiandaa, alitakiwa kufanya mock interview na watu wa Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu. Yani angekaa Ikulu na ile team yake, halafu ile team yake inajifanya kama waandishi wa habari, wanampiga maswali yote vigongo. Anawajibu, wanamnoa, akikosea wanamrekebisha, wanamnoa, mpaka anakuwa kaweza vizuri.

Hawa viongozi wa nchi zilizoendelea kina Obama mara nyingine wanaonekana wana akili saaana, kumbe ni suala la kujiandaa vizuri tu na timu zao, kufanya hizi mock interviews, halafu wanarudia majibu waliyokariri.Wanaonekana kama wamesema palepale, ma genius.Kumbe walishajiandaa kitambo tu.

Kuna muandishi mmoja wa John Fitzgerald Kennedy, rais wa zamani wa Marekani, huyo jamaa alikuwa anaitwa Ted Sorensen. Ted Sorensen alikuwa anafanya hizi mock interviews na Kennedy, anajua positions za Kennedy, anajua majibu ya Kennedy, mpaka watu wakasema Sorensen ni kama ubongo wa pili wa Kennedy, unaweza kupata jibu la Kennedy kwa kumuuliza swali Sorensen.

Watu wanafanya kazi kitaasisi zaidi, kwa kuangalia sheria na policy zaidi, si kwa rais kujibu kitu kutoka kichwani hapo hapo tu.

Angefanya mock interview.Halafu baadaye akija kuwa na waandishi wa habari wa kweli, maswali mengi huwa yanajirudia yale yale muhimu, kwa hivyo, na yeye kama kajiandaa vizuri, anakuwa anarudia tu majibu ambayo kashayafanyia mazoezi.

Kwa mtindo huu, rais anakuwa hatoi kitu kichwani hapo hapo anapoulizwa swali, majibu yake yanakuwa yamepitiwa kitaasisi na Ikulu.

Hiki ni kitu muhimu sana, hususan kwa rais mpya ambaye hajazoea urais bado.

Sasa, inaonekana hajajiandaa. Na inawezekana ikawa si vibaya sana, wanasema kosa moja haliachishi mke. Lakini, hofu yangu ni kwamba kuna utamaduni wa kutojiandaa.

Amesema mwenyewe kwamba hakujiandaa kuwa rais, alijiandaa kuwa makamu wa rais.

Hili jambo linaonesha huyu hata kazi ya umakamu wa rais haielewi.

Ukisema hujajiandaa kuwa rais, umejiandaa kuwa makamu wa rais, kimsingi, maana yake ni kwamba, hata huo umakamu wa rais hujajiandaa nao.

Kwa sababu, makamu wa rais ni mtu anayeweza kuwa rais wakati wowote.Ndiyo maana tukaweka kipengele cha kusema, makamu wa rais ni mgombea mwenza wa rais.Tunapomchagua rais hatumchagui mtu mmoja, tunamchagua rais na mgombea mwenza. Rais akipata matatizo asiweze kuongoza nchi, akiumwa au akifariki, makamu wa rais anachukua nchi mara moja.

Sasa ile habari ya kwamba hajajiandaa kuwa rais inaonesha nini? Hakujua kwamba makamu wa rais anaweza kuwa rais siku yoyote? Au ndiyo fake modesty tu ambayo inakuwa inaonesha lack of depth?

Kama mtu anashindwa kujiandaa kujibu vizuri maswali mepesi ya waandishi wa habari wa Tanzania wenye heshima kubwa na woga mwingi, ataweza kwenda kujadiliana mambo kwenye mikutano ya kimataifa?

Ataweza kumpinga rais wa Marekani kama Nyerere alivyompinga Ronald Reagan Cancun Mexico mwaka 1981 (soma hapa)

Hebu soma, New York Times wameaandika kistaarabu sana Nyerer alivyomjibu Reagan, lakini ilibidi Reagan apate msaada wa Margareth Thatcher, huku Nyerere akiwa upande mmoja na Prime Minister Trudeau wa Canada, baba yake na Prime Minister wa sasa, Justin Trudeau.

Rais Samia Suluhu Hassan, akishindwa kujibu maswali yanayoitwa "softball" ya waandishi habari wa tanzania, ataweza kumpandishia Waziri Mkuu wa Uingereza kama rais Benjamin William Mkapa alivyompandishia Tony Blair kuhusu Zimbabwe at the Commonwealth Heads of Government Meeting Australia in 2001, mpaka Blair akamuweka Mkapa kwenye tume zake huko ili kumfanya awe rafiki yake wa karibu? (soma hapa)

Kama Rais Samia Suluhu Hassan anashindwa kujibu maswali ya waandishi rafiki wa habari wa Tanzania, ataweza kwenda kwenye show ya kibabe ya HardTalk naStephen Sackur kujibu maswali ya "kumkoma nyani giladi"?

Anataka kufyungua nchi, ku deal na international media, kwa style hii ya ku quote article ya fake news kuhusu Coronavirus?
Jamaa una "Reasoning" ya hatari sana cief
 
Kama ni hivyo, huo ni udhaifu mkubwa tu.

Alitakiwa kujiandaa, alitakiwa kufanya mock interview na watu wa Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu. Yani angekaa Ikulu na ile team yake, halafu ile team yake inajifanya kama waandishi wa habari, wanampiga maswali yote vigongo. Anawajibu, wanamnoa, akikosea wanamrekebisha, wanamnoa, mpaka anakuwa kaweza vizuri.

Hawa viongozi wa nchi zilizoendelea kina Obama mara nyingine wanaonekana wana akili saaana, kumbe ni suala la kujiandaa vizuri tu na timu zao, kufanya hizi mock interviews, halafu wanarudia majibu waliyokariri.Wanaonekana kama wamesema palepale, ma genius.Kumbe walishajiandaa kitambo tu.

Kuna muandishi mmoja wa John Fitzgerald Kennedy, rais wa zamani wa Marekani, huyo jamaa alikuwa anaitwa Ted Sorensen. Ted Sorensen alikuwa anafanya hizi mock interviews na Kennedy, anajua positions za Kennedy, anajua majibu ya Kennedy, mpaka watu wakasema Sorensen ni kama ubongo wa pili wa Kennedy, unaweza kupata jibu la Kennedy kwa kumuuliza swali Sorensen.

Watu wanafanya kazi kitaasisi zaidi, kwa kuangalia sheria na policy zaidi, si kwa rais kujibu kitu kutoka kichwani hapo hapo tu.

Angefanya mock interview.Halafu baadaye akija kuwa na waandishi wa habari wa kweli, maswali mengi huwa yanajirudia yale yale muhimu, kwa hivyo, na yeye kama kajiandaa vizuri, anakuwa anarudia tu majibu ambayo kashayafanyia mazoezi.

Kwa mtindo huu, rais anakuwa hatoi kitu kichwani hapo hapo anapoulizwa swali, majibu yake yanakuwa yamepitiwa kitaasisi na Ikulu.

Hiki ni kitu muhimu sana, hususan kwa rais mpya ambaye hajazoea urais bado.

Sasa, inaonekana hajajiandaa. Na inawezekana ikawa si vibaya sana, wanasema kosa moja haliachishi mke. Lakini, hofu yangu ni kwamba kuna utamaduni wa kutojiandaa.

Amesema mwenyewe kwamba hakujiandaa kuwa rais, alijiandaa kuwa makamu wa rais.

Hili jambo linaonesha huyu hata kazi ya umakamu wa rais haielewi.

Ukisema hujajiandaa kuwa rais, umejiandaa kuwa makamu wa rais, kimsingi, maana yake ni kwamba, hata huo umakamu wa rais hujajiandaa nao.

Kwa sababu, makamu wa rais ni mtu anayeweza kuwa rais wakati wowote.Ndiyo maana tukaweka kipengele cha kusema, makamu wa rais ni mgombea mwenza wa rais.Tunapomchagua rais hatumchagui mtu mmoja, tunamchagua rais na mgombea mwenza. Rais akipata matatizo asiweze kuongoza nchi, akiumwa au akifariki, makamu wa rais anachukua nchi mara moja.

Sasa ile habari ya kwamba hajajiandaa kuwa rais inaonesha nini? Hakujua kwamba makamu wa rais anaweza kuwa rais siku yoyote? Au ndiyo fake modesty tu ambayo inakuwa inaonesha lack of depth?

Kama mtu anashindwa kujiandaa kujibu vizuri maswali mepesi ya waandishi wa habari wa Tanzania wenye heshima kubwa na woga mwingi, ataweza kwenda kujadiliana mambo kwenye mikutano ya kimataifa?

Ataweza kumpinga rais wa Marekani kama Nyerere alivyompinga Ronald Reagan Cancun Mexico mwaka 1981? (soma hapa)

Hebu soma, New York Times wameaandika kistaarabu sana Nyerere alivyomjibu Reagan, lakini ilibidi Reagan apate msaada wa Margareth Thatcher, huku Nyerere akiwa upande mmoja na Prime Minister Trudeau wa Canada, baba yake na Prime Minister wa sasa, Justin Trudeau.

Rais Samia Suluhu Hassan, akishindwa kujibu maswali yanayoitwa "softball" ya waandishi habari wa Tanzania, ataweza kumpandishia Waziri Mkuu wa Uingereza kama rais Benjamin William Mkapa alivyompandishia Tony Blair kuhusu Zimbabwe at the Commonwealth Heads of Government Meeting Australia in 2001, mpaka Blair akamuweka Mkapa kwenye tume zake huko ili kumfanya awe rafiki yake wa karibu? (soma hapa)

Kama Rais Samia Suluhu Hassan anashindwa kujibu maswali ya waandishi rafiki wa habari wa Tanzania, ataweza kwenda kwenye show ya kibabe ya HardTalk na Stephen Sackur kujibu maswali ya "kumkoma nyani giladi"?

Anataka kufyungua nchi, ku deal na international media, kwa style hii ya ku quote article ya fake news kuhusu Coronavirus?
Tz ilikuwa na sifa ya kuandaa viongozi wake, na wa nchi jirani. Sijui nini kilitokea : Mwendazake hakujiandaa (akimaanisha kuwa hakuandaliwa), mama naye nasikia mapichapicha. Something fishy!!!
Itakuja tokea kweli kuwa na kiongozi akipanda mimbari ya UN/Common Weakth/AU anatoa speech inayokata usingizi na uchovu.
 
Mkuu nasisitiza tulie nae sio halisi ni SHADOW.

Ukitaka kujua mwenyewe halisi leo 29/6/2021 amekabidhiwa MPANGO WA TATU WA MAENDELEO WA TAIFA na waziri mkuu.
 
Nakusoma mkuu wangu 'misasa'.

Sasa sijui itakuwaje; maana yaliyomwagika yamemwagika!
Mkuu tusisubirie yamwagike zaidi maana itakuwa majuto ni mjukuu.

Huyu atakuwa KIVULI tunatakiwa tuingie kiundani tumjue halisi ni nani? Inawezekana tunampa lawama sio zake kumbe kuna watu wamerudi kwa mlango wa nyuma.
 
Katiba inayotafutwa lazima iseme Tena kwa herufi kubwa "NI MARUFUKU KWA MTU KUSUKUMIZWA URAIS"
Hahaha

Na akisukumizwa je? Nashauri hicho kipengele kiwe kwenye ukurasa wa kwanza mkuu.😂😂😂😂
 
Kwenye kuteua, alimteua mpaka ndugu yake kiundugunization, bila aibu.

Kuna tatizo kubwa pale nchi ambapo kwenye makaratasi inakwenda kwa misingi ya utawala wa sheria, lakini kiuhalisi zile sheria zote za kwenye makaratasi zimewekewa figisu kubwa sana, nchi inakwenda kwa mazoea tu.

Huyu kashakaa sana chemba na dikteta uchwara, unafikiri siku zote walikuwa wanaongea nini kama si kurithishana udikteta tu?
Unataka kuniambia kuna gang jingine linakuja? Kazi kweli kweli.
 
Tz ilikuwa na sifa ya kuandaa viongozi wake, na wa nchi jirani. Sijui nini kilitokea : Mwendazake hakujiandaa (akimaanisha kuwa hakuandaliwa), mama naye nasikia mapichapicha. Something fishy!!!
Itakuja tokea kweli kuwa na kiongozi akipanda mimbari ya UN/Common Weakth/AU anatoa speech inayokata usingizi na uchovu.
Kwenye msiba wa Reginald Mengi, Dr. Bashiru alisema neno zito sana alipomuombea msamaha Paul Makonda, baada ya Paul Makonda kuharibu speech ndogo tu ya eulogy msibani.

Alisema CCM hapa katikati imeacha kuandaa vijana. Alisema kisiasa, lakini ile kauli imehusu zaidi ya vijana. CCM imepoteza dira na muelekeo siku nyingi kama alivyosema Dr. Horace Kolimba

In fact hata kitabu cha Nyerere alichomuandikia Mwinyi kuhusu kuvunja katiba kilionesha Mwinyi alipewa nafasi kugomnea urais kabla ya kuandaliwa vizuri.
 
Watanzania ujuaji mwingi. Kila mtu anasema lake. Kiongozi mzuri lazima uzibe masikio. Ni bora ukosee kwa kuamua kwa utashi wako, kuliko kelele za mitandaoni. Tuko hovyo sana, kila mtu anajifanya anajua. Wazee wa miruzi mingi!
 
Back
Top Bottom