Kama ni hivyo, huo ni udhaifu mkubwa tu.
Alitakiwa kujiandaa, alitakiwa kufanya mock interview na watu wa Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu. Yani angekaa Ikulu na ile team yake, halafu ile team yake inajifanya kama waandishi wa habari, wanampiga maswali yote vigongo. Anawajibu, wanamnoa, akikosea wanamrekebisha, wanamnoa, mpaka anakuwa kaweza vizuri.
Hawa viongozi wa nchi zilizoendelea kina Obama mara nyingine wanaonekana wana akili saaana, kumbe ni suala la kujiandaa vizuri tu na timu zao, kufanya hizi mock interviews, halafu wanarudia majibu waliyokariri.Wanaonekana kama wamesema palepale, ma genius.Kumbe walishajiandaa kitambo tu.
Kuna muandishi mmoja wa John Fitzgerald Kennedy, rais wa zamani wa Marekani, huyo jamaa alikuwa anaitwa Ted Sorensen. Ted Sorensen alikuwa anafanya hizi mock interviews na Kennedy, anajua positions za Kennedy, anajua majibu ya Kennedy, mpaka watu wakasema Sorensen ni kama ubongo wa pili wa Kennedy, unaweza kupata jibu la Kennedy kwa kumuuliza swali Sorensen.
Watu wanafanya kazi kitaasisi zaidi, kwa kuangalia sheria na policy zaidi, si kwa rais kujibu kitu kutoka kichwani hapo hapo tu.
Angefanya mock interview.Halafu baadaye akija kuwa na waandishi wa habari wa kweli, maswali mengi huwa yanajirudia yale yale muhimu, kwa hivyo, na yeye kama kajiandaa vizuri, anakuwa anarudia tu majibu ambayo kashayafanyia mazoezi.
Kwa mtindo huu, rais anakuwa hatoi kitu kichwani hapo hapo anapoulizwa swali, majibu yake yanakuwa yamepitiwa kitaasisi na Ikulu.
Hiki ni kitu muhimu sana, hususan kwa rais mpya ambaye hajazoea urais bado.
Sasa, inaonekana hajajiandaa. Na inawezekana ikawa si vibaya sana, wanasema kosa moja haliachishi mke. Lakini, hofu yangu ni kwamba kuna utamaduni wa kutojiandaa.
Amesema mwenyewe kwamba hakujiandaa kuwa rais, alijiandaa kuwa makamu wa rais.
Hili jambo linaonesha huyu hata kazi ya umakamu wa rais haielewi.
Ukisema hujajiandaa kuwa rais, umejiandaa kuwa makamu wa rais, kimsingi, maana yake ni kwamba, hata huo umakamu wa rais hujajiandaa nao.
Kwa sababu, makamu wa rais ni mtu anayeweza kuwa rais wakati wowote.Ndiyo maana tukaweka kipengele cha kusema, makamu wa rais ni mgombea mwenza wa rais.Tunapomchagua rais hatumchagui mtu mmoja, tunamchagua rais na mgombea mwenza. Rais akipata matatizo asiweze kuongoza nchi, akiumwa au akifariki, makamu wa rais anachukua nchi mara moja.
Sasa ile habari ya kwamba hajajiandaa kuwa rais inaonesha nini? Hakujua kwamba makamu wa rais anaweza kuwa rais siku yoyote? Au ndiyo fake modesty tu ambayo inakuwa inaonesha lack of depth?
Kama mtu anashindwa kujiandaa kujibu vizuri maswali mepesi ya waandishi wa habari wa Tanzania wenye heshima kubwa na woga mwingi, ataweza kwenda kujadiliana mambo kwenye mikutano ya kimataifa?
Ataweza kumpinga rais wa Marekani kama Nyerere alivyompinga Ronald Reagan Cancun Mexico mwaka 1981? (
soma hapa)
Hebu soma, New York Times wameaandika kistaarabu sana Nyerere alivyomjibu Reagan, lakini ilibidi Reagan apate msaada wa Margareth Thatcher, huku Nyerere akiwa upande mmoja na Prime Minister Trudeau wa Canada, baba yake na Prime Minister wa sasa, Justin Trudeau.
Rais Samia Suluhu Hassan, akishindwa kujibu maswali yanayoitwa "softball" ya waandishi habari wa Tanzania, ataweza kumpandishia Waziri Mkuu wa Uingereza kama rais Benjamin William Mkapa alivyompandishia Tony Blair kuhusu Zimbabwe at the Commonwealth Heads of Government Meeting Australia in 2001, mpaka Blair akamuweka Mkapa kwenye tume zake huko ili kumfanya awe rafiki yake wa karibu? (
soma hapa)
Kama Rais Samia Suluhu Hassan anashindwa kujibu maswali ya waandishi rafiki wa habari wa Tanzania, ataweza kwenda kwenye show ya kibabe ya HardTalk na Stephen Sackur kujibu maswali ya "kumkoma nyani giladi"?
Anataka kufyungua nchi, ku deal na international media, kwa style hii ya ku quote article ya fake news kuhusu Coronavirus?