Wote wameingia kibahati na kutotarajia, Rais Samia hana jipya tena

Wote wameingia kibahati na kutotarajia, Rais Samia hana jipya tena

tatizo ni UNAFIKI na kutaka kuonekana mwema kuliko mtangulizi wake.

Muda utaongea ATADHALILIKA TU.
 
Mkuu tusisubirie yamwagike zaidi maana itakuwa majuto ni mjukuu.

Huyu atakuwa KIVULI tunatakiwa tuingie kiundani tumjue halisi ni nani? Inawezekana tunampa lawama sio zake kumbe kuna watu wamerudi kwa mlango wa nyuma.
Nilijua wewe siyo mtu mwepesimwepesi kama hawa wengine tunaowaona humu JF kila siku wakipayuka bila kujua kitu wanachoshabikia.
 
Ni akili ndogo saaana kuona kila hoja pingamizi inatoka CHADEMA, hapa tunajadili national agenda sio vikundi kama CCM na CHADEMA
Mzee wa chibuku huko vema kwa kutema madini na kushusha nondo
 
Hayati Magufuli a.k.a mwendazake aliwahi kukiri kuwa hakutarajia kuwa Rais wa awamu ya tano. Wengi tunakumbuka yaliyotokea, mpambano wa Membe na Lowassa ndio uliomzaa Magufuli kama suluhu ya kambi mbili pinzani ndani ya CCM wakati huo.

Mwendazake alipata heshima na makofi mengi ndani ya siku 100 kwa kauli mbiu ya kutumbua majipu, akapata na sifa nyingi bandia. Akageuza sifa, mapambio na heshima aliyopata kuwa sera ya nyongeza. Hakutaka tena kitu chochote mbadala,akalewa sifa na kuona hakuna Rais kama yeye wote waliomtangulia akawaona kama wezi na wanyang'anyi!

Kwa kawaida ya kimaumbile ya IQ ndogo, mwanadamu wa IQ ndogo anapofikia hatua aliyofikia mwendazake ya kulewa sifa huwa hataki kushuka wala kukosolewa. Matokeo ni kwamba kila anaekosoa anashughulikiwa, amri na ubabe utawala, sheria nazo uonekana ni adui mwingine ivyo mtoto anaezaliwa ni uundaji wa vikundi vya kiharifu vinavyolindwa na serikali kushughulika na wapinzani ili kulinda heshima ya Rais na sio katiba aliyoapia kuilinda. Baadae anazaliwa mtoto wa pili yaani udikteta!

Nimemsikia jana Rais Samia anaelekea kwa kasi kuumba kile kile cha mwendazake. Sasa anaona heshima yake ni bora kuliko katiba na matakwa ya wananchi. Kauli yake kuwa suala la katiba kusubiri uchumi ukue, utajiuliza je unaweza kupata maendeleo bila katiba yenye kukubaliwa na wengi? Kwa nini watu wasiwe huru kufanya mikutano kama katiba ya sasa inavyosema? Je kauli ya Rais kuweka masharti ya uhuru wa mikutano umezingtia sheria ipi inayozidi katiba au ni kauli binafsi tu kama ya mwendazake? Ni wazi ameanza kupingwa sana.

Sasa ni dhahiri mama kalewa sifa. Atapingwa. Ataanza kulinda sifa hizo na heshima aliyopewa kwa gharama, ivyo ataunda vikundi haramu kushughulika na wanaompinga, akina Sabaya wapya tuwatarajie!

USHAURI: Rais Samia aondokane na chawa wa mwendazake, achague upande wa wananchi na sio kikundi cha wachache wenye kulenga maslahi binafsi, atapata heshima ya kweli na ya kudumu badala ya hii heshima ya bandia na ya muda mfupi.
Kama taifa bado tunasafari ndefu, ila yanamwisho ,
 
Kwa dalili ambazo anaonesha ni wazi kwamba alikuwa VP jina haja majukumu yake kikatiba alikuwa hajui huwezi kuwa VP alafu ukawa rais ukasema hukutajia hili Ni tatizo

Ninaweza ungana na kauli ya Dr.Ali Bashiru Kuna tatizo katika kuandaa viongozi.
Tatizo linakuja pale viongozi wanapopatikana kwa kuangalia uwezo wa kujipendekeza kuliko uwezo wa kazi.
 
Nilijua wewe siyo mtu mwepesimwepesi kama hawa wengine tunaowaona humu JF kila siku wakipayuka bila kujua kitu wanachoshabikia.
Uwa naangalia na kutafakari huku nikiwa natafiti hapa na pale.

Nina uhakika kwa asilimia kadhaa huyu tuliona nae amekuwa KIVULI sio halisi.

Au mkuu ujachungulia hilo?
 
Uwa naangalia na kutafakari huku nikiwa natafiti hapa na pale.

Nina uhakika kwa asilimia kadhaa huyu tuliona nae amekuwa KIVULI sio halisi.

Au mkuu ujachungulia hilo?
Nililiona mapema sana baada ya kuimbishwa nyimbo kwenye safari yake ya Nairobi na kutangaza "Nakwenda Kufungua Nchi."

Siku hiyo hiyo mashaka yangu yote kuhusu uongozi wake yaliondoka. Na baada ya hapo, kila siku inayopita inazidi kuonyesha kwamba huenda yeye akamzidi huyo anayemchezesha ngoma ambaye ndiye tunayemlaumu zaidi kwa sasa.
 
Acheni kupotosha. Hakuna demokrasia isiyokuwa na mipaka. Yes Katiba ina provide demokrasi ya vyama vingi ila kwa mipaka. Hata huko America kwa Adam Smith hili liko wazi. Rais ni Joe Biden. Fanyeni siasa za kimkakati.

Yaani turuhusu tu mtu siku kaamka aandamane au afanye mikutano kukata stress zake, no way! Magufuli was right and our dear President Samia yuko sahihi pia.
Mkuu mbona unaongea huku umeshika remote ya shemeji yako sebuleni? Hivi unaju katiba wewe. Au unasubiri shemeji yako azime taa ukapige chabo[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mmeshindwa kuingia Ikulu mmekalia ramli tu. Upinzani ulishajifia kitambo zimebaki kelele tu, ni CCM tu mpaka 2050.
 
Nakusoma mkuu wangu 'misasa'.

Sasa sijui itakuwaje; maana yaliyomwagika yamemwagika!
Inabidi tubanane kwenda mbele kesho yasimwagike tena.

Yani ile one mistake one goal mpaka kila mtu anatia akili.

Ile sifa ya rais kusema "Watanzania ni watu warahimu sana" inaonekana nzuri, lakini si sifa nzuri.

Maana yake rais kashajijengea taswira kwamba Watanzania watu poa fulani hivi, wana mercy sana, hata ukiwakosea si watu wa ku mind.

Kwa mtaji huo, atafanya lolote, hatachukulia katiba seriously, kama anataka kupiga atapiga. Ndiyo hivyo unsona mfano kashaweka ndugu yake kwenye baraza.

Si Watanzania watu poa tu, watafanyaje?

Hawafanyi kitu.

Rais kashawachukulia poa tu.
 
Mmeshindwa kuingia Ikulu mmekalia ramli tu. Upinzani ulishajifia kitambo zimebaki kelele tu, ni CCM tu mpaka 2050.
Ndio maana tunadai katiba mpya...na itapatikana tu,enough is enough
 
Inabidi tubanane kwenda mbele kesho yasimwagike tena.

Yani ile one mistake one goal mpaka kila mtu anatia akili.

Ile sifa ya rais kusema "Watanzania ni watu warahimu sana" inaonekana nzuri, lakini si sifa nzuri.

Maana yake rais kashajijengea taswira kwamba Watanzania watu poa fulani hivi, wana mercy sana, hata ukiwakosea si watu wa ku mind.

Kwa mtaji huo, atafanya lolote, hatachukulia katiba seriously, kama anataka kupiga atapiga. Ndiyo hivyo unsona mfano kashaweka ndugu yake kwenye baraza.

Si Watanzania watu poa tu, watafanyaje?

Hawafanyi kitu.

Rais kashawachukulia poa tu.
Siku hizi inaniwia vigumu kutenganisha kati ya "waTanzania kuwa watu poa sana", na "waTanzania kuwa watu wajinga sana".

Nikitakiwa kueleza, huenda nitaandika kitabu kizima.
 
Back
Top Bottom