Wote wameingia kibahati na kutotarajia, Rais Samia hana jipya tena

Wote wameingia kibahati na kutotarajia, Rais Samia hana jipya tena

Kufungua nchi, kukuza uchumi vinakwenda sambamba na utawala wa sheria.

Mikutano ya kisiasa haikuzuii Rais kutitimiza wajibu wako

Ruhusu watu wafanye siasa, Katiba ya sasa inaruhusu, sheria pia inaruhusu sasa katazo hili unataka kuririthi? CCM yako isiogope ushindani wa kisiasa watakuvurugia kabisa hizi sifa za siku 100 zako za kwanza.
 
Kwenye kuteua, alimteua mpaka ndugu yake kiundugunization, bila aibu.

Kuna tatizo kubwa pale nchi ambapo kwenye makaratasi inakwenda kwa misingi ya utawala wa sheria, lakini kiuhalisi zile sheria zote za kwenye makaratasi zimewekewa figisu kubwa sana, nchi inakwenda kwa mazoea tu.

Huyu kashakaa sana chemba na dikteta uchwara, unafikiri siku zote walikuwa wanaongea nini kama si kurithishana udikteta tu?
Dawa ipo tarehe 1 kwenye katiba day, makombora tutayorusha nadhani atakuwa dikteta rasmi na sio sasa hivi anafanya kwa kujifichaficha
 
Ndiyo ameanza rasmi safari ya udikteta
Kama una muda tunaomba tarehe 1 alhamisi ya keshokutwa uje tabata, tunahitaji sana michango na mawazo yenu. Muda ni sasa, huyu tukitumia nguvu kidogo tu katiba inapatikana asubuhi saa 4
 
Acheni kupotosha. Hakuna demokrasia isiyokuwa na mipaka. Yes Katiba ina provide demokrasi ya vyama vingi ila kwa mipaka. Hata huko America kwa Adam Smith hili liko wazi. Rais ni Joe Biden. Fanyeni siasa za kimkakati.

Yaani turuhusu tu mtu siku kaamka aandamane au afanye mikutano kukata stress zake, no way! Magufuli was right and our dear President Samia yuko sahihi pia.
 
Hakujiandaa kua raisi, bado anajipanga. Sasa hivi bado anafata ushauri wa wataalamu wake kwa kila jambo.
 
Kufungua nchi, kukuza uchumi vinakwenda sambamba na utawala wa sheria.

Mikutano ya kisiasa haikuzuii Rais kutitimiza wajibu wako

Ruhusu watu wafanye siasa, Katiba ya sasa inaruhusu, sheria pia inaruhusu sasa katazo hili unataka kuririthi? CCM yako isiogope ushindani wa kisiasa watakuvurugia kabisa hizi sifa za siku 100 zako za kwanza.
Yaani leo Mpinzani Kama Mzee wa wali akitaka kufanya mkutano Chato anazuia maendeleo [emoji1787][emoji1787]
 
Hivi dikteta uchwara kwa kiingereza Ni lame dictator eeeh!!!?

Au Lina kuaje?

I see another dikteta in the making
 
Kwenye kuteua, alimteua mpaka ndugu yake kiundugunization, bila aibu.

Kuna tatizo kubwa pale nchi ambapo kwenye makaratasi inakwenda kwa misingi ya utawala wa sheria, lakini kiuhalisi zile sheria zote za kwenye makaratasi zimewekewa figisu kubwa sana, nchi inakwenda kwa mazoea tu.

Huyu kashakaa sana chemba na dikteta uchwara, unafikiri siku zote walikuwa wanaongea nini kama si kurithishana udikteta tu?
Binafsi nahisi Mama hakutarajia Kama kwenye ule mkutano atakutana na swali la namna ile ndio maana kujibu kwake Mpaka sasa kumeacha ukakasi mwingi Sana juu ya msimamo wake katika suala la demokrasia nchini au alikuwa na dhamira hiyo ila muda ulikuwa bado kuonesha makucha yake ila ghafla akakutana na suala hilo hivyo kuonesha ngozi yake ya asili ya nini anawaza.
 
Acheni kupotosha. Hakuna demokrasia isiyokuwa na mipaka. Yes Katiba ina provide demokrasi ya vyama vingi ila kwa mipaka. Hata huko America kwa Adam Smith hili liko wazi. Rais ni Joe Biden. Fanyeni siasa za kimkakati.

Yaani turuhusu tu mtu siku kaamka aandamane au afanye mikutano kukata stress zake, no way! Magufuli was right and our dear President Samia yuko sahihi pia.
Labda kama haujasoma katiba,katiba inatambua HRs ivyo uhuru wa kukusanyika,kuongea na kuandamana ni haki za msingi na hakuna mipaka hapo.
Mipaka muwekee mkeo au mumeo
 
Acheni kupotosha. Hakuna demokrasia isiyokuwa na mipaka.
CCM hapa ndipo mkiwa kwenye vikao vyenu huwa mnajidanganyaga...acheni uwoga kama mnapedwa kweli hofu ya nini? Mtaomba poo kwa marais wawasaidie mpaka lini? Yaani ni sawa na toto la miaka 45 linasubiri msosi kwa baba na mama.

Msimrisishe Mama Samia udikteta wa jamaa..mtamchafua mapemaaa!!
 
Binafsi nahisi Mama hakutarajia Kama kwenye ule mkutano atakutana na swali la namna ile ndio maana kujibu kwake Mpaka sasa kumeacha ukakasi mwingi Sana juu ya msimamo wake katika suala la demokrasia nchini au alikuwa na dhamira hiyo ila muda ulikuwa bado kuonesha makucha yake ila ghafla akakutana na suala hilo hivyo kuonesha ngozi yake ya asili ya nini anawaza.
Kama ni hivyo, huo ni udhaifu mkubwa tu.

Alitakiwa kujiandaa, alitakiwa kufanya mock interview na watu wa Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu. Yani angekaa Ikulu na ile team yake, halafu ile team yake inajifanya kama waandishi wa habari, wanampiga maswali yote vigongo. Anawajibu, wanamnoa, akikosea wanamrekebisha, wanamnoa, mpaka anakuwa kaweza vizuri.

Hawa viongozi wa nchi zilizoendelea kina Obama mara nyingine wanaonekana wana akili saaana, kumbe ni suala la kujiandaa vizuri tu na timu zao, kufanya hizi mock interviews, halafu wanarudia majibu waliyokariri.Wanaonekana kama wamesema palepale, ma genius.Kumbe walishajiandaa kitambo tu.

Kuna muandishi mmoja wa John Fitzgerald Kennedy, rais wa zamani wa Marekani, huyo jamaa alikuwa anaitwa Ted Sorensen. Ted Sorensen alikuwa anafanya hizi mock interviews na Kennedy, anajua positions za Kennedy, anajua majibu ya Kennedy, mpaka watu wakasema Sorensen ni kama ubongo wa pili wa Kennedy, unaweza kupata jibu la Kennedy kwa kumuuliza swali Sorensen.

Watu wanafanya kazi kitaasisi zaidi, kwa kuangalia sheria na policy zaidi, si kwa rais kujibu kitu kutoka kichwani hapo hapo tu.

Angefanya mock interview.Halafu baadaye akija kuwa na waandishi wa habari wa kweli, maswali mengi huwa yanajirudia yale yale muhimu, kwa hivyo, na yeye kama kajiandaa vizuri, anakuwa anarudia tu majibu ambayo kashayafanyia mazoezi.

Kwa mtindo huu, rais anakuwa hatoi kitu kichwani hapo hapo anapoulizwa swali, majibu yake yanakuwa yamepitiwa kitaasisi na Ikulu.

Hiki ni kitu muhimu sana, hususan kwa rais mpya ambaye hajazoea urais bado.

Sasa, inaonekana hajajiandaa. Na inawezekana ikawa si vibaya sana, wanasema kosa moja haliachishi mke. Lakini, hofu yangu ni kwamba kuna utamaduni wa kutojiandaa.

Amesema mwenyewe kwamba hakujiandaa kuwa rais, alijiandaa kuwa makamu wa rais.

Hili jambo linaonesha huyu hata kazi ya umakamu wa rais haielewi.

Ukisema hujajiandaa kuwa rais, umejiandaa kuwa makamu wa rais, kimsingi, maana yake ni kwamba, hata huo umakamu wa rais hujajiandaa nao.

Kwa sababu, makamu wa rais ni mtu anayeweza kuwa rais wakati wowote.Ndiyo maana tukaweka kipengele cha kusema, makamu wa rais ni mgombea mwenza wa rais.Tunapomchagua rais hatumchagui mtu mmoja, tunamchagua rais na mgombea mwenza. Rais akipata matatizo asiweze kuongoza nchi, akiumwa au akifariki, makamu wa rais anachukua nchi mara moja.

Sasa ile habari ya kwamba hajajiandaa kuwa rais inaonesha nini? Hakujua kwamba makamu wa rais anaweza kuwa rais siku yoyote? Au ndiyo fake modesty tu ambayo inakuwa inaonesha lack of depth?

Kama mtu anashindwa kujiandaa kujibu vizuri maswali mepesi ya waandishi wa habari wa Tanzania wenye heshima kubwa na woga mwingi, ataweza kwenda kujadiliana mambo kwenye mikutano ya kimataifa?

Ataweza kumpinga rais wa Marekani kama Nyerere alivyompinga Ronald Reagan Cancun Mexico mwaka 1981? (soma hapa)

Hebu soma, New York Times wameaandika kistaarabu sana Nyerere alivyomjibu Reagan, lakini ilibidi Reagan apate msaada wa Margareth Thatcher, huku Nyerere akiwa upande mmoja na Prime Minister Trudeau wa Canada, baba yake na Prime Minister wa sasa, Justin Trudeau.

Rais Samia Suluhu Hassan, akishindwa kujibu maswali yanayoitwa "softball" ya waandishi habari wa Tanzania, ataweza kumpandishia Waziri Mkuu wa Uingereza kama rais Benjamin William Mkapa alivyompandishia Tony Blair kuhusu Zimbabwe at the Commonwealth Heads of Government Meeting Australia in 2001, mpaka Blair akamuweka Mkapa kwenye tume zake huko ili kumfanya awe rafiki yake wa karibu? (soma hapa)

Kama Rais Samia Suluhu Hassan anashindwa kujibu maswali ya waandishi rafiki wa habari wa Tanzania, ataweza kwenda kwenye show ya kibabe ya HardTalk na Stephen Sackur kujibu maswali ya "kumkoma nyani giladi"?

Anataka kufungua nchi, ku deal na international media, kwa style hii ya ku quote article ya fake news kuhusu Coronavirus?
 
Dawa ipo tarehe 1 kwenye katiba day, makombora tutayorusha nadhani atakuwa dikteta rasmi na sio sasa hivi anafanya kwa kujifichaficha
Duh,

Mkuu naona unataka awe dikteta rasmi kama ubaya ubaya tu upate kumpiga full blast bila kuremba, au siyo?
 
Aina ya viongozi tulionao ndio aina ya watu na wananchi tulivyo. Tujenge nchi ndivyo tulivyo
 
Ni akili ndogo kuona kila hoja pingamizi inatoka CHADEMA, hapa tunajadili national agenda sio vikundi kama CCM na CHADEMA
ni chadema wacha kukimbia kivuli wewe mjusi.

mbona nyinyi kila aliyempinga mtu kabla mlimwita mataga??
 
Hili sio swala LA chadema wala CCM mambo yanayoendelea hapa Tanzania ni ya hovyo.
hii ndio ccm tunayoijua,hakuna mtu alikuwa anaibadili nchi na ccm yenyewe kama magufuli.mkamdhihaki,mkamzomea na mbaya zaidi mkamshtaki kwa muumba,Mungu alivyo msikivu na kujua amaetupa mtu ambaye tunaona hatuna kazi naye akamchukua.

mara paap,kilio ghafla.
subirini na la bagamoyo port mtamwelewa magufuli,labda miaka kadhaa ijayo,ila lazima mumwelewe.
 
Back
Top Bottom