WW1, WW2 na kinachoendelea sasa Middle east vilipangwa mwaka 1871 kama barua hii ni kweli

Wanasema ili dunia iwe salama kwako ni lazima uwe na vitu viwili ELIMU na PESA na ukikosa pesa jitahidi uwe na ELIMU. Kama hauna hivyo vitu kamwe dunia haiwezi kuwa salama kwako

Mwisho wa kunukuu...
 
Kuna sehemu nilikuwa nasoma ilikuwa inaelezea juu ya bob marley alikuwa akijinasibu kuwa yeye ni muisrael kutokana na haya mataifa kumi na mbili
 
Duh!.....
 
Eiyer fafanua upapa wa Vatican na lengo lao kutawala dunia
Upapa ni kijisehemu kidogo ambacho ni sehemu ya mpango mkubwa kabisa wa kuutawala ulimwengu chini ya dini moja na mungu mmoja.Dhana ya Mungu mmoja haipo kwenye "Abrahamic religion" pekee bali ipo hata kwa Shetani maana yeye anataka awe ndiyo mungu wa dunia hii na yeye pekee tu....

Mpango wa kuitawala dunia na vilivyomo ulianza ramsi huko mbinguni miaka maelfu mengi yaliyopita pale malaika mmoja mzurisana alipoanzisha harakati za "kumpindua Mungu".Malaika huyu hakupendezwa na mambo mengi ikiwemo namna Mungu alivyokuwa akiendesha mambo yake hivyo akaanzisha "movement" huko mbinguni ya kufanya mapinduzi lakini bahati mbaya alishindwa kabisa baada ya Jemedari mkuu wa majeshi ya Mbinguni,Mikael kumsambaratisha malaika huyo pamoja na jeshi lake...

Malaika huyo wakati wa harakati zake alikuwa akiwashawishi malaika wengine waungane naye na alifanikiwa kuwashawishi robo ya malaika walioko mbinguni na hapo alipoona ameweza kuwashawishi hao aliamua "kulianzisha" lakini alishindwa...

Baada ya kushindwa alitupwa huku duniani lakini aliazimu kuendeleza harakati zake kama za mbinguni za kuwafanya viumbe wengine wamuone Mungu hafai na ni dikteta.Miongoni mwa harakati hizi ni tukio lililobadilisha kabisa maisha na hali ya duniani tukio lililotokea miaka zaidi ya 5500 iliyopita pale Eden baada ya malaika huyo kufanikiwa kumshawishi binadamu kumuasi Mungu....

Kuanzia hapo amekuwa akiendesha harakati zake kupitia njia nyingi na miongoni mwa njia hizo ni kuanzisha utaratibu wa kufanana na ule wa Mungu wa kumuokoa mwanadamu ambao ni dini.Ameanzisha dini nyingi fake na zinazofanana kwa sehemu kubwa na njia aliyoianzisha Mungu kwaajili ya kumuokoa mwanadamu...

Pia,ameanzisha harakati kupitia siasa,elimu n.k,lengo ni kumueweka mwanadamu mbali kabisa na Mungu na miongoni mwa alivyoanzisha ni hiyo taasisi uliyoitaja lakini kuna vitengo vya kiimani kama Freemason,Illuminati,Bohemia group,Roscrucian,Theosophical sociate n.k....

Hizi ni harakati zake katika kufanikisha kazi yake ambayo nimeisema hapo juu lakini hii ni sehemu ndogo sana ya yote haya....
 
Mada nzuri sanaa lakini isiwe katika mtazamo wa kidini especially kisabato anachosema faiza foxy kina mantiki
 
Mkiweka kidini hasa kikristo wakati tuna diversity kubwa ya dini finalised kama wabudha,waislamu ,Africans, mmewafikiria pia
 
Our God is full of suprises .....ni swala la muda tu....kauli yake moja inatosha kusafisha dunia.......Lucifer/shetani ni kiumbe kilichoumbwa na Mungu ana mamlaka ya kukidhibiti kadri atakavyo.......ukiangalia kwa mbali unaweza ukadhani kwa kiasi kikubwa shetani amefanikiwa kuwa na wafuasi wengi huku duniani lakini in reality shetani amepotezwa vibaya sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…