Asante sana mkuu,nilikuwa bado nafuatilia maandiko yako pamoja na majibu yako,pamoja na wale woote waliokuwa wanakubishia,mimi si mtaalamu sana wa Bibilia lakini huwa napenda kufikirisha ubongo wangu na siyo kwenda kwenda tu kama mzigo kwenye gari.
Niliwahi kuona picha flan hivi yamazishi PAPA John Paul 11,waliokuwa wamelizunguka lile jeneza walikuwa ni viongozi mashuhuri wa Dunia, Bush,Clinton na wengine wengi tu hakuna hata cardinal hata mmoja aliyekuepo karibu na hilo jeneza nilitafakari sana na picha nyingine tena nilimuona Hitler yupo na PAPA Pius wakiteta jambo,picha zote zile ukiziangalia zinakufanya utafakari zaidi maana zina maswali mengi,asante sana mkuu,mimi nafikiri kuwa huru na kudadisi mambo ni jambo jema sana wala siyo dhambi.