WWF waponda na kupinga mradi wa umeme wa Stiegler’s Gorge

Paskali umepiga lager kabla kuandika haya au? unaikana Environmental impact assessment hujui faida yake? Kuna maendeleo yoyote Nchi inaweza kuyapata bila athari za kimazingira kutokea? Taratibu ushabiki gani huu!
 
Paskali nia ya kupata nishati mW 2000 sio mbaya,kibaya ni madhara yatokanayo na kujenga bwawa hili.
Kwanini tusingefua umeme kutokana na gesi asilia?Jibu ni rahisi sana Mikataba mibovu ya waliotangulia kuwamilikisha wageni vitalo vya gesi itakuwa gharama sana.
Nashauri tufute mikataba yote mibovu ili tutumie gesi yetu kwa bei nafuu,kuliko kjiingiza na uharibifu wa mazingira kwa makusudi.Eti tunajali mikataba mibovu
 
Huu mradi ungefanyika Kenya bila Shaka ungesikia sifa toka upinzani.

Mradi uendelee.
 
kwa nini ushangai kila siku watu walikuwa wanalalamikia kuhusu uvaajiwa nguo zisizofaa za wanamuziki na vijana wetu hasa wasichana lakini walionekana hawana maana lakini aliposema mwenye kiti mao ndio inaonekana kama limeanza leo, apingwagwi huyo kila kitu kwake ni ndio tu,
 
Mkuu tindo nimekusikia, karibu tena
WWF waponda na kupinga mradi wa umeme wa Stiegler’s Gorge

Paskali
 
Hela za mradi tunazo au tutaenda kutembeza bakuli kwa wasiopenda huo mradi??
 
Ni kweli tunahitaji umeme kwa ajili ya kupunguza gharama za uzalishaji na kuleta ushindani wa bidhaa zetu. hata hivyo naona pia serikali yetu ina mapungufu kwa kuhamisha malengo.

TULIANZA NA UMEME WA GAS, lkn sasa naona sio kipaumbele cha serikali. Kwa kutumia gas tungeweza kulinda mazingira yetu na kutunza hicho chanzo ( stiglier gorge) kwa miaka 20 ijayo. Tunarukaruka bado. Hatuna vipaumbele kama nchi na kuwa na mwendelezo wa vipaumbele. Kila Rais anakuja anavyoona yeye, hili ni tatizo sana kufikia malengo. Kutokana na kurukaruka na kutokuwa na msimamo, ndio maana barabara ya Ubungo mpaka Kimara katika miaka 20 ( 1995-2018) imejengwa mara tatu. katika hali ya kawaida tulitegemea barabara ikijengwa ikae angalau miaka 30 bila kubadilisha ramani yake kwa kuwa makadirio ya matumizi ya barabara kila mwaka yanakuwa yamefanyika. Barabra ya Ubungo imejengwa wakati wa Mh. Mkapa ( 1997-1999), wakati wa Mh. Kikwete ( mradi wa DART kusanifiwa na kujengwa 2007-2014 ) na wakati wa Magufuli (Mradi wa ubungo flyover nadhani 2016-2019). Kutokana na kukosa mwelekeo, barabara ya Ubungo kuelekea kibaha umekuwa na sheria tofauti tofauti na umesababisha hasara kwa serikali. wananchi na mateso yasisyo ya lazima. Ni pesa nyingi zimetumika kwa sababu kukosa focus.

Binafsi, Mradi wa Stigler ulikuwa uje baada ya kumaliza miradi ya gas lkn kwa kuwa kila mtu/Kiongozi anataka aweke kumbukumbu zake, ndio hayo ya mitazamo tofauti.
Pia athari za kimazingira hatuwezi kuziona leo, lkn wengi tumeshuhudia changamoto zilizosababishwa na ubishi wa huko nyuma.
 
Wapo walioguswa zaidi na Faru John pia kuliko......
 
Mkuu Pascal Mayalla kama usingeongeza kuanzia point namba 9 na kuendelea nahakika hii ndo ingekuwa for me the best sarcastic post of 2018 (unless itokee post kama ya Edo Kumwembe kule Fb) bila kujali kuwa huu mwaka ndo kwanza umeanza maana sidhani kama ningekuja kupata post nzuri tena.
 
WWF wanaanza kwa kujigamba kwamba wao ni muhimu ktk conservation ya eneo hilo. Aliyeandika ni m-TZ maana naona makosa kibao ya lugha, au ni hiyo rapid assessment na rapid reporting? Baada ya hiyo rapid study, hebu tunawaomba wafanye study iliyo kamili sasa!

Mradi kama huu WWF wasubili kuona matokeo ya EIA na mitigation zake halafu walinganishe na study ya consultant wao.

They new it in plan since 1960s, why now come up with that rapid study?

Ripoti haielezi nini hasa kitaathilika badala yake wanakumbushia tu mambo ya heritage. Hydro ni non consumptive user wa maji. Tuna tap energy na kuyaachia maji yaende yaendako lakini bado mtu anasema kilimo downstream kitaathilika, HOW?

Huyo consultant wao anaweza kuwa alikuwa siyo mtu makini au siyo mtaalamu na aliamua kuandika wanayotaka waliompa pesa. Sehemu kubwa ya ripoti hii haina ushahidi wa kitaalamu. Sioni quantitative evidence, badala yake naona mambo ambayo ni qualitative. Unawezaje kuhusisha utalii wa chi nzima, ndege mpya na Selous? Je mbona sioni sehemu yoyote WWF akilinganisha faida za ujenzi huo vs faida za kutojenga? Hii ni report isiyo na matumizi. Wasubili EIA.

Presd. Magufuli, Tuendelee! Bhla-bhla hizo!
 

Kwa post hiyo nimekukubali kwa 100% Paskali. Hii ndio michango inayofanya nikuheshimu sana humu jukwaani.
 

Patriot naona umepinga kwa hoja, wangalau hoja zako zinakubeba. Sasa tuje kwenye kipi ni sahihi kufanyika. Unaweza ukatuambia kwanini hizo hela zisiingizwe kwenye umeme wa gas, ambao tayari ni mradi ulionza na hat uzalishaji kwa sehemu fulani. Na kwakuwa hilo bonde ni letu huko mbele ya safari uhitaji ukiwepo tukatumia pia? Kumbuka kwenye gas tutapata umeme na gas ya majumbani. Kama unaweza hebu tupe mchanganuo wa ipi ni faida sana kama tutaanza mradi mpya wa stiegler gorge, huku tukiupa msukumo mdogo mradi wa umeme wa gas ambao tayari tumeshauanza? Please fafanua hili kwani ni muhimu.
 
Tunahitaji umeme.
WWF au UN wakafuge wanyama na ecology systems pale Washington DC au Brussels.

Mbona, Trump kajiondoa kwenye mkataba wa Climate Change Summit uliofanyikia Paris!?

Waache upoyoyo.
To be open America under Trump Doesn't need Africa they are safe contained they dont need dirty Africa . Africa let us shake hands with China and Asian Countries like India etc who feel Africa is more important to them not America under Trump who feel Africans are dirty like buttocks .Let Americans stay with their cleanness so that they can't be contaminated with dirty Africans. let us join hands with dirty Chinese and Asians who don't know Americans health rules .America under Trump is so clean and disease free nation that doesnt need dirty like buttocks Africa they are a great nation and safe contained
 
Mnajidanganya nyie, wamarekani licha ya kutokuwa na wanyama wengi kama sisi lakini karibia kila jimbo wana ZOO na wanyama ni hawa hawa wetu tunaojivunia, Tembo, Twiga, Nyani, Chui, na wengine wengi. Wamewatunza vizuri na kuwazalisha, sisi tunazo mbuga za asili na wanyama wa asili sio ZOO. Hao WWF wanatusaidia sisi na wanyama wetu, ushauri wao kwetu ni wa kitaalam sisi tuna leta siasa na ujuaji.
Watalii wengi kutoka huko marekani waliisha waona Twiga, Tembo,Chui na wengine huko huko marekani, hukuk wetu, Tanzania, Kenya, Afrika kusini Namibia wakija wanataka kuwaona wanyama hao kwenye natural habitat zao, na hicho ndicho hao WWF wanakitetea, eti sisi tunawasikiliza wanasiasa wasiofahamu chochote kuhusu ecologia na maisha ya wanyama wetu lakini wanahamasisha UTALII waingize pesa.
Ohoo viwanda, hata hawafahamu wanataka viwanda gani vya kutengeneza nini, kwa teknologia ipi na ya nani kutoka wapi?!
Siasa zenu ziishie bungeni acheni wataalamu wawaambie ukweli.
 
Mkuu unajua jamaa hawa ni vigeugeu. Hydro ni renewable energy, gas siyo renewable. na mara zote wanashabikia renewable energy. Pale TANESCO upande wa solar energy wamekuwa wakipiga hela ndefu sana kwa kisingizio cha cheaper energy, ingawa mimi naelewa ni kupoteza pesa zetu na kutafuta mbinu za kuiba kupitia makandarasi binafsi.

Kama alternative ya hydro ingekuwa ni nuclear ningesema twende nuclear lakini huwezi kuacha hydro over gas. South Africa hawakuwahi kuwa na hydro. energy source yao ilikuwa nuclear na wanapanua reactor zao beyond anyone sasa hivi, lakini wamekwisha anza hydro kwenye Limpopo. Iache gesi iwepo lakini tusiache hydro. Hiyo faida ya pili ya gesi kutumika majumbani, kwa TZ bado. Hiyo ni methane ambayo ni flamable kuliko propane na butane tunazotumia kwenye mitungi. Kwa hali ya maendeleo tulipo ni hatari kuingiza methane majumbani na wataalamu wanaelewa hilo na itachukuwa miaka mingi. Nyumba zetu hizi na mazingira yake hayafai.

Angalia ripoti inavyogusagusa vipengele vingi kutaka kuhalisha maamuzi yao. Wanagusa hata Climate change bila kusema climate change inasema nini juu ya East africa. Ukisoma ripoti za IPCC utagundua jamaa hawa ni watunzi wa hadithi tu! Bahati mbaya tunao watu humu JF ambao nahisi wanajifunza kujenga hoja na ikifikia ushabiki, hoja wanaacha na kuanza CCM vs CHADEMA. Ndo maana nimewahi kuomba rais atimue mbio tu maana baadhi ya wanaoomba kusikilizwa hawana la kusikilizwa!
 
Chochote ambacho kina manufaa kwa nchi ndicho chapaswa kuwa kipaumbele. Tanzania kwanza. "World heritage" yapaswa kuja baada ya Tanzania. WWF watuache au washauri namna ya kuhifadhi wakati na baada ya uanzishwaji Wa mradi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…