WWF waponda na kupinga mradi wa umeme wa Stiegler’s Gorge

Hahaha ndugu wachina wanateknologia ya viwanda nyingi ilitoka marekani. Sisi hatuna teknologia tunaimba viwanda. Hata wakiua wanyama wote labda hatutaathirika mbona kuna nchi hazina hata zoo lakini zina maendeleo?! Mimi sikatai wasijenge, wao wajenge tu ila pia wasikilize ushauri wa kitaalam.
Hiyo strigler gorge siyo na haitakuwa solution ya umeme Tanzania, na haitaleta wala kurudisha viwanda Tanzania, wanasiasa kuimba ni kawaida na wananchi kuitikia imekua kawaida.
China siyo Tanzania na Tanzania haitakuwa china.
 
2035 nitarudi kufukua hizi Hoja zako
 
Kwanza hao WWF hawajakataza wameshauri, mkiona ushauri haufai fanyeni kama kawaida yetu, athari tutajijua huko baadaye, isitoshe mawanyama ya nini sisi tunataka umeme wa viwanda, ingawa sijui ni viwanda gani hahaha nchi hii kiboko.
 
mbona huwa wanashangilia rais anaposema unaodaiwa ni ukweli hata Kama hakuzingatia utu leo iweje wakasirikie Maneno ya Trump?
 
mbona huwa wanashangilia rais anaposema unaodaiwa ni ukweli hata Kama hakuzingatia utu leo iweje wakasirikie Maneno ya Trump?
Hahaha wadanganyika hawajiamini mpaka wapendwe na Trump. Lakini utawasikia eti tuliwafukuza wakoloni na wanasheherekea uhuru. Sasa Trump hawapendi sijui wanakosa nini?! Na huyo Trump akiwapenda sijui ndio watajiona ni binadamu?! Ninavyohisi siku Trump akisema anaipenda afrika anakuja kuitawala, miafrika italipuka kwa furaha, inapenda kupendwa na wazungu balaa hahaha
 
nimekuelewa sana boss!
 
Sina ushabiki mkuu, nionyeshe hiyo link. Over
Hakuna link hapo....watu wakurupuka tu kujadili mada pasi na kusoma kwanza rejea zilizowekwa. Hii yaonesha namna watu wengi walivyo wavivu ktk usomaji. Na muanzisha mada mwenyewe akiombwa link awa mkaliiii na akunasibisha na CCM!
 
Kwa hiyo Paskali kwako wewe mazingira si lolote si chochote, ila uchumi tu?
Hujali athari zozote za mazingira. Unadhani Tanzania inao uwezo wa kukabiliana na athari hizo?
Nchi zilizoendelea kwa sasa zinaachana na matumizi ya vyanzo vya nishati vinavuoharibu mazingira, kwa mfano nchi za Ujerumani na Ufaransa zinaachana na nuclear energy na kuingia kwenye solar.
Hata mkaa wa mawe sasa haaatumii tena.
Halafu unapongeza uvunjifu wa katiba na mikataba ya kkmataifa ya haki za binadamu? Tulisaini ya nini sasa?
Hapo ndipo ninapotilia shaka uwezo wako wa kufikiri
 
Hapo namba tatu sijakuelewa
 
Tatizo ni kwamba athari za kimazingira huwa tunazidharau sana hasa kwa nchi changa kama yetu.

Sitaki kuamini kwamba huu umeme ndio mkombozi wa viwanda ikiwa bonde la rufiji liko hayaoni kupotea. Sijui kilimo kitafanyikaje, sijui wanyama wataishi wapi huku tukiwa tunasubiria utalii.

Mabadiliko ya tabia ya nchi athari zake zipo wazi, kwan wahanga ni sisi wa nchi maskini afu Leo tinatengeneza matatizo makubwa zaidi kwa kuua mabonge yetu.
 
Yawezekana nilikuweka higher wakati ulihitaji maelezo ya chini chini. Kwa ufupi energy kwa nchi inatakiwa iwe diversified ili ujihakikishie usalama. Kwa TZ tuna gesi na hydro. Hata kama gesi inakidhi na kuzidi mahitaji yako, bado tafuta njia nyingine ili ujikinge. TZ bado tuko chini ya mahitaji yetu na siyo busara kukubaliana na WWF eti kuna njia mbadala, ipi? Gesi ipo na hata ikitosha bado tunahitaji hydro.
 
Hiyo inaeleweka Duniani, kwamba ukiwa nyuma kimaendeleo suala la mazingira huwa siyo muhimu. Ukiendelea hapo ndo madhala ya mazingira huanza kuonekana na unachukuwa hatua.

Wana JF tunapoandika taarifa za mambo muhimu kama haya na kujadiliana tuseme kwa viwango. Unaposema matatizo ya ya mabadiliko ya tabia nchi athari zake zipo wazi. athari hizo ni zipi? Angalia WWF walivyoshindwa kuonyesha uhusiano wa Madaliko ya Tabia nchi na mradi wanaoupinga. Ni bhla-bhla tu, wanataja hili na lile. Nawe unataja kwamba ziko wazi, wapi? hapa TZ? Duniani? au wapi? Zinahusu nini kwenye mradi?
 
Nadhani yabidi tuwaulize misitu yao na mbuga zao za wanyama walipeleka wapi? Wanataka Afrika iendelee kuwa 'shithole' wawe wanakuja kutuona na kutulinganisha na nyani wa msituni kwa ufukara wetu. NO! NO!
 
Mambo ya Wamarekani na zoo hayatuhusu jamani! Au unatuonyesha unaifahamu Marekani? Taarifa ya WWF ina utalaamu gani? Hakuna lolote ni Bhla-bhla tu! Athali gani waliyoionesha na hiyo itatokea kwa njia gani? Ukiwa mtaalamu, lete taarifa ya kitaalamu.
 
Tunawabishia ili hali ndio hao hao wanatuuzia na kutufundisha kutumia vifaa ili TMA watuambie kuwa kesho mvua itanyesha juu/chini ya wastani, bahari itachafuka n.k.

Wanatuambia tutaharibu ecolojia tunang'aka as if tunazo mbinu mbadala.

Hata sijui nikae upande gani, zaidi ya kungoja tu siku zangu ziishe nikaangangalie hayo makazi mapya.
 
Mwacheni dereva aendeshe gari anajua kona na mashimo ya barabara
 
Hapo namba tatu sijakuelewa
hujaelewa nini hapa?.
  1. Mradi unaelezwa unakwenda kinyume cha mikataba ya kulinda World Heritage ambayo Tanzania tumesaini, this also is nothing!,
  2. Tanzania tumesaini mikataba kibao ya kimataifa ya haki za binaadamu na kila siku serikali inakiuka mikataba hiyo,
  3. kama rais Magufuli, ameikanyaga katiba alioapa kuilinda, what are the chances kuheshimu mikataba ya kimataifa kama itatuzuia kupata manufaa,
  4. to hell with mikataba ya kimataifa at the expense of development.
P.
 
Mkuu Kidamva, umekuwa too subjective kuwa kwangu mazingira si lolote, si chochote na kuwa sijali athari zozote za mazingira!, kisha ninapongeza uvunjifu wa katiba na mikataba ya kimataifa ya haki za binaadamu...
Hapa ni suala la uelewa tuu. kitu nilichofanya nimekuwekea jinsi hoja za WWF zitakavyopanguliwa, na hoja zangu nimeziweka pande mbili, on government perspective na my take.
Ruksa kabisa kutia shaka uwezo wangu wa kufikiri, kwa watu wote ambao uwezo wao wa kuelewa unatia shaka!.

P.
 
Hahahahah nimewastukia wazungu wanataka tuendelee kuwategemea kila kitu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…