Crocodiletooth
JF-Expert Member
- Oct 28, 2012
- 20,561
- 24,428
Boss lady asikurupuke, chonde Chonde, vijana wenye papara viburi ni shida, Yapo yanayohitaji hekima, na wakati mwingine kuishi kwingi kuona mengi, kuachia ngazi kwa chongolo isichukuliwe kirahisi rahisi, kuna tatizo kubwa!Wanaotumiwa na mafisadi wamepambana sana kumshauri boss lady eti asimpe kijiti bwana mdogo na ambakishe palepale alipomteua siku chache zilizopita na huku wakimpigia debe kijana wao mwenye jina la mtoto wa Yoseph ili awe.
Hali kadhalika, wenye mlengo wa kulia wamemshauri boss lady amrejeshe mu-cubya ili kwalo aje awe boss wa Sekretalieti. Na kwa ushirikiano wa Yeye na Mwenezi, wanaamini Chama kitapaa juu mawinguni kwa kuaminiwa tena na Wananchi.
VC hamtaki yule mlima nyanya! Na akaenda mbali zaidi, eti, yupo tayari akalee wajukuu kuliko kufanya kazi na vijana wenye viburi. Mlengo wa kulia wakamuuliza, vijana ama kijana? Na kama ni vijana, je, na yupi mwingine!? Jibu lake akaishia kuguna pekee!
"....wazee wangu na wana MCC wenzangu nimewasikia. Na acheni nami na wenzangu wanaonishauri mambo ya siasa, tukalipitie." Jibu la boss lady.
Nb: Mradi wa mama bado chaji inasoma 90%.
BABU YENU, YANGU MACHO!