Ya MC Pilipili hayapaswi kufanywa na mwanaume rijali

Ya MC Pilipili hayapaswi kufanywa na mwanaume rijali

Yaani sisi watu wa ajabu sana. Unaweza kuta huyu aliyeanzisha hii mada pia huwa analia na kupiga magoti akiwa faragha na mwenzi wake Ila hapa kwa vile yupo nyuma ya keyboard anajifanya yeye mgumu. Sasa tunamsema Pilipili kwa vile tumemuona vipi kuhusu sisi tusiyewahi kuonwa. Kulia si tatizo kwani kila mtu anareaction zake kwa kila jambo linalomtoke katika maisha hivyo unavyomuona pilipili boya pia wengine wanakuona boya

Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji23] ushasema ni faragha babu faragha ni tofauti na hadhara kupiga goti c shida sasa unalia kwamba umepata bahati ya kuwa naye au vp wakulia ni mwanamke maana kuolewa kwa sasa imekuwa bahati.
Wanaume wanaenda kwa waganga kutafuta pesa, wanawake wanaenda kwa waganga kutafuta wame angalia tofauti iyoo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kulia mbele ya mwanamke, kumlilia mwanamke au vyovyote tu......!!

Msingi mkuu wa tendo ni kulia kwa sababu ya mapenzi' kwa mtazamo wa kawaida haileti maana nzuri hasa unapofanya tendo hilo mbele za watu,

Ila mtazamo wangu unaweza kua tofauti kidogo na mawazo ya walio wengi.... Katika mapenzi kila mmoja ananamna yake ya kupenda na kuexpress hisia zake kwa anae mpenda.

Wanaume tulio wengi huwa tunatoka katika uhalisia wetu linapo kuja swala la kuwasilisha hisia zetu kwenda kwa wale tunao wapenda, ni kitu kizuri maana kinamfanya mwanamke aione thamani na umuhim alionao kwako, na kila mmoja humuona mwenzie kapotea kwa anayo yafanya, kumbe hata yeye nae alitenda yasiyo faa kutendwa wakati akimfukuzia huyo alienae sasa.... kitu muhim ni kuto kuishi hivyo kwa kipindi chote cha mahusiano yako, usipo badirika lazima uje ujutie ulicho kitenda.

Baada ya mlengwa kukuelewa rudi katika misingi sahihi ya ki uanaume, kujali, kuheshim, kuthamini na kutimiza wajibu, na muhim zaidi ni kusimamia nidham ya familia.
 
Hisia sahihi za mtu huwezi kuzijua, ni kitu kipo ndani yake. Hisia si za mapenzi tu, hisia zipo za namna nyingi... Amini hata mchumba wake atakuwa alimuuliza hapo baadae wakiwa faragha, wame-relax... "...tell me darling, what happened, le' me know why you criiied!!.." Jibu kwa swali hili laweza lisieleweke kirahisi, hivyo dawa yake ni 'kupiga kimya' tu. Mc Pilipili atakuwa zwazwa kama alilia 'mapenzi' tu kwa mchumba wake.

Lakini kama alikumbuka kwa mfano, kauli fulani aliyowahi kupewa na mamake kama wosia, ama kejeri iliyomkwaza kutoka mpezi wake wa zamani aliyemgharimia kisha akamtosa kwa dharau...au jambo jingine ambalo kimsingi analifahamu na kulielewa yeye mwenyewe, nitamuunga mkono. And it's healthy, by the way.

Wengi wetu tunapenda kuwa watoa hukumu kwa wenzetu, sioni kama ni sahihi.
Toa ujinga wako hapa na utokwe na pepo la upumbavu kichwani mwako we kijana.

Baba yako naye alimlilia Mama yako hivi hivi mbele za Wakwe kumvalisha Mkewe pete ya ndoa?

Biblia inasema "MLEE MTOTO KATIKA NJIA IMPASAYO NA KAMWE HATAIACHA HATA ATAKAPOKUWA MZEE", inamaanisha ndivyo Wazazi wako walivyokulea hivyo?

Hata ile kauli ya "JIKAZE MTOTO WA KIUME" hauwezi kuitumia mbele za Watu ili ufiche upumbavu wako?

MC Pilipili ndiye wa kwanza kuwa na hisia sana za kupenda kupita kiasi duniani hadi ashindwe kujitambua na kuelewa matokeo ya kuzidiwa na hisia mbele za Watu?

Wewe na MC Pilipili ni mataira sana ambayo hayajawahi kutokea duniani na hayatatokea hadi dunia itapoangamizwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kazi ya moyo ni kusukuma damu, hayo mambo mengine mnajitakia wenyewe.
 
Mbona wanaume wengi mnalilia na kusemasema na miguno miiiingi wakati wa kuchikuchi? Bora alie sasa akatulie wakati wa kazi sio mlionyamaza wakati ule na mnalia kila siku sasa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanza huo utaratibu n wa kimagharibi Mimi namvisha akiwa amekaa yeye au laa namnunulia atajivisha yeye mwenyewe...huuu kiukweli n ujinga na haifai kwa kijana wa kiume kua dhaifu namna hio
Atajivisha mwenyewe? [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Kweli konki likwidii konki fayaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haka kajamaa kama kuna watu wanakafaham leo hii Wanaume wa Humu ndani Tupitishe Muswada/Azimio tukatenge haka kajamaa kanakodharirisha wanaume halisi hivi.

Naomba nilete huu mswada kwenu tuangalie kama akidi itatimia tukatenge kapumbuvuu kabisa haka. Kana mpa dada wa watu kazi ya kukabembeleza. Naye huyu dada anapatikana wap nimcheck?
Huyu sio yule jamaa mchekeshaji kwenye stand up comedy?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Toa ujinga wako hapa na utokwe na pepo la upumbavu kichwani mwako we kijana.

Baba yako naye alimlilia Mama yako hivi hivi mbele za Wakwe kumvalisha Mkewe pete ya ndoa?

Biblia inasema "MLEE MTOTO KATIKA NJIA IMPASAYO NA KAMWE HATAIACHA HATA ATAKAPOKUWA MZEE", inamaanisha ndivyo Wazazi wako walivyokulea hivyo?

Hata ile kauli ya "JIKAZE MTOTO WA KIUME" hauwezi kuitumia mbele za Watu ili ufiche upumbavu wako?

MC Pilipili ndiye wa kwanza kuwa na hisia sana za kupenda kupita kiasi duniani hadi ashindwe kujitambua na kuelewa matokeo ya kuzidiwa na hisia mbele za Watu?

Wewe na MC Pilipili ni mataira sana ambayo hayajawahi kutokea duniani na hayatatokea hadi dunia itapoangamizwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu umehukumu kabla hujahukumiwa, ila nakusapoti kuwa mwanaume kulialia mbele ya wakwe ni udhaifu wa hali ya juu, baba mkwe anakuangalia unavyojiliza, baba yako anakuangalia unavyojiliza sijui wanakuonaje km baba wa familia anayefata, mfano sisi kabila yetu ukioa siku ya harusi baba yako mzazi anakuvesha kanzu unakaribishwa rasmi katika jukwaa la wanaume sasa siwezi kuelewa mila za kwao wanafanyaje ila hainiingii akilini wazee watamheshimu vipi kijana wakujilizaliza

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom