Ya MC Pilipili hayapaswi kufanywa na mwanaume rijali

Ya MC Pilipili hayapaswi kufanywa na mwanaume rijali

[emoji23][emoji23][emoji23] ndo uanaume kamili huo mkuu, pilipili kashasaliti kambi ya kiumeni so hatuwezi kumwelewa hata mtu anieleweshe vipi siwezi kuelewa hata kidogo hii swala la kujiliza mbele ya mwanamke eti mapenzi yamezidi hadi yanamwagika daah niwe oldschool tu ila hiyo inashusha nyota za kiumeni

Sent using Jamii Forums mobile app
🤣🤣Walimwengu mna matatizo muacheni SHARUKHAN WA TANZANIA.
 
[emoji4][emoji4][emoji4]
123031.jpeg
 
kulia kuna release tension,ndio maana wanaume mnakufa mapema ni sababu mnabeba mengi kifuni vyenu
Mamy hao wanao bisha hapa kulia kwa Mc pilipili wasikusumbue pengine wao wanalia kuliko Mc na kamasi juu. Mapenzi hayana komando, kulia, kucheka, kupiga chafya n. K, inatokea bila kutalajia.
 
Huyu MC pilipili nimemfuatilia ana trend zisizo za kiuwanaume na hii clip yake ya kumlilia mpenzi wake siku ya kumvika pete ni hitimisho la nilichokuwa namuwazia siku nyingi.
Namshauri hii clip aifute kwani itakuwa ni kadhia kubwa kwa watoto wake.
 
hii thread itawafanya waliotaka kupiga magoti wawavishe pete wachumba wao wasifanye hivyo kwa kuhofia kuonekana 'dhaifu'...jamani kupiga magoti na kulia ni expression how you feel...kusema kweli anayeliliwa hujisikia vizuri na yule anayelia anajiskia vizuri kumuonyesha jinsi anavyompenda na jinsi hafichi hisia zake juu yake…kwa kimombo ni 'affection'..kwa kweli ni gesture tu..UANAUME WA MC PILI PILI ANAYEJUA NI HUYO MCHUMBA WAKE..msimpake kaka wa watu matope mpaka aanze yeye na mkewe mtarajiwa kujishtukia...MC POLE POLE KAMA UNAISOMA HII TOPIC JUA ULICHOFANYA NI PERFECT NORMAL...
 
Why would a man's tears make me feel like am in control of him?

I would let him shed his tears because he is winning over some battle in his heart I may never get to know about.

Then I would lift up my King, dust his knees and let him lead us into the journey we are just beginning.

His bitter past got buried together with the tears he shed, when they touched the ground.

haha... if you say so....
 
Don't be quick to judge. You never know.

Hizi nyoyo zetu tunazotembea nazo bwana, acha zijifiche tu zimebeba mengi.

Huwezi jua huyo mdada ana impact gani katika maisha yake. Maybe its a dream come true, maybe she saved his life.... maybe he never thought he would ever be loved again after previous breakup.

Let him cry his heart out. Whatever is in his heart, his Lord understands better.
Ndiyo ulie??? Mc Pilipili ameonyesha ufala wa kiwango cha PHD

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yani kula mbele ya uchafu ndo uanaume una safari ndefu aisee

Sent using Jamii Forums mobile app
Umetafsiri kadiri ulivyosoma au umeanzia kusoma maoni yangu hapo tu. Hoja yangu ilikuwa hivi:Kuna vitu viwili huwa vinanishinda kuvitekeleza. Kutapika kwa hiyari/kujitapisha kwa nguvu na kulia kwa hali yoyote. Sikuhusisha uanamke au uanamume katika hayo. Nimeeleza hayo mambo huwa yananishinda tu. Nashindwa kukuelewa hiyo hoja kuwa eti ndiyo "uanaume" umeitoa wapi hadi uniwekee mdomoni!
 
Hili jambo la mwanaume kupiga goti wakati wa kumvalisha pete mchumba naona linazidi kukomaa,si utamaduni wetu japo sio mbaya sana kwani ni effects za globalization kwenye muingiliano wa kiutamaduni na wazungu/waarabu/wachina na vile tunasema "strong culture absorbs weak culture" na hii inachangiwa sana na nguvu ya kiuchumi.

Tuyaache hayo,leo Mc wa taifa Pilipili kama anavyojiita mwenyewe kamvisha pete mdada mrembo sana huko Boko Dsm hongera kwake but concern yangu kubwa ni kitendo cha yeye Pilipili kama Mwanaume kulia sana wakati kapiga goti mbele ya binti halaf binti anaonekana hana hata chembe ya hofu na kuguswa na kilio cha pilipili,huu ni udhaifu ambao kama.

Mwanaume lijali hakika hupaswi kuuonyesha,that is a big point of weaknes,hata kama umewahi kuumizwa sana kwenye mapenzi jitahidi usitoe chozi mbele ya mwanamke ambaye si mama yako,hii itakusaidia sana hata ukiwa kwenye ndoa ukitoa maamuzi yanakua ya kiume kweli kweli but hii ya kulia lia si dalili njema sana,kwa anayewajua vizuri wanawake atakua amenielewa.

By the way hongera sana Pilipili kwa kupata mchumbaView attachment 987138View attachment 987135
Mchekeshaji maarufu Bongo, MC Pilipili jioni ya leo amemvalisha pete ya uchumba mpenzi wake (Mke mtarajiwa) Philomena Thadey, nyumbani kwa Wazazi wa mwanamke maeneo ya Boko (Tegeta) jijini DSM, sherehe hiyo imehudhuriwa na watu mbalimbali wa Serikali na taasisi zisizo za kiserikali.

wa gogo ni washamba kuliko wasukuma.sio wote lakini
mc chachandu mbichi kachekesha watu baada ya kuchekesha visivyo chekesha.
tokea nizaliwa leo ndo na shuudia huyo jamaa utazani alikuwa anataka kuvishwa pete mbele ya watu gafla
 
Hahahahahahaaa! Dah! Ulimwengu hauishi vibweka. Yaani kakidume kamelia hadi kwikwi na mafua juu kwa sababu ya kutojiamini? Very disgusting! Nooo! Sikubaliani mwanaume kujiliza wala kupiga magoti kwa sababu ya hiyo kuvishana pete ya uchumba. Kulia aachie mashangazi!
 
Ila naona kama huyo mwanamke hajampenda mcpilipili, kaolewa tu ilimradi cariha
Ukiona kidume kinajiliza kimandazi namna hio ujue kuna walakini, huyo demu ni dhahiri kabisa upendo wake umeegama katika huruma zaidi na sio hisia. Yajayo yanafurahisha. Usiombe upendwe kwa kuonewa huruma maana siku hio huruma ikiisha unaweza tafta mti na kamba ukajimalize!
 
Mbona huyo dada mbona kama ana rangi mbili? Njano usoni na nyeusi kuanzia shingoni. Nauliza ndio mrembo mwenyewe?

Hio ya kupiga magoti na kulia ni utahira tu. Sema kila mtu huwa na kichaa chake ila tumezidiana tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom