Akili zako zimeishia hapo?
Unaweka vineno ndani ya JF, tena visivyokuwa na mwelekeo wowote; halafu unategemea viwe ndiyo njia ya kumwondoa Tundu Lissu gerezani?
Mwelekeo wa mada zako, ambazo kiuhalisia ni Vichwa vya mada tu visivyo ambatana na hoja nyuma yake zina mlengo fulani; kwa mtu anayejuwa kuzitafsiri.
Hazilengi kumsaidia Lissu wala CHADEMA wala Tanzania kuondokana na waovu waliopo madarakani.
Wewe ni kama mchokonozi tu unayesaidia kuonyesha hisia za wasomaji na wachangiaji.
Mada zako hazilengi kupambana na hao waovu zaidi ya kuwaonyesha njia za kupambana na waTanzania wanaotaka kujiondoa kwenye uovu wao..
Ukitaka kuelewa elewa; na nimemalizana nawe kuhusu hili.
Huna msaada wowote wa maana katika mapambano na waovu.