Yajue makundi manne ya dawa za kulevya & madhara yake

Yajue makundi manne ya dawa za kulevya & madhara yake

Kwenye mambo ya kiimani tunaamini kila kitu kipo kwa reason sasa wewe ukihukumu maamuzi ya muumba wako sijui akili yako inakuwa inafikilia nini kwa mfano sie tuliopiga medic idara ya pharm kila mmea ambao unafaida lazima utumike kusaidia watu hata pombe inatumika kusaidia watu hawa pombe kali kwenye kikohozi kikavu simple yaani
 
Zote zina compoud ya caffeine so hazina tofauti na tumbaku na mirungi zote ni CNS stimulant sema mirungi ni mild stimulant kwahiyo ni kali kuliko hizo nyingine
Tobacco ina nicotine ambayo unaweza kuchanganya pamoja paracetamol ukapata dawa nzuri ya mauvi
Mirungi ina cathinione inaweza kutumika kama euphoric effect kwa wazee na vijana ambao wako na mistress
Coffee ina caffeine pia unaweza changanya pamoja na paracetamol na asprin kwaajiri ya maumivu
Chocorate ina theobroma inaweza tumika kama dawa ya pressure ya kushuka(hypotension)
 
Kemikali yoyote au mchanganyiko ambao huleta mabadiliko ya kihisia na ufahamu ni dawa za kulevya.
Matumizi ya dawa za kulevya huleta utegemezi na usugu.

Utegemezi ni hali ya kushindwa kuishi maisha ya kawaida mpaka utumie dawa ya kulevya. Utegemezi huo huwa wa kisaikolojia na kiafya.

Kuna makundi manne ya dawa za kulevya

1. VIPUMBAZA

Vipumbaza ni aina ya dawa za kulevya ambazo hupunguza kasi ya ufanyaji kazi wa mfumo wa ufahamu. Mfano wa dawa hizi ni;
_ Pombe
_ Heroin
_ Mandrax nk

Unapotumia vipumbaza;
_ Kasi ya ufanyaji kazi wa mfump wa ufahamu hupungua.
_ Mapigo ya moyo hupungua.
_ Shinikink la damu hushuka
sana.
_ Kiwango kidogo huleta furaha
kubwa.
_ Kiwango kikubwa huleta
kizunguzungu, kuongea kwa
kuvuta ulimi, matendo yasiyo
ya busara, kuchanganyikiwa,
ubongo kushindwa kuratibu
mifumo mbalimbali ya mwili.

2. VICHANGAMSHO.

Hizi ni dawa za kulevya zinazoongeza kasi ya ufanyaji kazi wa mfumo wa fahamu.
Mfano wa dawa hizi ni;
_ Mirungi
_ Nicotine
_ Vidonge vya kupunguza hamu
ya kula.
_ Cocaine
_ Caffeine nk
Dawa hizi husababisha yafuatayo;
_ Kuongezeka kwa mapigo ya
moyo.
_ Ubongo kushindwa kuendesha
mifumo ya fahamu.
_ Kutokulala
_ Wasiwasi nk.

3. VILETA NJOZI.

hizi ni aina ya dawa zinazosababisha mtumiaji kuona maono au kusikia vitu visipokuwepo. Mfano wa dawa hizi ni;
_ Bangi
_ Uyoga (peyote, mescaline,
psilocybin)
_ LCD

Unapotumia vileta njozi mambo yafuatayo huonekana;
_ unasikia na kuona vitu
visivyokuwepo.
_ Kujiona unapaa.
_ Kuongezeka ukubwa wa
mboni ya jicho.
_ kubadilisha utambuzi nk

4. VIYEYUSHI.

Aina mbalimbali ya kemikali ambazo mvuke wake huweza kutumika kama kilevi. Mfano wa dawa hizi ni!
_ Petrol
_ Dawa za kuuwa wadudu
_ Dawa za kuondoa rangi za
kucha
_ Dawa za ganzi kama Nitrous
oxide, Propane, butane,
helium nk.

Matumizi ya viyeyushi husababisha yafuatayo;
_ Kuumwa na kichwa
_ Ongezeko ia hisia na
mwanga
_ Kupata njozi
_ Kizunguzungu
_ Mwili kukosa nguvu na hats
kuzimia nk

MADHARA (kijamii)

Watumiaji hukosa busara na umakini maishani hivyo kusababisha;
_ Magomvi na wazazi na
wanandoa.
_ Kushindwa kutunza familia
_ Ujambazi
_ Mauaji ya kikatili
_ Wizi nk

MADHARA (kiuchumi)

_ Kupungua kwa nguvu kazi
kwenye familia na taifa.
_ Kutumika vibaya kwa
rasilimali za familia na taifa
ktk kuwatibu waathirika.
_ Hasara itokanayo na uharibifu
wa Mali unaofanywa na
waathirika (ajali, fujo nk)

MADHARA (kiafya)

Utumiaji wa dawa za kulevya huambatana na matatizo mengi ya kiafya kama;

_ Saratani ya mapafu na damu
_ Kupungua kwa uwezo wa
damu kuchukua hewa (oxygen)
_ Kuharibika kwa mfumo wa
fahamu kunakoambatana na
ukiziwi, kichaa, kupungua
uwezo wa kukumbuka na
kufikiri, luppoza nk.

Pamoja na madhara hayo kwanini watu hawaachi kutumia dawa za kulevya?

Nawasilisha.
Na wewe unatumia ipi? Apo
 
Tobacco ina nicotine ambayo unaweza kuchanganya pamoja paracetamol ukapata dawa nzuri ya mauvi
Mirungi ina cathinione inaweza kutumika kama euphoric effect kwa wazee na vijana ambao wako na mistress
Coffee ina caffeine pia unaweza changanya pamoja na paracetamol na asprin kwaajiri ya maumivu
Chocorate ina theobroma inaweza tumika kama dawa ya pressure ya kushuka(hypotension)
Naona mfamasia umeingia kazini.
 
Na wewe unatumia ipi? Apo
Nilitumia vileta njozi na vichangamsho, lkn niliacha baada ya kunusurika ukichaa.

Nipo salama huu no mwaka wa tano tangu niache kutumia hizi dawa.
 
Nakushukuru mtoa mada .
Hulka asilia ya mwanadamu ni udadisi . Anapenda kuthubutu , na mara nyingi ukizuia kitu unamuongezea hamu ya kudadisi na matokeo yake yanaweza kuwa chanya au hasi .
 
Ndio niliwahi tumia uyoga mara moja ila cannabis naipenda sana japo situmii kila siku
Uyoga ni huuhuu au ni neno la kupunguzia makali kitu kingine kama "dawa" kwa cannabis? Kama ni uyoga kweli, nao imekuwaje uingizwe ktk kundi hili wakati ni mlo tu wakawaida?
 
Kwamba uyoga ni madawa ya kulevya....! Hii ni mpya kwangu (asante JF), kwa hiyo...huku vijijini sisi ni 'mateja' ama !? Maana kila msimu tunakula uyoga.
-----------
Ebu mleta mada fafanua kidogo juu ya hili.
 
Uyoga ni huuhuu au ni neno la kupunguzia makali kitu kingine kama "dawa" kwa cannabis? Kama ni uyoga kweli, nao imekuwaje uingizwe ktk kundi hili wakati ni mlo tu wakawaida?
Kuna uyoga aina nyingi sana upo hadi unatumika kutibia kikohozi ila huu niule wa mambo spiritual awake (recreational)psilocybin mushroom pia inajulikana kama psychedelic mushroom psilocybin mushrooms include Copelandia, Gymnopilus, Inocybe, Mycena, Panaeolus, Pholiotina, Pluteus, and Psilocybe. Over 100 species are classified in the genus Psilocybe. Psilocybin na hiyo ndio chemical compound yake ukila hiyo ni hatari euphoric yake na wamefanya uchunguzi hivi karibuni kuwa haina addiction
 
Vipi, unapatikana hapa nchini? Na kama upo utautambuaje?
 
Back
Top Bottom