Wanabodi,
Niko hapo Dodoma asubuhi ya leo kuja kuishuhudia kwa macho Rasimu ya Tatu, nimessafiria ungo, huko njia pia nikakutana na Waheshimiwa mawaziri 8 wa serikali ya JMT na wawili wa SMZ, wamejazana kwenye ungo huo huo, likija kutokea la kutokea kwa hizi nyungo kugomea njiani, one can not imagine!. Dar-Dom ni dakika 40 tuu!.
Kwanza rasimu bado, nimeambiwa na taarifa rasmi kuwa itakuwa tayari kesho, taarifa isiyo rasmi, hata kesho haitakuwa tayari!, what a waste kukimbilia Dodoma!.
Tukiwa njiani kwenye ungo wetu, nilipata fursa kuzungumza na Wanzanzibari ambao ni wajumbe wa BMK, kiukweli walinieleze kuwa kufuatia wajumbe wengi wa BMK wakutokea Zanzibar, wamekwenda Hijja, hakuna namna yoyote Akidi ya 2/3 kutoka Zanzibar, haiwezi kutimia!, hivyo asubuhi hii BMK, limeleta marekebisho ya kanuni, kuwaruhusu wajumbe wa BMK kupiga kura mahali popote walipo, iwe ni ndani ya ukumbi wa bunge au nje ya ukumbi, popote walipo, kwa sababu zozote.
Kanuni hii, pia itawaruhusu wana UKAWA, wasiokubaliana na misimamo batili ya vyama vyao kususia BMK, waweze kupiga kura za siri mahali watakapokuwepo!. Nimeshikwa sikio kuwa wana UKAWA, wamemuomba M/Kiti wa BMK, kuruhusiwa kupiga kura za siri wakiwa mafichoni!, wameeleza wamelazimishwa kususia kuhudhuria vikao vya BMK, kinyume cha ridhaa na utashi wao!, wamekubali tuu kususia kukubali collective responsibilities, kuepuka kuitwa wasaliti na kutengwa!.
Kama hili litafanyika, ni hakika 100%, AKIDI Itatimia!.
Katika jokes hizi na zile tukiwa ungoni, mjumbe mmoja wa BMK, alisema AKIDI lazima, itimie, isipotimia itamilizwa ili kuhalalisha ghara kubwa zilizotumika kwenye BMK hadi sasa!.
My Take.
Kama kura muhimu kuliko zote, ambayo ni uchaguzi wa Rais na Wabunge, Tanzania hatuna utaratibu wa kupiga kura nje ya kituo cha kupigia kura!, kisheria kura ni kama kutia saini kwenye mkataba, "the place of contract" ni very crucial, kama sheria ya BMK, ilisema BMK litapiga kura, neno BMK kisheria ni "the place" lilipo BMK!, ikimaanisha ni ndani ya ukumbi wa BMK tuu na sio mahali pengine popote nje ya BMK!.
Kura yoyote itakayopigwa nje BMK, sio valid vote!. Marekebiso hayo ni kuhalalisha tuu ile dhana ya AKIDI isipotimia!, "itatimilizwa!"
Wasalaam.
Pasco
Dodoma.
Mode: Hii sio yanayojiri, hii ni opinion article!.