Kwa hali inayoendelea huko bungeni, nina uhakika mpaka sasa raia wa nchi ya Tanganyika na Zanzibar wameshagawanywa kwa misingi ya uchama na bado kidogo tu tutaelekea kwenye ukabila maana udini tumeshajuana wabudha na wahindu na washaoline tempo. Kwa kuongezea bunge hili linachochea uhasama miongoni mwetu kwa misingi hiyo niliyoitaja hivyo kupelekea kuanza kuumizana wenyewe kwa wenyewe huku mitaani. Tumwombe Mwenyezi Mungu Mtukufu atuepushie hili balaa na atupunguzie hasira tuliyonayo juu ya uchama, udini, ukabila, nk nk. Amina.