Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, leo Novemba 4, 2019 kuanzia majira ya saa tatu na nusu (3:30) asubuhi atawaapisha viongozi mbalimbali aliowateua hivi karibuni
Wanaoapishwa ni pamoja na;
1. Charles Edward Kichere kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (Controller and Auditor General – CAG)
2. Katarina Tengia Revocati kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe.
3. Mhandisi Aisha Amour kuwa Balozi wa Tanzania nchini Kuwait.
4. Kanali Francis Ronald Mbindi kuwa Kamishna wa Kazi katika Ofisi ya Waziri Mkuu
Aidha, Mhe. Rais Magufuli anawaapisha Majaji 12 wa Mahakama Kuu
*****
View attachment 1253571
IKULU: Charles Kichere akiapa kuwa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG) akichukua nafasi ya Prof. Mussa Assad aliyekuwa CAG kwa miaka mitano - CAG Kichere alikuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe na awali alikuwa Kamishna Mkuu wa TRA
UPDATES:
Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma: Leo ni siku ya shukrani na tunamshukuru Rais kwa kutuongezea nguvu kazi. Tumeweza kupata watu bora Namshukuru pia Msajili Mkuu wa Mahakama kwa utumishi uliotukuka Mahakamani na naamini akifika Njombe atafanya kazi zaidi
View attachment 1253651
Prof. Juma: Asante Rais kwa kutuongezea Majaji 12, tukiondoa Majaji 2 wenye majukumu maalumu, nguvu kazi inabaki ni Majaji 76 - Majaji 2 watastaafu mwisho wa mwaka na watabaki 74 na mzigo kwa kila Jaji kwa sasa ni mashauri 518 na uwezo wa kila Jaji ni mashauri 220
Prof. Juma: Majaji tumejiwekea utaratibu wetu katika utendaji. Mfano, kila mwaka tunatakiwa kutoa mashauri angalau 220 kila Jaji, kuangalia hukumu zinatoka kwa wakati - Tuna mfumo wa kujiangalia wenyewe na kwa kujiangalia tunakuwa tunarudisha imani tuliyopewa na Katiba
Spika Job Ndugai: "Mlioteuliwa leo mmepata imani ya Rais Magufuli. Na kwa vile Watanzania walimuamini Rais Magufuli, basi mmepata imani ya Watanzania. "Ndugai akitoa neno kwa wateule walioapishwa na Rais leo. "Nakupongeza sana Mhe.rais kwa teuzi hizi, nawapongeza sana walioapishwa leo, mna imani ya watanzania, mnalo jukumu kubwa, tunawategemeeni sana"
Spika Job Ndugai: "Niwapongeze walioteuliwa, mmepewa imani kubwa kwa walioteuliwa. Kwa kuwa sisi sote tulimpa imani kubwa Mhe. Rais Dkt. Magufuli mjue pia mna imani ya watanzania wote. "CAG Kichere karibu sana, sisi Bunge tunaanza shughuli zetu kesho za kuangalia mipango ya Taifa ambayo inaweka vipaumbele ambavyo vitaisaidia Serikali kuona ni aina gani ya Bajeti ya Serikali ambayo itakuja 2020/21, wewe CAG ndio jicho letu tunakutegemea."
View attachment 1253671
Spika Job Ndugai: "Hivi karibuni Mhe. Rais alitembelea Gereza la Butimba na kutoa maagizo, hata mimi huwa natembelea sana Gereza la Kongwa, nawaomba majaji mkafanye kazi yenu ili kila mtu apate haki yake, anayestahiki kukaa gerezani akae asiyestahiki atolewe na arudi uraini. "Jicho ndiyo kila kitu kwa Binadamu bila jicho hujui unaenda wapi kwahiyo wewe CAG ni jicho letu tunakutegemea kushauri kuona namna ya kurekebisha na taaarifa yako inapojadiliwa Bungeni huwa ni taarifa nzito, tunaahidi kukusaidia kazi yako ni nzito."
View attachment 1253656
Rais Magufuli: Nawapongeza wote mlioapa leo. Zingatieni viapo vyenu mlivyovisoma leo. Pia, mkamtangulize Mungu katika kazi zenu - Nimeambiwa mmoja wa Majaji walioapa leo alifiwa na mke wake wiki iliyopita. Kassim pole sana, roho ya Marehemu ipumzike kwa Amani
Rais Magufuli: Ndugu zangu Majaji kafanyeni kazi ya haki. Judgement huwa inatolewa na Mungu tu ila kwa hapa Duniani mpo ninyi - Katoeni hukumu kwa haki ila haki hizo pia msizicheleweshe kwa sababu changamoto zipo sehemu mbalimbali, Waheshimiwa wamesema hapa
Rais Magufuli: Nakumbuka Jaji, aliyekuwa kwenye Fair Competation (si ni wewe?), huyu wakati akifanya kazi alishaamuliwa kufukuzwa kwasababu alisimamia haki - Walikuwa wanamshangaa kuona Mchaga asiyependa rushwa. Kwasababu pale kwenye Fair Competation kuna kazi
Rais Magufuli: Nendeni mkatimize wajibu wenu, mkawatumikie Watanzania hasa wanyonge ambao haki zao zinapotea - Mkienda kufanya kazi vizuri mtaipunguzia Tume ya Haki za Binadamu mzigo. Kafanyeni kazi
Rais Magufuli: Kamishna wa Kazi nawe kasimamie kazi hivyo hivyo, pale kuna changamoto nyingi. Kawanyooshe Wizara ya Kazi - Malata alifanya kazi nzuri ndio maana nimekaa naangalia muda wote nikaona panafaa Mwanajeshi wenye Qualification. Usiende pale kazi zikawa za hovyo
Rais Magufuli: Kwa CAG mpya nakutakia kazi njema. Usiende huko ukajifanya Muhimili. Mihimili ni mitatu tu na umeiona hapa Mahakama, Bunge na Sisi wa Serikali - Katika Kiapo chako ni Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali, kwa hiyo mwenye Serikali yupo
Rais Magufuli: Kafanye kazi zako za ukaguzi vizuri bila kuonea mtu. Unapopewa kazi na Mihimili mingine kama Bunge, katekeleze. Usibishane nao - Ukipewa maagizo na Mahakama katekeleze, wewe ni Mtumishi. Lakini pia kasimamie hiyo ofisi, kasimamie watendaji wako
Rais Magufuli: Kuna baadhi ya watendaji wako wanapopewa jukumu la kwenda kukagua kwenye Balozi wanalipwa fedha hapa na wakifika kule wanaomba pesa - Sitaki nikutajie majina yao, wewe nenda kule kachambue mwenyewe kwenye ofisi hii. Ofisi ya CAG sio Clean kama mnavyofikiria
Rais Magufuli: Nenda ukapange nafasi za watu wako ili mauchafuuchafu haya ukayasafishe. Najua una Qualification nzuri tu na hatufanyi makosa ktk kuteua - Form 4 umetoka na Div. I, Form 6 Div. I. Hii ni kuonesha wewe ni Kipanga sio Kilaza. Ukachukua Shahada ya Sheria na Account
Rais Magufuli: Tunakuamini. Pia, una heshima, umetolewa kwenye Ukamishna Jenerali wa TRA hukusema neno, 'You're humble, very polite' ukaenda ukafanya kazi huko - Wapo wengine ukiwateua wanafikiri ni nafasi zao. Unampa U-DC ukimtoa ananza kulalamika, wakati hakulalamika ukimteua