Yaliyojiri Ikulu Dar: Rais Magufuli amtaka CAG Kichere kutojifanya Muhimili mwingine, amwambia anaweza kuondolewa hata akiwa na mwaka mmoja

Yaliyojiri Ikulu Dar: Rais Magufuli amtaka CAG Kichere kutojifanya Muhimili mwingine, amwambia anaweza kuondolewa hata akiwa na mwaka mmoja

Kuna idara iliyobaki huru? naona hakuna. Majeshi yote, Bunge, Mahakama, Watunmishi wote wa Uma. Labda waliobaki uhuru kwa 50% ni Wananchi ndio maana sanduku la kura linaogopwa.
 
I quote, "
Rais Magufuli: Nakumbuka Jaji, aliyekuwa kwenye Fair Competation (si ni wewe?), huyu wakati akifanya kazi alishaamuliwa kufukuzwa kwasababu alisimamia haki - Walikuwa wanamshangaa kuona Mchaga asiyependa rushwa. Kwasababu pale kwenye Fair Competation kuna kazi"

Wapo wasiopenda rushwa! Kumbe kwenye rushwa vipo vi-factors vya ukabila pia. Punguza hawa na unapunguza rushwa etieh?
Ktk vita ya wahujumu uchumi na wizi mbalimbali serikali ni wachaga wangapi walikamatwa?
tatizo mkiwa maofisini mnalemaa na kamwe hamjishulishi na kazi nyingine nje ya ofisi kwa ajili ya kipato cha ziada, ndio maana mnakalia kuona wengine wezi wakati mmekalia uvivu!
 
Kwahiyo Assad naye alikuwa fisadi?

Alafu mbona dingi anaongea kibabe sana
Anaongea utadhani nae atapita 2020
Namshauri CAG nae atumie rungu hilo kumshusha aanze na fedha zilizolipwa kutoka kwa wahujumu uchumi
 
Assad Atanyanganywa passport yake. Assad atavamiwa na document na electronic zote Atanyanganywa
 
Hii nchi kwa sasa kuwa na akili,mafanikio kiuchumi,nidhamu ya kazi/biashara/kilimo,utoaji, ni dhambi sana sana tena sana kama ukiwa mchaga!!?
Hii inchi kwa sasa kuteuliwa huku ukiwa na "merits" zote ni dhambi hasa hasa ukiwa Msukuma!!??
Tumefikaje hapa kama Taifa!? Wapi tumejikwaa tukaanguka!?
Miuu Wako wachaga wacha Mungu ingawa ni wachache wa kumulika kwa tochi lakini wapo.
 
Kicheere anaenda kukagua madudu yake TRA.

Wakati akitumbuliwa TRA tuliambiwa ali 'under perform'.

Sasa hivi kapewa kazi ya kukagua taasisi ambayo mwaka wa fedha uliopita yeye ndie alikuwa Mtendaji Mkuu wa Taasisi hiyo.

Siye Team TANROAD tunamtakia kila la kheri.
Umeamua kuhamia upande ule rasmi
 
Hv huyu Rais mbona ana maneno magumu namna hii, hajishtukii hata kidogo..?
 
Kwa sababu Serikali zetu kote duniani zinaongozwa Na binadamu ambao kiasili ni dhaifu,(Kwa sisi wakatoliki wakati wa Kwaresma huwa tunafundishwa kuwa Yesu alianguka Mara tatu msalabani, hiyo ni ishara kuwa katika ubinadamu wetu tu dhaifu na tunaweza anguka dhambini),tukakubaliana tuwe na Vyombo,sheria,kanuni Na taratibu za kuhakikisha katika ubinadamu watu tutasimamiwa na kudhibitiwa .

Katika udhaifu wetu huu uwezekano wa kwenda kinyume ni mkubwa kwani sisi ni binadam na ni dhaifu,tukakubaliana iwepo taasisi huru ambayo Kazi yake ni kukagua na kudhibiti utendaji kazi wetu hasa matumizi ya umma.

Uongozi bora ni pamoja kujenga taasisi huru ambazo zitakagua na kudhibiti hesabu za Serikali na namna pekee ya kuuthibitisha ubinadamu wako ni kukubali kuwa tupo dhaifu.

Mwalimu Nyerere aliwahi kusema mbali na udhaifu wa kibinadamu unapokuwa Kiongozi utazungukwa na Presha nyingi kama familia,rafiki,Ndugu,jamaa ambao wanaweza sababisha ukashindwa kutimiza wajibu wako vizuri,hivyo lazima kuwe na vyombo huru vitakavyokusimamia katika Kazi zako ili usianguke na umalize salama.
Ni wazi kabisa hata ATCL haitaweza kaguliwa na Kama ndivyo Basi ikatokea imekaguliwa taarifa yake itakuwa Haina Tena mashiko Kama kaguzi za nyuma tulizooea kuziona
 
"Kwa CAG mpya nakutakia kazi njema, usije ukaenda huko ukajifanya na wewe ni mhimili, mihimili ni mitatu tu na umeiona hapa, na katika kiapo chako nilikuwa nakisikiliza nafasi yako ni Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, kwahiyo mwenye Serikali yupo"- @MagufuliJP #MwananchiUpdates

"Katika maisha ya Duniani hapa huwezi kupewa mamlaka ya kuteua halafu usiwe na mamlaka ya kutengua, ukishindwa hivyo hufai kuwa Rais, CAG kasimamie kazi yako vizuri, mwenzako amemaliza miaka 5 yake, inaisha leo saa sita usiku, kesho nenda pale ofisini kayatoe mauchafu yaliyopo"-JPM
#KiapoIkulu
#MillardAyoIkuluUPDATES


Na katika kiapo chako (Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali) nilikuwa nakisikiliza, nafasi yako ni Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, kwa hiyo mwenye Serikali yupo, mwenye serikali yupo, kafanye kazi zako vizuri za ukaguzi bila kuonea watu.

Unapopewa maagizo na mihimili mingine kama Bunge katekeleze, usibishane nao. Ukipewa maagizo na mihimili kama Mahakama kaitekeleze, wewe ni mtumishi, wewe ni mtumishi.- Rais John Magufuli.
Kama kayasema haya hadharani je sirini kayasema yapi?

Kama anataka CAG awe upande wa serikali sasa unamkagiaje mtu uliye na maslai nae utamsaidiaje kulinda maslai ya umma?

Ivi CAG akiwa upande wa serikali nani atawasaidia umma kujua madhaifu ya serikali kwenye mapato na matumizi?

Ni kitu gani Magufuli analificha kwenye ukaguzi huru?

Kwanini mihimili yote anaifanya kuwa ya serikali?
Mkuu kwan kazi ya mkaguzi ni nn. Tuanzie apo kwanza. Hata jeshi tu sio mhimili lazima CDF atii amri anazopewa na wakuu.

Kazi ya CAG ni kumsaidia rais kujua matumizi na kumshauri namna bora ya ku manage matumizi. Kazi yake sio ku expose waliomteua bali ni kuwashauri namna bora.

Ukiwa kinyume na waliokuteua lazima wakutoe. Sasa ww uwe kinyume na rais, ambae kachaguliwa na wananchi, then uwe kinyume na bunge ambalo ndio wawakilishi wa wananchi, then pia uwe kinyume na mahakama. Sasa ww ni nani.

Yaan sasa utakuwa ww ni nan.
 
Alishasema yeye ndo mwenye serikali. CAG mpya keshaambiwa kuwa lazima atii
 
Na assad naye bado anapitia pitia vifungu vya katiba na sheria vilivyotumika kumsataafisha. Kazi ipo. Sijui hiyo saa sita atakuwa keshaondoa documents zake zote au bado atakuwa anapitia pitia vifungu vya sheria.
Asubuhi kesho profesa Assad hatakiwi kuonekana ofisini Kama Ana Cha kukabidhi akabidhi Leo kwa msaidizi wake.Mwenyewe kesho akiingia ofisini aikute tupu
 
Afu kuna wajinga wanadhani Magufuli atatoka 2020 au 2025
Huyu ndio keshakaa milele hatoki ngo
 
Angalia Orodha ya wahujumu uchumi kisha angalia majina ya wachagga ni wangapi?
Magufuli kamuapisha jaji mmoja, ambaye ni Mchagga na alikuwa fair competition. Anasema jamaa alivyo muadilifu hadi alipokuwa fair competition watu walikuwa wanajiuliza "Huyu ni Mchagga gani asiyependa rushwa?"

Alisema Makonda, kuwa Mengi alikuwa ni Mchagga wa pekee, Mchaga gani anaesaidia yatima, na leo baba naye amewakilisha mawazo ya wengi, walio kuwa kumbe watu wengi hushangaa wakiona Mchagga haibi, hapokei rushwa, na anasaidia watu.

Swali, Wachagga mlifikaje hapa, kwenye jamii kuwaona namna hii?
 
Back
Top Bottom