Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sasa amekuwa kama mcheza mpira vile: Ni rais wa mateuzi muda wote!
Ktk vita ya wahujumu uchumi na wizi mbalimbali serikali ni wachaga wangapi walikamatwa?I quote, "
Rais Magufuli: Nakumbuka Jaji, aliyekuwa kwenye Fair Competation (si ni wewe?), huyu wakati akifanya kazi alishaamuliwa kufukuzwa kwasababu alisimamia haki - Walikuwa wanamshangaa kuona Mchaga asiyependa rushwa. Kwasababu pale kwenye Fair Competation kuna kazi"
Wapo wasiopenda rushwa! Kumbe kwenye rushwa vipo vi-factors vya ukabila pia. Punguza hawa na unapunguza rushwa etieh?
Anaongea utadhani nae atapita 2020Kwahiyo Assad naye alikuwa fisadi?
Alafu mbona dingi anaongea kibabe sana
Katiba zinavunjwa hatarii duh
Nadhani sababu ashatoaNipo siti ya mbele hapa kusikiliza sababu za kushindwa kumwongezea CAG awamu ya pili.
Miuu Wako wachaga wacha Mungu ingawa ni wachache wa kumulika kwa tochi lakini wapo.
Hayo maneno yenu kila mtu na mfumo wake wa uongoziAnamuapisha MPISHI MKUU wa HESABU ZA SERIKALI
Umeamua kuhamia upande ule rasmiKicheere anaenda kukagua madudu yake TRA.
Wakati akitumbuliwa TRA tuliambiwa ali 'under perform'.
Sasa hivi kapewa kazi ya kukagua taasisi ambayo mwaka wa fedha uliopita yeye ndie alikuwa Mtendaji Mkuu wa Taasisi hiyo.
Siye Team TANROAD tunamtakia kila la kheri.
Ni wazi kabisa hata ATCL haitaweza kaguliwa na Kama ndivyo Basi ikatokea imekaguliwa taarifa yake itakuwa Haina Tena mashiko Kama kaguzi za nyuma tulizooea kuzionaKwa sababu Serikali zetu kote duniani zinaongozwa Na binadamu ambao kiasili ni dhaifu,(Kwa sisi wakatoliki wakati wa Kwaresma huwa tunafundishwa kuwa Yesu alianguka Mara tatu msalabani, hiyo ni ishara kuwa katika ubinadamu wetu tu dhaifu na tunaweza anguka dhambini),tukakubaliana tuwe na Vyombo,sheria,kanuni Na taratibu za kuhakikisha katika ubinadamu watu tutasimamiwa na kudhibitiwa .
Katika udhaifu wetu huu uwezekano wa kwenda kinyume ni mkubwa kwani sisi ni binadam na ni dhaifu,tukakubaliana iwepo taasisi huru ambayo Kazi yake ni kukagua na kudhibiti utendaji kazi wetu hasa matumizi ya umma.
Uongozi bora ni pamoja kujenga taasisi huru ambazo zitakagua na kudhibiti hesabu za Serikali na namna pekee ya kuuthibitisha ubinadamu wako ni kukubali kuwa tupo dhaifu.
Mwalimu Nyerere aliwahi kusema mbali na udhaifu wa kibinadamu unapokuwa Kiongozi utazungukwa na Presha nyingi kama familia,rafiki,Ndugu,jamaa ambao wanaweza sababisha ukashindwa kutimiza wajibu wako vizuri,hivyo lazima kuwe na vyombo huru vitakavyokusimamia katika Kazi zako ili usianguke na umalize salama.
Mkuu kwan kazi ya mkaguzi ni nn. Tuanzie apo kwanza. Hata jeshi tu sio mhimili lazima CDF atii amri anazopewa na wakuu."Kwa CAG mpya nakutakia kazi njema, usije ukaenda huko ukajifanya na wewe ni mhimili, mihimili ni mitatu tu na umeiona hapa, na katika kiapo chako nilikuwa nakisikiliza nafasi yako ni Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, kwahiyo mwenye Serikali yupo"- @MagufuliJP #MwananchiUpdates
"Katika maisha ya Duniani hapa huwezi kupewa mamlaka ya kuteua halafu usiwe na mamlaka ya kutengua, ukishindwa hivyo hufai kuwa Rais, CAG kasimamie kazi yako vizuri, mwenzako amemaliza miaka 5 yake, inaisha leo saa sita usiku, kesho nenda pale ofisini kayatoe mauchafu yaliyopo"-JPM
#KiapoIkulu
#MillardAyoIkuluUPDATES
Na katika kiapo chako (Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali) nilikuwa nakisikiliza, nafasi yako ni Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, kwa hiyo mwenye Serikali yupo, mwenye serikali yupo, kafanye kazi zako vizuri za ukaguzi bila kuonea watu.
Unapopewa maagizo na mihimili mingine kama Bunge katekeleze, usibishane nao. Ukipewa maagizo na mihimili kama Mahakama kaitekeleze, wewe ni mtumishi, wewe ni mtumishi.- Rais John Magufuli.
Kama kayasema haya hadharani je sirini kayasema yapi?
Kama anataka CAG awe upande wa serikali sasa unamkagiaje mtu uliye na maslai nae utamsaidiaje kulinda maslai ya umma?
Ivi CAG akiwa upande wa serikali nani atawasaidia umma kujua madhaifu ya serikali kwenye mapato na matumizi?
Ni kitu gani Magufuli analificha kwenye ukaguzi huru?
Kwanini mihimili yote anaifanya kuwa ya serikali?
Ukaguzi ukiisha ripoti inahaririwa na malaika mkuu Yohana kabla haijachapishwa.Ni wazi kabisa hata ATCL haitaweza kaguliwa na Kama ndivyo Basi ikatokea imekaguliwa taarifa yake itakuwa Haina Tena mashiko Kama kaguzi za nyuma tulizooea kuziona
Asubuhi kesho profesa Assad hatakiwi kuonekana ofisini Kama Ana Cha kukabidhi akabidhi Leo kwa msaidizi wake.Mwenyewe kesho akiingia ofisini aikute tupuNa assad naye bado anapitia pitia vifungu vya katiba na sheria vilivyotumika kumsataafisha. Kazi ipo. Sijui hiyo saa sita atakuwa keshaondoa documents zake zote au bado atakuwa anapitia pitia vifungu vya sheria.
yani CAG mpya anapewa vitisho live alafu kuna fisi wanashangilia.Hii ndio makada wa CCM wanaita vita na mafisadi?! Nigga?!!!!
Magufuli kamuapisha jaji mmoja, ambaye ni Mchagga na alikuwa fair competition. Anasema jamaa alivyo muadilifu hadi alipokuwa fair competition watu walikuwa wanajiuliza "Huyu ni Mchagga gani asiyependa rushwa?"
Alisema Makonda, kuwa Mengi alikuwa ni Mchagga wa pekee, Mchaga gani anaesaidia yatima, na leo baba naye amewakilisha mawazo ya wengi, walio kuwa kumbe watu wengi hushangaa wakiona Mchagga haibi, hapokei rushwa, na anasaidia watu.
Swali, Wachagga mlifikaje hapa, kwenye jamii kuwaona namna hii?